Je, ungependa zawadi ya Mtoto awe Wako?

Preciouss

JF-Expert Member
May 15, 2017
339
276
Habari wanajanvi

Nashukuru Mungu tangazo la kwanza lilipokelewa vyema na mhusika anachanganua kwa utulivu. Leo Kuna kitu tofauti kidogo na nimetafakali Sana kwa kina Kama Ni saidie huyu Dada kwa kupost au nimshauri kwa mdomo.

Lakini kutokana na jambo lenyewe nikaona nililete hapa kwenu wanajanvi kwani penye wengi hapakosi Mambo mema.

Ni hivi niliunganishwa na Mdada mmoja na Dada aliyepita wa tangazo lamchumba muislamu.Baada ya kusimuliwa kumbe unaweza mpata mfariji wa moyo kupitia hapa akaona Naye asikate Sana tamaa.

Ni kwamba alikosea mno mno kuanzisha maisha na mtu ambaye kumbe hakuwa tayari kwa maisha ya kifamilia Kama ambavyo aliniahidi na kumshauri ahamie kwake waanze kuishi taratibu zingine zikifuata kumbe Ni Kama aliingia kwenye tanuru la Moto.

Kwa maana bwana aliyempata Ni wale wababa ambao tayari kichwani mwake hayupo tayari kuishi na mtu kwa muda mrefu.

Kwa maana alishaishi na watu nyuma Kama watano wakaishia kutengana.
Sasa na huy bila kujua akaingia mkenge akidhani atambadilisha na kuwa Baba Bora matokeo yake Ni maumivu yasiyokwisha na tofauti tofauti kila kukicha.
Anaeleza.

Mara tu baada ya kuanza kuishi pamoja Kati ya vituko alivyowahi fanyiwa Ni pamoja na kuletewa mwanamke mwingine ndani siku akiwa anapika na walienda moja kwa moja mpaka chumba Chao wakaanza kufanya ngono akiwepo na kusikia kila kitu kitanda kikaanza kulia na miguno ya mahaba anasimulia

Na hata alipoenda chumbani mlango haukufungwa waliendelea tu na Mambo yao.(Akalia akuumia na hata alipotaka kuondoka alikwama wkt huo huo Mana hakuwa amejipanga kwa ghafra )bwana aliomba msamaha ya kwamba Hali Ile isingejirudia.Akaenda kanisani pengine Bwana ana pepo la ngono kutokana na historia yake ya nyuma akawa anamuombea kila uchwao na pia akaambiwa amvumilie na kwa kuwa anadai anampenda Sana akaamua kulifumbia macho.Hilo likapita.

Wakaendelea kuishi Ni vituko baada ya vituko ikiwepo vipigo mpaka Kuna wakati akiwekewa Hogo baada ya kutumia mguu pia....
Bwana hawezi kumsaidia kitu chochote hata Ile pesa ya salon au Mambo ya wanawake(Akidai si anafanya kazi)

Dada anafanya kazi na wanachangia wote mahitaji ya ndani lakini hata akiishiwa Kama ilivyo kwa waishio ndani hawezi msaidia Ni kumsimanga tu na ikitokea amemwazima hata elfu 3 ataidai kwa nguvu licha ya kwamba wanalala kitanda kimoja.

Kisa kingine bwana si mtu wa kujali hata kidogo mfano anaweza dada akaumwa na amemwacha ndani anaumwa lakini hata kupiga simu hawezi piga hata hawezi na akihoji anadai akiwa namtongoza mtu Mara ya kwanza ndo huwa na mzuka wa kupigapiga simu Ila wakianza kuishi wote hawezi na si watakutana nyumbani. (Dada ana Bima ya Afya lakini inaongelewa Ile Hali ya Mtu kaumwa Kichwa ghafra usiku au kusema akachukie Panadol Ni kitu hakipo.Kumbe katika historia ya nyuma Ndivyo alivyo kwa wanawake wote akidai tangu kuzaliwa mapenzi yalishaisha Sasa huenda alitendwa au ana sababu.

Mimi Nimeshangaa Sana Mana hata House Girl huwezi kumtreat hivyo Kuna ule ubinadamu wa chini kabisa ambao binadamu huwa nao hata kwa jirani.Ila akiumwa yeye anayehangaika naye Ni yeye kwa huduma zote
Na Mambo mengi ambayo hayawezi kuandikwa hapa kwa jili ya maadili.
Basi huyu Dada akaamua Basi inatosha (enough is enough) akaanza kutafuta Mahali pengine ambapo ataanza maisha upya aondokane na ukatili wa kihisia.
Sasa btn wkt anataka kumove on akawa hajisikii vyema akaamua kwenda hospitali Kama ilivyo ada ndipo akabainika ana ujauzito..

Bwana alipoambiwa hakuonyesha interest akidai ana watoto wengine wengi ambao Ni 3 alipoambiwa mwanzo kwa wamama wengine na akamwambia atajijua mwenyewe kwa kila kitu(imagine huyu Dada anapitia wakati gani.Wanawake waliopitia hali hii wanaelewa .

Sasa ameomba Sana Mana Clinic ataanza mwezi huu mwenyewe alidhani Ni bwana atabadilika na kuwa na familia alifanya na maombi kwa wingi Ila anaona wakati haujafika.

Na kwake hayupo tayari kutoa ujauzito pia anaona Ni BARAKA Kuna wengi wanatafuta hawajabahatika na Ni Kama mfariji wake kwa baadaye..
Sasa anaomba Kama Kuna baba umri kuanzia 40-46 anahitaji mtoto pengine hakuwahi kupata mtoto au anahitaji mtu wa Aina hiyo yupo tayari card ya Clinic kumuandika jina Baba mpya.Anahitaji mtoto wake atakayezaliwa awe na Baba mwenye mapenzi kwake na waishi Kama familia.

Nimejaribu kumuandikia kwa kirefu kwa maana atakayejitokeza asimuumize Mana alipo hayupo sawa kimawazo kihisia na hata kiutendaji kwa mawazo mazito.

Dada Ni mkristo ana ajira pia kabla hata ya kuanza kuishi na huyo bwana Ni mtu aliyekuwa anajitegenea na akiwa na future yake nzuri( a promising future) kwa maana ana Mambo Yake tu anayofanya mbali na ajira. Ila Kama ilivyo Ada kwa binadam uhitaji wa familia akadhani kapata kumbe alikutana na mtu asiyejua thamani ya wanawake hata angemuonyeshea upendo wa Aina gani (mfano anasema alijitengea kila mwezi awe anamnunuia mavazi ya kazini bwana awe anapendeza Lakini huyo bwana hajawahi hata kukosea kwa bahati mbaya kumletea nguo ya ndani na hata mwanaume akiambiwa anadai hajawahi mnunukia mwanamke kitu mna sio lazima au atanunua akija furahi.

Mana anadai ameshajaribu hata kumshawishi aanze kwenda kanisani ili walau aone maisha ya familia Ni mazuri kwa kuona wenzake huko kanisani au aone majirani wanavyoishi na akamsihi wanaume wengi Wana michepuko lakini Ni heshima usimuonyeshee yaani Ni wale wanaume ambao hata siku akienda kulala na mwanamke mwingine atarudi nyumbani na kujisifu mbele ya huyu Dada akidai mwanamke mwenyewe sijampa pesa aliyotaka yaani hawezi waza haya yatamwathiri vipi huyu ninayemwambia especially mwandani anayempikia anayemfulia anayemuuguza akiumwa anayesimama badala yake akiwa na shida. Lakini bwanahataki kubadirika licha ya miaka 47 anapenda Uhuru wa Leo kuwa na huyu na kesho huyu.Maisha ya familia hayataki yanambana.

Baada ya yeye kuniomba nimtangazie niliomba kuonana naye ana kwa ana kuona Hali halisi Mana kwa Njia ya simu sikuweza kumpata vizuri.
Baada ya kuonanana naye hata Mimi nilijisikia huzuni Sana na kwa Hali yake ya Sasa Ni mtu anahitaji faraja Sana au rafiki licha ya mwenza nilivyoona Mimi kwa Sasa..Maana anahitaji wanasaikolojia kwa hatua aliyofika.

Lakini option nyingine nilimshauri Ukikosa Usijali Mungu atakusaidia ukipata mwanao Lea mwenyewe Mana Wakati wa Mungu ukifika atakuja kupata wa faraja wa maisha yako.Mana Mimi huwa naamini kila binadamu kapangiwa fungu lake Ila Hali inayotokea Ni binadamu kutokujitambua na kukurupuka kuanza kuishi na mtu wkt hujamsoma vizuri matokeo yake mtu anaanza kuishi Kama mtumwa kwa unyonge mwingi.

Ni Bora aanze mwanzo kabisa na akaacha kila kitu kwa jili ya amani ya moyo.
Mana maisha anavyoishi Sasa Ni ya mateso Sana.

Sasa kwa atakayekuwa interested atakuja PM nitamuunganisha au hata kwa ushauri tu ili kumfariji mwenzetu anayepitia changamoto.
Aksante.
 
Itoshe kusema mleta mada ni dalali wa mapenzi maana nyuzi zake nyingi anawatafutia watu wapenzi,Hongera mkuu kwa kuwa dalali wa mapenzi!
 
Wewe ni Dalali ama?
Hapana Wala ukisoma hii Ni ya pili tu.
A ukweli mtaani huku Kuna Mambo mengi Kuna watu wanajiua kwa kukosa furaha to ya maisha.
Sasa unakutana na mtu unaamua kumfariji kwa njia unayoona anaweza akapata faraja.
Mfano yule Dada mwingine ameanza kutabasamu..
Na wengine hawana interest na mitandao
Najua someone somewhere atamfaa au hata kwa faraja
 
Ndefu sana
Najua buy Ni muda was kazi
Ukitulia sio ndefu especially Kama Ni msomaji was vitabu
Ukimaliza kazi ukitulia huku unakunywa Pepsi bardi ndo utasoma vizuri na kuelewa
 
Itoshe kusema mleta mada ni dalali wa mapenzi maana nyuzi zake nyingi anawatafutia watu wapenzi,Hongera mkuu kwa kuwa dalali wa mapenzi!
Hapana hata kidogo hii Ni ya pili na Mimi nipo humu miaka
Sema Kama nilivyosema Kuna Ile Hali unakutana mtu yupo so desperate Hali ya kukata tamaa uwezo wako unakushawishi walau umsaidie unapoweza
Hata wewe najua huwa unasaidia na si lazima kusaidia kuwe mfumo mmoja.
So nikaona huyu nimtafutue marafiki was kumfariji akipoa mengine yatafuata
 
Hapana hata kidogo hii Ni ya pili na Mimi nipo humu miaka
Sema Kama nilivyosema Kuna Ile Hali unakutana mtu yupo so desperate Hali ya kukata tamaa uwezo wako unakushawishi walau umsaidie unapoweza
Hata wewe najua huwa unasaidia na si lazima kusaidia kuwe mfumo mmoja.
So nikaona huyu nimtafutue marafiki was kumfariji akipoa mengine yatafuata
Vipi tukikutaka wewe mwenyewe taratibu zikoje,? Tunaweza kuja PM?
 
kuna mtu anatafutwa hapa!!
fbi gifs | WiffleGif
 
Dah mpe pole Sana ....

ila usikute hapo kuna mtu alikua anampenda kweli hapo mwanzo ila akamzingua akakimbilia huko ....matokeo yake ndo hayo...

haya mambo hayana formular aisee
 
kuna mtu anatafutwa hapa!!
fbi gifs | WiffleGif
Mtu gani atafutwe kwa njia hii.
Ina maana hata wewe ukijitolea kuwa rafiki wa kawaida au ushauri ndo unatafutwa.
Watu wengine huogopa kutoa ya MOYONI. Mwao na kujifia ndani kwa Sampuli ya watu Kama nyie.
Maana kutwa Ni kutafuta negative na ukosoaji mdogo mdogo hata sehemu isiyohusika.
Sasa mfano hapa JF Ni Mtandao mpana na sidhani Kama wote waliomo humu watapitia uzi huu kwa dhamira uliyosema
Na mtu gani na amefanya Nini atafutwe kwa njia hiii.Au kakosea Nini
 
Dah mpe pole Sana ....

ila usikute hapo kuna mtu alikua anampenda kweli hapo mwanzo ila akamzingua akakimbilia huko ....matokeo yake ndo hayo...

haya mambo hayana formular aisee
Kabisa haya mambo Yana karma....asipokaa chini akajuta na kutubia hyo karma itamtafuna Sana..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom