Ndege Tausi
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 992
- 476
Tangu jana amenuna kisa...
Muda sasa umepita tangu awe na mawasiliano na wanawake wawili, mmoja ni binti wa miaka 24 ambaye alinitambulisha kuwa ni mtumishi mwenzake anayefanya kazi kwa kujitolea, na mwingine mama wa makamo ambaye ni kiongozi mwenzake katika michezo.
Wanawake hawa wamekuwa wakimpigia simu kila mmoja kwa wakati wake. Kinachonitia shaka na kunipa hisia kuwa labda ni wapenzi wake ni mawasiliano ya mara kwa mara na namna anavyoongea nao.
Mara zote wanapompigia simu hutaka kufahamu mahali alipo na wakati mwingine kumlaumu wanapompigia na kukuta simu yake ipo bize. Huwa nayajua haya kutokana na anavyokuwa anajitetea.
Huwa anapokea simu na kuongea na mimi nikiwepo bila hofu kwani nikimuuliza huyo ni nani hujibu kuwa ni yule binti au wakati mwingine yule mama.
Sasa jana binti kapiga na kumuuliza maswali hayohayo, nikaona bora nimuulize ili aniondoe shaka. Kilichofuata hapo ni kununiwa hadi sasa asubuhi kaondoka bila kuniaga.
Naombeni mnisaidie mawazo. Je ungekuwa wewe isingekuuma ?