orangutan
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 757
- 773
Habari Wakuu,
Katika jamii ya Kitanzania kama sio Africa nzima tumekuwa tukishuhudia watu wanaobahatika kuongezeka ukubwa wa mwili pamoja na kuota vitambi wakisifiwa na kuonekana kama wametusua kimaisha hivi.
Hata leo hii wewe uliekuwa kimbaumbau halafu baada ya kipindi fulani ukaanza kutoka mashavu na kuota kifriji tumboni utaona raia wanavyoanza kukupongeza na kufurahia hayo mabadiliko yako ya kimwili.
Swali ni kwamba, Je ni kweli ubonge ni kitu cha kukishabikia na kutoa hongera kwa wale waliofanikiwa kuukimbia ukimbaumbau na kuwa vibonge? Hasahasa tukijaribu kuangalia na namna ambavyo ubonge unavyohusianishwa na maradhi mengi huku vibonge wengi wakitenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kwenda gym na kufanya 'diet' ili kupunguza ukubwa wa miili yao.
Maoni yenu wadau.