Je, Unene ni ishara ya mafanikio?

orangutan

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
760
771
Habari Wakuu,

Katika jamii ya Kitanzania kama sio Africa nzima tumekuwa tukishuhudia watu wanaobahatika kuongezeka ukubwa wa mwili pamoja na kuota vitambi wakisifiwa na kuonekana kama wametusua kimaisha hivi.

Hata leo hii wewe uliekuwa kimbaumbau halafu baada ya kipindi fulani ukaanza kutoka mashavu na kuota kifriji tumboni utaona raia wanavyoanza kukupongeza na kufurahia hayo mabadiliko yako ya kimwili.

Swali ni kwamba, Je ni kweli ubonge ni kitu cha kukishabikia na kutoa hongera kwa wale waliofanikiwa kuukimbia ukimbaumbau na kuwa vibonge? Hasahasa tukijaribu kuangalia na namna ambavyo ubonge unavyohusianishwa na maradhi mengi huku vibonge wengi wakitenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kwenda gym na kufanya 'diet' ili kupunguza ukubwa wa miili yao.

Maoni yenu wadau.

20111217_MAP044_0.jpg
 
Attachments

  • 20111217_MAP044_0.jpg
    20111217_MAP044_0.jpg
    10.9 KB · Views: 54
Tatizo ni dhana iliyopo kwenye jamii zetu kuanzia ngazi ya familia!

Tafsiri ya mafanikio hutokana na mtu anavyo ifafanua kichwani mwake!

Kuhusisha unene na mafanikio sidhani kama ni sahihi!

Binafsi huwa napata tabu sana pale napokutana na mtu kisha akanishangaa eti nimekonda! wakati tangu nipate akili sijawahi kunenepa!

Wakati fulani mtu aliwahi kuniona tu kwenye luninga na kuna nyakati camera hukufanya uonekane mnene kiasi au mweusi/mweupe nk. akastaajabu kwamba kajitu kenyewe ndio haka kembamba kana mwili mdogo! sijui alidhani ntakua na mwili tembo au nyati!

Jamii zetu zina tudharau kweli vimbau mbau!

Ingekua ni mimi mjadala huu ninge uweka hivi: Nini kipimo cha mafanikio?
 
M

Mijitu mingi / asilimia kubwa, ikinenepa kupita kiasi huwa naona inakuwa mipuuzi puuzi tu hata uwezo wa kufikiria unakuwa duni,sijui ni kwa nini.Hata kufa kwao mingi huwa inafia chooni ikiwa inak...nya, yaani ni Ghafla pwaaa!
 
Mimi masikini wengi huwa nawaona ni wembamba, na baadhi ya matajiri nawaona ni wanene sasa mimi huwa napata Picha kuwa kuna uhusiano fulani kati ya unene au wembamba na kipato cha mtu
 
vimbau mbau wakinona raha bhana dalili ya pesa kama mi nakaribia kuachana na jina la miss nishaaanza kuwa kbonge nyanya
 
M

Mijitu mingi / asilimia kubwa, ikinenepa kupita kiasi huwa naona inakuwa mipuuzi puuzi tu hata uwezo wa kufikiria unakuwa duni,sijui ni kwa nini.Hata kufa kwao mingi huwa inafia chooni ikiwa inak...nya, yaani ni Ghafla pwaaa!
Hahaha! kwenye uwezo wa kufikiri plus Upuuzi (nadhani umbea umo ) hayo mengine uliotaja sina hakika nayo!
 
Wakina Bill, Mark, Dewji na matajiri wengi tu wao hawana vitambi wala sio wanene.

Sasa na kamshahara kako ka Laki nne miezi miwili tu tayali umefutuka na likitambi juu, huko ni kuridhika kimaskini.

Unene sio mafanikio bali ni kujiendekeza kwa mtu mwenyewe!
 
Unene ni maradhi kama yalivyo maradhi mengine.
Hata wanawake wabaya wengi ni wale wanene...........umewahi kumwona mlimbwende bonge?
 
M

Mijitu mingi / asilimia kubwa, ikinenepa kupita kiasi huwa naona inakuwa mipuuzi puuzi tu hata uwezo wa kufikiria unakuwa duni,sijui ni kwa nini.Hata kufa kwao mingi huwa inafia chooni ikiwa inak...nya, yaani ni Ghafla pwaaa!
Ha ha eti ikiwa inakunya
 
Unene ni maradhi kama yalivyo maradhi mengine.
Hata wanawake wabaya wengi ni wale wanene...........umewahi kumwona mlimbwende bonge?
Ha ha ha hakunaga mlimbwende bonge..sijawahi kuwa na mwanamke bonge hata kuwatongoza tu nawaogopa
 
Ha ha ha hakunaga mlimbwende bonge..sijawahi kuwa na mwanamke bonge hata kuwatongoza tu nawaogopa
Tatizo la wengi ni kuwa misinformed. Uongo unakuwa ukweli na ukweli unakuwa uongo.
Kuna mengine huwa yanajichubua ili kuwa warembo mwishowe wanaanza kuwa na rangi zote za bendera ya taifa.
 
Ushamba wa wabongo wengi,,, yani ukishika hela kidogo tu, unafutuka hatari, mi najaribu kumwangalia Diamond naona ni mfano tosha wa jinsi mwanaume unapaswa kuwa, sio unanenepeana ovyo tu. Ova
 
ndivyo baadhi ya jamii ya tanzania inavyoona ukiwa mnene unapesa kitu si sawa kabisa
 
Mimi masikini wengi huwa nawaona ni wembamba, na baadhi ya matajiri nawaona ni wanene sasa mimi huwa napata Picha kuwa kuna uhusiano fulani kati ya unene au wembamba na kipato cha mtu
Check watu kama Aliko Dangote,Mohamed Dewji,Reginald Mengi,Diamond Platnum,Bill Gates?
Halafu mwanaume ukinenepa sana ka shafti kanakuwa kadogo utafikiri kitovu,wengi wanaishia kupigiwa tu na mashamba boi wao,watu wanabaki kusema ohh wanawake wengine ovyo kabisa,nyumba kajengewa,gari kanunuliwa na miradi kafunguliwa ,vyakula ndani kibao ,matunda kwenye friji hayakatiki,wewee,watu wanahitaji matunda ya kwenye boksa.
 
Tatizo la wengi ni kuwa misinformed. Uongo unakuwa ukweli na ukweli unakuwa uongo.
Kuna mengine huwa yanajichubua ili kuwa warembo mwishowe wanaanza kuwa na rangi zote za bendera ya taifa.
Mkuu usipotee please,hebu Ongelea mijamaa yenye mitumbo mikubwa utafikiri imebeba mizigo ya mwizi,na mashavu manene utafikiri kameza paka wa muhimbili,achana na hawa wauza sura wenye rangi za kuchovya na kubandika vi-plastic hairs akiwa anaongea anatikisa vinywele kawa wazungu wakati hakuna kitu nyambafu zao mimavi tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom