je unene ni afya au ugonjwa

click

Member
Feb 9, 2012
7
1
mi nina swali ambalo nashindwa kulipatia uvumbuzi je unene au kuwa na mwili mkubwa ni afya au ugonjwa.kwa sab wengine wanasema flan ana mwili ana afya.na wengne kukonda wanaona ni kutokuwa na afya.ukweli upo wapi hpa?.
 
Kila kitu kikizidi ni hatari. Uzito wa mwili wako unatakiwa uendane na urefu wa mwili wako kuna formula ambayo uwa inatumika na ikizidi kiwango fulani ni hatari kwa afya yako kwa kuweza kupata magonjwa kama vili cholestrol na moyo, ingawa mimi siyo daktari ninafahamu kwa kusoma. Nimeisahau hiyo formula, wanaoifahamu watatujuza.
 
Obesity ni ugonjwa,what is obesity? Refer to BMI.

Kujua BMI ni kitu muhimu sana.Hii misemo ya ''jamaa ametoka shavu kapendeza sana'' wakati hilo shavu haliendani na urefu wake ni hatari sana.Obesity hupata mwanya katika hali ya kutojua BMI.
 
MSAADA JAMANI: Nina imani watu tunapendana na lengo la kuishi ni kwamba mwisho wa siku tufike mbinguni. MADA: Nina mchumba ambae tumedumu kwa mda mrefu na tumeazimia kuoana. Yeye ni roma mimi msabato yeye hataki kubadili dini. Je mimi nifanye nini?
 
Bosco massawe;3347526]MSAADA JAMANI: Nina imani watu tunapendana na lengo la kuishi ni kwamba mwisho wa siku tufike mbinguni. MADA: Nina mchumba ambae tumedumu kwa mda mrefu na tumeazimia kuoana. Yeye ni roma mimi msabato yeye hataki kubadili dini. Je mimi nifanye nini?

mbona ww hutaki kubadili au ya kwako ndio ya kwenda peponi?ushauri wa bureeeee kafungeni ndoa kwa DC mpate kibali cha kuzini.
 
unene sio ugonjwa sawa na vile wembamba sio uzima,vyote inategemea. huwezi kuhitimisha hata kama ww ni daktari kwa kusema unene ni ugonjwa,ukimaanisha kuwa wembamba ni uzima,japo hatari kubwa ya kuwa na mgonjwa ya tabia ipo zaidi kwa watu wanene kuliko watu wemba. Ukweli ni kwamba wembamba si kitambulisho cha afya njema wala sio kinyume chake...
 
MSAADA JAMANI: Nina imani watu tunapendana na lengo la kuishi ni kwamba mwisho wa siku tufike mbinguni. MADA: Nina mchumba ambae tumedumu kwa mda mrefu na tumeazimia kuoana. Yeye ni roma mimi msabato yeye hataki kubadili dini. Je mimi nifanye nini?

Mbona kama haina uhusiano na mada iliyopo hapo juu!!au nawe mchumba'ako nimnene pia?
 
Sio kila unene ni ugonjwa, wala sio kila wembamba ni afya au ugonjwa. Ukweli ni kwamba kuwa mnene sana kunaweza kukuletea madhara mengi yakiwemo magonjwa ya Moyo. Ikiwa una ugojwa wa kisukari, utashauriwa kupunguza uzito kwa sababu hii ina madhara katika ufyozwaji wa sukari kutoka kwenye utumbo mdogo kuingia damuni. Yapo madhhara mengine mengi, ila kwa kifupi kujua kama unene au wembamba wako ni afya, tumia fomula ya kutafuta BMI:

Yaani,
BMI = Body weight (kg)/ Height (m[SUP]2 [/SUP])
Jibu utakalopata linganisha na categories hapa chini, ujue ulipo.

BMI Categories:

  • Underweight = <18.5
  • Normal weight = 18.5–24.9
  • Overweight = 25–29.9
  • Obesity = BMI of 30 or greater
Kila la heri.
 
Ndugu Ambitious naomba unifafanulie unaposema Obesity hupata mwnya katika hali ya kutojua. je,unamaanisha mwanya wa kwenye kinywa??
 
Ndugu Ambitious naomba unifafanulie unaposema Obesity hupata mwnya katika hali ya kutojua. je,unamaanisha mwanya wa kwenye kinywa??

Uwii jamani kiswahili kigumueeeh. Wewe si unajua mwanya, mwaya si una nafasi au uwazi katika meno mawili ya mbele. Sasa hapo kilichomaanishwa ni kuwa unene unapata nafasi endapo hujui BMI. Mimi sijui kutafsiri BMI in swahili.

Unene ni maradhi, jaribu kumaintain BMI not above 25
 
Back
Top Bottom