Je unayajua makabila ya wazungu?

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
309
500
Ni swali pengine wengi wetu tumekuwa tukijiuliza kama ilivyo kwetu sisi waafrika na waarabu Je,wazungu(Europeans) makabila yao ni yapi? Nini kilitokea kwa makabila hayo?

Ukweli ni kwamba wazungu wanamakabila,miungu,mila na desturi kama ilivyo kwetu sisi.

Kuna rafiki yangu hupenda kuniambia hawa jamaa (Wazungu) kama wangekuwa hawana “ndumba” wasingewaweza wazee wetu na kiwapiga mijeredi na kuwafanya watumwa! Wangewalaza nje na kuwafanyia vibweka vyote vya kichawi.

Katika uzi huu wa kwanza nitakuletea majina ya makabila hayo na asili yake (maeneo yalikokuwa yanapatikana) na wakati mwengine nikihitimisha na hali ya makabila hayo kwasasa.

Moja kwa moja niingie kwenye uchambuzi ;

GAULS
Maarufu kwa jina la Gallic
Jamii hii inahusisha makabila matatu ya Celtae (Galli), Belgae na Aquitani
Usiwachanganye na Gaels

IMG_1990.JPG

Walikuwa jamii ya koo mbalimbali isiyokuwa na mfumo wa kifalme lakini waliweza kuunganisha nguvu na kukabiliana na adui zao pale ilipowabidi kufanya hivyo na walifanya hivyo kwenye vita za Telamon ya mwaka 225 BC na vita za Gallic miaka ya 50s BC.

IMG_1980.JPG

Gauls chimbuko lao kulikuwa kwenye Karen ya 5 BC katika maeneo ya La Tène kaskazini mwa Alps na wakisambaa katika eneo lote la Seine,Middle Rhine na upper Elbe ) mpaka inafika karne ya 4 BC walishafika maeneo kwasasa yakijulikana kama Belgium ,Ufaransa,Ureno,Australia,Uswiss,Slovakia,Jamuhuri ya Czech,Uhispania na Ujerumani ya kusini.

IMG_1979.gif

Kiuchumi walikuwa wakimiliki njia za biashara kuzunguka eneo la mito Rhône,seine,Rhine na Danube na hii iliwafanya waweze kujitanua mpaka maeneo ya Kaskazini mwa Italia,Transylvania,Ugalatia na Balkan

Kwasasa wanajulikana kama watu wa jamii ya Celtics.

IBERIAN
Jamii hii inajumuisha makabila yapatikanayo katika Penisula ya Iberia hapa tunakutana na watu wa Roman Hispania ambayo ndiyo Ureno ya sasa ,Uhispania na Andorra yapo makabila mengine yanayoshabihiana na jamii hii kiutamaduni na desturi.

IMG_1981.JPGIRISH
miongoni mwa makabila ambayo pengine tamaduni zao bado zipo kwa sehemu mpaka sasa ni hii ya ki Irish.

Jamii hii inapatikana ulaya ya visiwani na inasadikika chimbuko lake ni watu wa Gaelic.

Tofauti na watu wa Gaelic hawa walikuwa na ufalme ulijulikana kama túatha, ambao pia uliimarika katika makundi matano ya Old Irish cóiceda, Modern Irish cúige hii ikijumuisha makabila ya Ulaid (upande wa kaskazini ), Connacht (upande wa magharibi ), Laighin (upande wa mashariki), Mumhan (upande wa kusini ) na Mide (katikati ).

Kutokana na kukua kwa kasi mara nyingi kulitokea vita katika maeneo haya na mfalme Norman alifanikiwa kutawala sehemu kubwa ya eneo hili

IMG_1982.JPG
IMG_1984.gif
IMG_1985.JPG
IMG_1983.gif

IMG_1986.JPG

MAKABILA YA BRITAIN
katika zama za Chuma.Makabila kadhaa yaliandikwa na wanahistoria na wanajiographia kama Ptolemy. Asili kubwa ya watu hawa iliaminika kuwa ni watu wa Celtics.

IMG_1988.JPG

IMG_1989.JPG

IMG_1987.JPG

GERMANIC
Jamii hii inahusisha makabila ya Teutonic,Suebian na Gothic jamii hizi hufaamika kama “European ethnolinguistics” kutoka kaskazini mwa Ulaya na hutambulika kwa kuzungumza Germanic historia yao huanzia millennium ya 2 BCE hadi sasa.

IMG_1991.JPG

Jamii hii inasadikika walichipukia kipindi cha Nordic Bronze ambayo ilitukia wakati wa vita ya Axe culture kusini mwa Scandinavia na hapo baadhi ya makabila ya kijerumani wakaanza kusambaa kuelekea kusini na kupeleka vita vikali na watu wa Celtics na Roma ya zamani na ni kutoka kwa watu wa Roma jina la Germanic lilipopatikana .

Walikuwa wakiabudu mungu Odin.

Jamii hii ndio inasadikika kuwa walikuwa kiboko kwa warumi kwani waliweza kuwapiga vibaya Arminius katika misitu ya Teutoburg 9 CE.
Walikaa maeneo ya Rhine na Danube kwa sehemu kubwa.

Wakati mwengine tutaona nini kilitokea kwa makabila haya/jamii hizi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
mtu kitu

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
570
500
Ni swali pengine wengi wetu tumekuwa tukijiuliza kama ilivyo kwetu sisi waafrika na waarabu Je,wazungu(Europeans) makabila yao ni yapi? Nini kilitokea kwa makabila hayo?

Ukweli ni kwamba wazungu wanamakabila,miungu,mila na desturi kama ilivyo kwetu sisi.

Kuna rafiki yangu hupenda kuniambia hawa jamaa (Wazungu) kama wangekuwa hawana “ndumba” wasingewaweza wazee wetu na kiwapiga mijeredi na kuwafanya watumwa! Wangewalaza nje na kuwafanyia vibweka vyote vya kichawi.

Katika uzi huu wa kwanza nitakuletea majina ya makabila hayo na asili yake (maeneo yalikokuwa yanapatikana) na wakati mwengine nikihitimisha na hali ya makabila hayo kwasasa.

Moja kwa moja niingie kwenye uchambuzi ;

GAULS
Maarufu kwa jina la Gallic
Jamii hii inahusisha makabila matatu ya Celtae (Galli), Belgae na Aquitani
Usiwachanganye na Gaels

View attachment 1029069

Walikuwa jamii ya koo mbalimbali isiyokuwa na mfumo wa kifalme lakini waliweza kuunganisha nguvu na kukabiliana na adui zao pale ilipowabidi kufanya hivyo na walifanya hivyo kwenye vita za Telamon ya mwaka 225 BC na vita za Gallic miaka ya 50s BC.

View attachment 1029029

Gauls chimbuko lao kulikuwa kwenye Karen ya 5 BC katika maeneo ya La Tène kaskazini mwa Alps na wakisambaa katika eneo lote la Seine,Middle Rhine na upper Elbe ) mpaka inafika karne ya 4 BC walishafika maeneo kwasasa yakijulikana kama Belgium ,Ufaransa,Ureno,Australia,Uswiss,Slovakia,Jamuhuri ya Czech,Uhispania na Ujerumani ya kusini.

View attachment 1029028

Kiuchumi walikuwa wakimiliki njia za biashara kuzunguka eneo la mito Rhône,seine,Rhine na Danube na hii iliwafanya waweze kujitanua mpaka maeneo ya Kaskazini mwa Italia,Transylvania,Ugalatia na Balkan

Kwasasa wanajulikana kama watu wa jamii ya Celtics.

IBERIAN
Jamii hii inajumuisha makabila yapatikanayo katika Penisula ya Iberia hapa tunakutana na watu wa Roman Hispania ambayo ndiyo Ureno ya sasa ,Uhispania na Andorra yapo makabila mengine yanayoshabihiana na jamii hii kiutamaduni na desturi.

View attachment 1029040

IRISH
miongoni mwa makabila ambayo pengine tamaduni zao bado zipo kwa sehemu mpaka sasa ni hii ya ki Irish.

Jamii hii inapatikana ulaya ya visiwani na inasadikika chimbuko lake ni watu wa Gaelic.

Tofauti na watu wa Gaelic hawa walikuwa na ufalme ulijulikana kama túatha, ambao pia uliimarika katika makundi matano ya Old Irish cóiceda, Modern Irish cúige hii ikijumuisha makabila ya Ulaid (upande wa kaskazini ), Connacht (upande wa magharibi ), Laighin (upande wa mashariki), Mumhan (upande wa kusini ) na Mide (katikati ).

Kutokana na kukua kwa kasi mara nyingi kulitokea vita katika maeneo haya na mfalme Norman alifanikiwa kutawala sehemu kubwa ya eneo hili

View attachment 1029047 View attachment 1029048 View attachment 1029049 View attachment 1029050
View attachment 1029055

MAKABILA YA BRITAIN
katika zama za Chuma.Makabila kadhaa yaliandikwa na wanahistoria na wanajiographia kama Ptolemy. Asili kubwa ya watu hawa iliaminika kuwa ni watu wa Celtics.

View attachment 1029064
View attachment 1029066
View attachment 1029067

GERMANIC
Jamii hii inahusisha makabila ya Teutonic,Suebian na Gothic jamii hizi hufaamika kama “European ethnolinguistics” kutoka kaskazini mwa Ulaya na hutambulika kwa kuzungumza Germanic historia yao huanzia millennium ya 2 BCE hadi sasa.

View attachment 1029082

Jamii hii inasadikika walichipukia kipindi cha Nordic Bronze ambayo ilitukia wakati wa vita ya Axe culture kusini mwa Scandinavia na hapo baadhi ya makabila ya kijerumani wakaanza kusambaa kuelekea kusini na kupeleka vita vikali na watu wa Celtics na Roma ya zamani na ni kutoka kwa watu wa Roma jina la Germanic lilipopatikana .

Walikuwa wakiabudu mungu Odin.

Jamii hii ndio inasadikika kuwa walikuwa kiboko kwa warumi kwani waliweza kuwapiga vibaya Arminius katika misitu ya Teutoburg 9 CE.
Walikaa maeneo ya Rhine na Danube kwa sehemu kubwa.

Wakati mwengine tutaona nini kilitokea kwa makabila haya/jamii hizi?
Sent using Jamii Forums mobile app

Mpaka leo wanazo hizo Kabila Ila ukisema "Kabila" wanajiona wako nyuma ila baadhi zimekufa na kubaki au kuchukuwa utamaduni wa makabila makubwa. Siku hizi hayo "makabila" wanaita jamii ila wao wakija Afrika wanalazimisha kuita Kabila..... Mfano Uhispania, wapo Kabila la kikatalan ambalo limegawanyika makundi mengi kidogo ila wapo wakatalani wa kule Girona (Gerona), wa Barcelona, wavalencia hâta wabaleari (Ibiza huko visiwani). Pia wapo wagalicia ambapo wao wapo kaskazini magharibi,waastruia, wabasko , ukienda Italia, Ujerumani n.k
Wanazo lugha zao za kikabila n'a utamaduni wao mwengine Pia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom