Je, unaweza vipi kushinda maumivu ya kusalitiwa?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,241
4,326
Habari za muda huu wana MMU.

Leo nimekuja kwenu na mada hii kutokana na mambo yanayoendelea ya watu kuuana na kufanyiana mambo mengi mabaya ikiwa chanzo kikuu kinachosikika ni kusalitiana.

Si jambo jema mtu kumsaliti mpenzi wake, mke/mme wake lakini kutokana na sababu mbalimbali inapelekea jambo hili kutokea,hivyo hatuwezi kulizua lisitokee.

Sasa tujadili njia za kushinda maumivu ya kusalitiwa ili ikitokea mtu kasalitiwa na kajua kua kasalitiwa au anahisi anasalitiwa afanye nini? Ili asije chukua maamuzi mabaya, maana maumivu hayo si ya kitoto eti...

Naomba michango yenu watu wachukue hatua gani ili kuepusha madhara au ulichukua hatua gani ulipogundua umeibiwa mtu wako? Tiririka.
 
1. usipende kupitiliza.
2.usiwe na mtu moja (dawa ya moto ni moto).
3.kama sio mkeo wa ndoa na humhitaji tena tengeneza mazingira ya kutokuonana naye wala kuona kitu kitakachokufanya umkumbuke angalau kwa wiki moja.
4.KUMBUKA KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI. (Ifanye kuwa siri yako)
 
Mara nyingi mtu anayechukua maamuzi ya kuua mtu ama kujiua mwenyewe ni ile hali ya kuwa stressed/depressed

Moja of the best way to overcome stress ni kuongea na mtu....to let it out,na kuna namna nyingi za kuyatoa yaliyo moyoni,kama hivi JF
Kimsingi tabia ya usiri uliopitiliza sometimes una madhara kama haya

Kuna ule usemi "everybody needs somebody"
Tukubali tukatae,huwezi kusurvive on your own,kuna some cases zinahitaji msaada kutoka kwa mtu
 
Usimfatilie au kumchunga mpenzi wako awe mumeo/mkeo (ila mpende sanaa)

Hata akikusaliti hautojua maana ulikua humfatiliiiii

Kipaumbele chako katika mahusiano iwe ni AFYA

hata ukiweza kila mtapotaka kuburudishana "pimaneni" kama mzima endeleeni

Usaliti upo na hautokaaa uishe.
 
CONTROLA,
Mzee hiv hiz vipimo ziko zinapatikana locally???sijui zinaitwaje bt something like mrdt.
But mbali na hivyo,kuna magonjwa mengi sana ya ngono mbali na Aids like homa ya Ini. Sasa utapima vingapi mzee na utapimaje pimaje kila mara?ni ngumu sana
 
Vinapatikana mpaka kwenye pharmacy mkuuu

Ni kweli kuna magonjwa mengi na hutoweza yapima yote

Siku moja moja unakua mnaenda hospital kumpiga full check up (bima si ipo mkuu)

Hapo naongelea utakapokua na wasi wasi nae uliopitiliza.

Magonjwa ni mengi ila acha tujikinge na hili moja ambalo ukilipata "vidole utanyooshewa vingi"

asajizow
 
nimesalitiwa na ubongo wangu kwenye chumba cha mtihani sikujali sembuse mwanadamu tulokutana meno 32,hapana kwakweli

sijawahi fikiria kujidhuru kisa mapenzi kwa namna yoyote ile,walengwa nashindwa kuelewa huwa wanafikiria nini muda huo pengine ningejua cha kuwashauri.
 
Nakushauri,
Ukiona ni mchepukaji /hajatulia basi
ACHANA NAYE.

Afya hainunuliwi dukani.
 
Unatakiwa usihisi Bali uwe na uhakika.
Na kama mimi nikiwa na uhakika
Ni kuacha nae tu
Hakuna haja ya kugombana.
Tuliza akili na maisha yaendelee
Ni kweli yanaumiza
Ila relax
 
Juzi demu wangu simu yake tangu saa1 usiku ili kuwa haipatikani mpaka saa sita usiku.
Alipopatikana akatoa sababu ambazo sijazielewa.
Sasa hivi namchunguza Kwanzaa.
Nikiwa na uhakika basi nitaachana nae
 
Kitu bora ni kukaa mbali na huyo mtu na usimfuatilie kinachoendelea kwenye maisha yake. Tafuta ushauri n.k.Watu wengi wanaumia pale wanapoendelea kumfuatilia mtu pindi wanapoachana
 
Mimi nacho kifanyaga ili kutuliza maumivu yangu ni kitu kimoja tu kama huyo mwanamke anaye dada au mdogo wake wa kike wa damu hapo mmoja wao lazima ni toke nae ili kulipiza kisasi
 
Back
Top Bottom