Hatua sita za kukabiliana na hali ya kusalitiwa na mahusiano kuvunjika

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,490
14,356
Hatua zifuatazo zinaweza kukusaidia

1.JIFUNZE TABIA ZA WATU

Kama hujui asili ya tabia za watu utaumizwa sana miaka yote.Kwa asili ya tabia za binadamu ni kwamba mtu mwenye sifa ya kusema wengine kwa mabaya muda wote,anakusifia sana na kukashifu wengine,anasema wengine kwa ubaya kupita kiasi huwa ni mtu mbaya sana kuliko mtu yeyote anaweza anaweza kuja kichwani mwako.

Watu ambao husema wengine kwa mabaya hufanya hivyo kwa sababu ya wivu kupita kiasi ambao huonekana kwa viashiria vifuatavyo mtu akiwa anaongea
Kushusha thamani mafanikio ya wengine,kukosoa kupita kiasi tabia za wengine,kuwasema wengine vibaya sana wakiondoka baada ya mazungumzo,

Mtu mwenye wivu utamjua kwa kumwambia taarifa zako nzuri ghafla utaona anakuwa na hasira lakini ndani ya sekunde chache anajilazimisha kutabasamu kwa nguvu hiyo ni alama ya hatari kwako

Sifa nyingine ukimpa taarifa mbaya kuhusu maisha yako anakuwa na furaha ghafla kisha anajilazimisha kukuonea huruma lakini katika kuonyesha huruma unahisi kitu cha tofauti ndani ya maneno yake hayaendani na muonekano wa sura yake hiyo ni alama ya hatari kwako ,

Mwengine anaweza kukupa pongezi kupita kiasi lakini ghafla utaanza kujisikia vibaya sana kwa kumpa taarifa zako labda kwa namna anakupa pongezi inaonyesha anataka kujua namna utakuwa na mafanikio makubwa sana katika lugha yenye kejeli

2.EPUKA KUJUTA KWA JAMBO LOLOTE AMBALO LIMETOKEA
Kujuta au kujilaumu ni kupoteza muda Hivyo endapo mahusiano yatavunjika epuka kujuta kwa jambo lolote badala yake jiulize nini cha kufanya kwa wakati huo.Huwezi kurudi nyuma kubadilisha maamuzi yako lakini unaweza kufanya maamuzi mapya muda huu.

Huwezi kudhibiti tabia za wengine, maamuzi ya wengine, vipaumbele vya wengine epuka kupoteza muda eneo hilo.

3.JIWEKEE MIPAKA

Tambua kwa mtu yeyote anaweza kufanya wema au ubaya kwako muda wowote bila kujali muda mrefu umejenga nae mahusiano au uwekezaji wako katika mahusiano yako hivyo tambua tabia gani huwezi kuvumilia katika mahusiano yako mapya ili uwe mwepesi kukemea tabia hizo endapo zitatokea

4.TAZAMA MAKOSA YAKO NA MAPUNGUFU YAKO TU UJIREKEBISHE
Huwezi kurekebisha makosa ya wengine,huwezi kufanya maamuzi kwa ajili ya mtu mwengine bali unafanya maamuzi kwa niaba yako tu.Ni kweli sio rahisi kuona makosa yako au mapungufu yako lakini ukiwa makini unaweza kuyaona.

Kushindwa kujua makosa yako au mapungufu yako ni hatari sana kwa maisha yako kwa ujumla.Watu wengine watatumia mapungufu yako dhidi yako bila wewe kujua.

5.TAMBUA KWAMBA HUWEZI KUPENDWA NA KILA MTU

Haijalishi utakuwa mchamungu au mshirikina, mwema sana au muovu, mchoyo au mkarimu, muaminifu au msaliti, muongo au mkweli bado huwezi kupendwa na kila mtu.

Ukiwa rafiki wa kila mtu unakuwa adui kwako mwenyewe hivyo .Katika kutambua hayo vilevile fahamu kwamba upo na mapungufu kama watu wengine.

Kwa kawaida binadamu akiwa na màumivu huwa anaamini watu wengine ndio wabaya lakini sio kweli sisi sote ni wabaya kwa baadhi ya watu na vilevile ni wazuri kwa baadhi ya watu.

Hivyo huwezi kutarajia kuwa kipenzi cha kila mtu kwa sababu haiwezekani.

6.ZINGATIA MAISHA HAYATAZAMI MALENGO YAKO

Katika maisha ni rahisi kuona unastahili kufanikiwa sana kuliko wengine lakini maisha hayatazami malengo yako, matatizo hayatazami kama wewe ni mchamungu au mshirikina, matatizo hayatazami kama wewe ni muaminifu au msaliti, matatizo hayatazami kama wewe ni mwema au muovu, matatizo hayatazami kama wewe ni mchoyo au mkarimu, matatizo hayatazami kama wewe ni muongo au mkweli, matatizo hayatazami kama wewe ni mpole sana au mkali sana.

Katika maisha yako utapoteza watu wengi sana kama marafiki, ndugu, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako,watoto wao au wazazi wako labda kwa kutengana, mahusiano kuvunjika au kifo n.k lakini huwezi kudumu na mtu yeyote MILELE.

Unaweza kujenga mahusiano kwa nia njema lakini huwezi kupanga maamuzi ya wengine katika kudumisha mahusiano baina yenu hivyo kuwa muelewa eneo hilo.Epuka kulaumu mwenendo wa wengine, epuka kurekebisha tabia za wengine,epuka kumfanya mtu yeyote ajute au ajione mkosaji baada ya mahusiano kuvunjika.

Hakuna binadamu mzuri kwa 100% au mbaya kwa 100% na wewe ukiwa miongoni mwao

Si jambo sahihi kujiweka katika kundi la watu wazuri kwa 100% au wabaya kwa 100% kila mtu yupo na sifa zote nzuri na mbaya.
 
Ameniharibia mambo mengi mno

Huwezi kupanga nini kitokee katika maisha yako ila unapanga ufanye nini kwa kila tukio lenye kutokea maishani mwako.

Huwezi kudhibiti tabia au maamuzi ya wengine.Baadhi ya watu ni wavivu wa kufanya maamuzi,wengine ni wepesi,wapo wenye huruma wapo wasiokuwa na huruma,wapo wenye kujali mahitaji ya wengine wapo wenye kujali maslahi yao binafsi
Watu wa aina hiyo utakumbana nao .

Ikiwa mafanikio yako hutegemea sana maamuzi ya wengine basi uwezekano wa kufeli eneo hilo ni mkubwa sana kwa sababu kila mtu huwa na vipaumbele tofauti.


Makosa yake mwaachie mwenyewe,tabia zake mwaachie wenyewe, maamuzi yake mwaachie mwenyewe. Msahau na wekeza nguvu kurekebisha tabia zako tu ndio zipo ndani ya uwezo wako.


Bado una nafasi ya kutengeneza mambo mazuri zaidi. Mambo yaliyoharibika wacha yaharibike wewe songa mbele. One day uje kuwa Oprah Winfrey
 
Back
Top Bottom