Shukran sana kiongoz... nimepitia NACTE nimeona instute na colleges tu ndo kuna guidelines... naanza safari ya kutembelea kila web ya chuo kikuu nione imekaaje...
Acha nikunufaishe na kauzoefu kangu kidogo.
Kwa kurahisisha mambo tunaweza kusema kwamba kuna diploma za aina mbili (kwa kigezo cha muda/miaka ya kuisoma).
1. Diploma ya miaka mitatu.
2. Diploma ya miaka miwili.
Vigezo vya kujiunga na diploma utakayoisoma miaka mitatu mara nyingi au mara zote ni ufaulu kwenye masomo kadhaa (kutegemea na aina ya kozi) kwenye cheti cha KIDATO CHA NNE. Mifano ya hapa ni diploma karibia zote za kozi za afya, za uhandisi, usanifu majengo, umeme, n.k
2. Kwa diploma ambazo unazisoma kwa miaka miwili, vigezo huwa ni ufaulu wa angalau principal moja kwenye cheti cha kidato cha sita au ufaulu wa angalau GPA ya 2.0 kwenye cheti cha elimu husika "ngazi ya cheti" (astashahada). Kundi kubwa la diploma zinaangukia kwenye fungu hili. Na za kwako zinaangukia hapa.
Kwa muktadha huo ukiwa na elimu ya kidato cha nne kama ndio elimu yako ya juu zaidi basi omba kozi uitakayo ila utaanzia ngazi ya certificate na ukishamaliza utapata sifa sasa za kusoma diploma.
Nadhani unaweza kuwa umepata picha