puker
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 1,057
- 2,195
Habari za muda huu wana JF! Bila shaka mnaemdelea vyema na mapambano.
Sasa, turudi kwenye mada husika, katika hali ambayo pengine wengine wanaweza kuona sio kawaida kwangu hua naifanya mara kwa mara, pindi ninapoenda tofauti na mikakati/mipango niliyojiwekea aidha ya muda mfupi au mrefu.
Nimekuwa na katabia cha kujipa adhabu pale ninapokwenda nje ya mikakati yangu ... unaweza jiuliza najiadhibu vipi?
Ngoja niwape, mifano michache[emoji4], mfano inaweza kutokea siku nikafanya matumizi makubwa yasiyo ya lazima, ikapelekea kutoka nje ya badget niliyojiwekea, mfano kama nilipanga kutumia 20k sehemu... ikatokea nikatumia zaidi ya hapo kwa uzembe au tamaa ambayo haikuwa na ulazima. Basi siku inayofwata nitahakikisha... najibana aidha kwa kujinyima kitu fulani kwa kufidia upumbavu nilioufanya jana yake...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] waheshimiwa, sio jambo la ajabu kabisa upande wangu hata kuuwa mlo mmoja na hela ninayo...lakini kwa kuwa jana nilitumia fedha nyingi hivyo nita ifeed kwenye pengo la siku hiyo. Hivyo kutembea kwa mguu, kupanda daladala na kuacha gari home, ni jambo la kawaida sana kwangu.
Kingine ninaweza kuchelewa kufungua ofisi, mfano ratiba yangu ni saa 2 kamili asubuh duka linatakiwa kuwa wazi na saa 3 kamili usiku nafunga, ikitokea siku nimechelewa kwa uzembe nikafungua saa 4 asubuhi, jua kesho yake lazima niongeze masaa mawili mbele ya kazi yani duka nitafunga saa 5 usiku kufidia masaa mawili ya jana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hii kitu inatokea kwenye kila kitu... ukisikia watu wanaokwenda na muda mimi ni miongoni mwao, aisee hakuna kitu nachukia kama tupange tukutane muda fulani hlf ukachelewa hata dk 10, kwangu ni big issue sana, na hata ikatokea mm ndio nikachelewa hata Dk 5 utashangaa samahan nitakazo kuomba hutoamini.
Mbaya zaidi kipindi ambacho naishi na mzazi mwenzangu, alikuwa mpaka ananishangaa...huwa nilikuwa natabia ya kumwachia pesa ya matumizi kwa wiki, ikatokea aka miss use matumizi akaniambia fedha nimekwisha kabla ya wiki kuisha, wala sipanic nitakachofanya nikumuuliza matumizi yake yalikuwaje...kama nikigundua ni uzembe wa makusudi, basi atajua pa kuipata hiyo hela ajazie nikirudi nikute chakula...
Kiufupi nina vimikakati vyangu naviheshimu sana. Watu wengi wananitafsiri ni UBAHILI, upande wangu nasema hapana maana kama nikiamua kuspend kiasi fulani cha pesa hata kama nikikubwa, ila kwa kuwa niliweka kwenye ratiba zangu wala roho haiwezi niuma ila ikitokea nimekwenda tofauti hapo ndio balaa huanza...
Sasa ndugu zangu hebu mnishauri, hili ni tatizo la kisaikolojia au ndio namna nimeumbwa, imefika wakati hata familia yangu wanajua kabisa mm ni mtu mwenye misimamo mikali sina kauli mbili...
#Karibuni kwa hoja na ushauri