Je, unaufahamu "upupu"?

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,471
12,373
Huu ndio upupu, ni mmea unaoota porini maeneo ya mikoa ya kusini hasa kipindi cha kiangazi ni mmea unaotambaa na kutoa mbegu kama maharage iliyozungukwa na vitu mithili ya manyoya hii kitu ikikupata mwilini "inawasha" vibaya mno kiasi kwamba hakuna maelezo, unaweza hata kupoteza maisha kama ukikupata kwa wingi, pia mbegu zake ni chakula na pia ni Natural viagra shughuli yake ni zaidi ya kidawa vumbi cha Congo.

Upupu tulikua tunatumia kama silaha kwa walimu unavizia unaenda kumwaga kwenye meza yake na kiti, basi akijichanga na kuketi tu balaa lake hatokuja kusahau anaweza akavua mpk nguo hadharani kwa kuwashwa.

NB: Dawa ya kutuliza muwasho wa upupu ni ndogo sana kujipaka majivu ya moto ama mchanga uliopigwa na jua kali na kupata moto.
1483455441199.png
1483455463984.png
 
Hiyo kitu inawasha kuliko kitu chochote duniani.
kuna vidudu vinaitwa washawasha akikutambaa yule hadi ngozi utahisi inawaka moto, japo upupu nao ukikupatia kwenye jua kali halafu ukuingie kama kwenye nywele hivi utahisi ndo kifo chako
 
Yale maji ya kuwasha wanayoyatumia polisi kuzima fujo, zamani yalikua yanajulikana kama maji ya upupu.
 
kuna vidudu vinaitwa washawasha akikutambaa yule hadi ngozi utahisi inawaka moto, japo upupu nao ukikupatia kwenye jua kali halafu ukuingie kama kwenye nywele hivi utahisi ndo kifo chako
unaujua vzuri upupu? acha mchezo kabisa.
 
Ule upupu unaoliwa ni bonge la biashara kwa maeneo ya kusini. Siku na miezi kama hii bei inafika hadi Tsh. 90,000/= kwa gunia moja la debe sita. Ni aina hii ya upupu inapikwa na kuandaliwa kwa siku mbili hadi kuwa tayari kwa kuliwa. Nakumbuka binafsi nimesoma kwa biashara ya upupu na NIPA. Mama yangu alihangaika sana hadi kufikia hapa nilipo. Asante Mamangu!
 
Nikiwa mdogo nilikuwa mtata sismsikilizi bimkubwa shughuli za nyumbani napangiwa sifanyi,sasa ikija kwenye adhabu nilikuwa nachapwa bakora za kutosha kisha naambiwa chagua adhabu either upupu au kulala njaa...siku zote option ya pili ndo nilikuwa nachagua.upupu usikie hivi hivi hata ukikugusa bahati mbaya shughuli yake sio ndogo!
 
Nakumbuka sana hii kitu. Walio wahi kuogelea mtoni wanaijua vizuri. Ilikuwa inapakwa juu ya mawe. Ole wako uende ukalale juu ya jiwe. Lazima ulie kama mbwa mwizi
 
Back
Top Bottom