kerubi afunikaye
JF-Expert Member
- May 20, 2013
- 1,183
- 1,057
Nililetewa zawadi ya shower gels za Axe toka U.S na shem wenu.Nikatokea kuzipenda sana kutokana na harufu yake nzuri,si mnajua tena,pale kwenye label yake imeandikwa UNLIMITED FEMALE ATTENTION maskini sijui shem wenu hakuisoma vizuri?!nikawa naogea asubuhi na kujipaka kidogo mikononi na kwenda ofisini!kweli bwana,watu wa mwanzo kunotice harufu ile nzuri walikuwa staff wa kike pale ofisini.Nikaanza kufanya research ni maduka gani hapa mjini naweza kuzipata zile gels ili niachane kabisa na haya "marevola" yetu ya kkoo!Ghafla baada ya kama wiki mbili za matumizi ya hii axe shower gel nilianza kuwashwa sana maeneo ya miguuni hasa nikiwa nimetoka kuoga.Sikugundua mapema,nikaendelea!hali ilizidi kuwa mbaya nikawa nawashwa na kujikuna hadi napata michubuko.Niliamua kwenda kwa daktari na kumweleza.Akaniuliza naogea nini nikamtajia.Akaniambia nimpelekee ile shower gel.Nilipompelekea na kuisoma tu ingredients zake akaniambia niache mara moja matumizi ya ile kitu kwani ina chemicals nyingi ambazo huenda mojawapo iko allergic na ngozi yangu.Sikuridhika,kutokana na "mahaba" niliyokuwa nayo kwa harufu ile nzuri ya Axe.Nikawapigia simu jamaa zangu mbalimbali wa huko ughaibuni ambako vitu hivi vinatumika sana na wengineo wa hapa nyumbani,wote wakanitahadharisha kuwa kesi hizi za skin irritation baada ya matumizi ya shower gels ni nyingi sana huko kwao.Nikaamua kufanya karesearch kangu mtandaoni na kuprove kuwa kweli hizi gels zinawaletea watu wengi muwasho wa ngozi.Zilizo mbaya zaidi ni zile zenye fragrances(perfumes) na alcohol pamoja na chemicals nyingi(na kwa kweli hizi ndio hunukia kweli).Hizo chemicals huondoa mafuta ya asili ya ngozi na kuifanya iwe kavu kitu kinachosababisha matatizo baada ya matumizi ya muda mrefu.Likanishuka shuuu!nikazikumbuka zile revola zangu nilizozitupa huku natukana!Nimeacha kutumia zile gels na ngozi imeacha kuniwasha kabisa.Si kwa sababu ngozi yangu ni delicate sana na iko allergic,no,ni kwa sababu haya madude yetu ya siku hizi yamejaa chemicals nyingi sana!Shem wenu amesikitika manake na yeye ilikuwa nikitoka kuoga tu basi anataka tukae kiti kimoja!Nikamwambia ptuuu,kama kununa anune tu,hiyo harufu siitaki tena,watu wanakusifia unanukia huku ngozi inawaka moto,ujinga mtupu!Wenzangu na mie naamini mmenipata!Chukueni tahadhari!Hivi vitu vyetu vya kisasa hivi...hebu nijiondokee mie,shauri zenu mkiendelea,mie nimeacha,niko safi kabisa na "revola" zangu tena nataka nitafute arovela kabisaa!