Je, unauelewa msimbomilia au barcode?

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
“MSIMBOMILIA-BARCODE” Je, unauelewa juu ya msimbomilia au Barcode? Kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanajua umuhimu wake katika soko la ushindani toka kiwandani mpaka kwa mlaji na bidhaa ina nafasi gani? Nani anatoa na kidhibiti Msimbomilia?

Dj5PzABXgAAKRw-.jpg
 
Leo naona umeamkia JF,nishasoma nyuzi zako hapa si chini ya 5 within 30 minutes,lazima na wewe uwe maarufu hapa...keep it up!
 
Kiswahili bwana

Kwa hiyo kwa ajili ya mistari myeusi, tulianza na punda - ikaongezewa milia, tukapata pundamilia
Tukaanza na simbo (symbol), na kwa ajili mistari myeusi, tukapata simbomilia!

Naona karibu tutapanda neno la kiswahili kwa ajili ya "zebra crossing' barabarani - napendekeza vukamilia!

Very creative.
 
Ewaaa nilikuwa nahitaji kujua hii wapi naweza pata barcode na ni vigezo na hatua gani za kupata?
 
Hizi zipo aina nyingi tu, zilianza kutumika kwa kuwa namba zikiandikwa ni rahisi kuharibika na computer kushindwa kuzisoma yani mara nyingi utaona mistari mistari halafu chini kuna namba zimeandika sasa ile mistari computer inaisoma kama ile namba iliyoko chini kwa maana nyingine ile mistari inawakilisha namba iliyoandikwa chini yake..
EAN ndiyo naona wanatumika sna hapa nchini watatoa na kukupa barcode ya bidhaa zako ambapo barcode zao zina tarakimu 12 za namba.
ile scanner uwa inasoma ile mistari ambapo kila mistari mitatu huwakilisha namba flani
 
Back
Top Bottom