Je, unataka kupoteza umaarufu wako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unataka kupoteza umaarufu wako?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by yusufummaka, Jul 7, 2012.

 1. y

  yusufummaka Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliye na hamu ya kupoteza umaarufu wake ndani ya jamii aendelee kuunga mkono migomo ya madaktari. Wagonjwa wanaokwenda kwenye hospitali zetu za rufaa huwa wanatoka mikoa na willaya zote nchini, hivyo usumbufu wanaoupata wagonjwa, wanafamilia na jamaa za wagonjwa zinaikumba mikoa na wilaya zote nchini equally. Atakaeibuka hero of the day ni yule atakaefanikiwa kuwashawishi madaktari warudi kazini waokoe wanaofia mivunguni bila matibabu huku akitumia njia mbadala za kutafuta maslahi bora ya madaktari bila kulazimika kugoma. Tunapomsikitikia dk wetu ulimboka tusisahau pia kusikitikia hatima za wagonjwa waliokosa matibabu (trike a balance). Daktari asitarajie kugongeana bilauri za mvinyo huko mitaani na wagonjwa, wana-familia ama jamaa wa mgonjwa aliyepata masahibu ya kukosa matibabu. be care vita haina macho!!!!.
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,170
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Hivi selikali inpo wasimamisha kazi ma dr huku ikiwa haina hata mbadala wanategemea nin? Acha tufe kama watakavyo huku wakiendelea kuficha kodi zetu uswis. Napendekeza re-allocation ya balance ya rushwa ya rada kwenda afya!
   
 3. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Serikali ndio itakayo pata hasara kuwaacha wagonjwa wafe bila msaada hapa wa kulaumiwa ni SERIKALI kwa kuzembea kuwalipa madaktari na kuzorotesha huduma Mahospitalini.
   
 4. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Kama vita tu,maendeleo yoyote lazima yagharimu maisha ya watu kidogo.kwangu mimi,naona mgomo ndiyo njia pekee.Mgomo huu ukiendelea utaifanya serikali ianze kutumia akili kidogo.

  Mfano mdogo tu,ule mgomo wa kwanza ulikuwa January mwaka huu.Madaktari wakaeleza kuhusu upungufu wa vifaa na yafananayo.Kama serikali ingekuwa inapenda demokrasia si ingeyaadress haya masuala kwenye bajeti hii mpya iliyopita June??

  Ni wazi.Mgomo ndiyo njia pekee..ila hakuna vita isiyo na majeruhi.Hata vita sio jambo jema,lakini wakati mwingine ni lazima.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kupoteza umaarufu na heshima yako kuwa mwanachama wa CCM. Huku kwetu ukivaa shati la kijani unazomewa kila unapopita, hata watoto wanahusisha mavazi ya kijani na ufisadi,ukware na uuaji.
   
Loading...