ekari 15 mahindi unaweza kulima kwa sh ngapi?
Wazo zuri sana mkuu.swali mfano kuitokea majanga labda mazao kusombwa na mafuriko hafu tusipate faida yoyote hapo ina kuaje?
Wakuu mi nimefanya na wengi mpango huu, na wengi wapo maofisini na wanafaidika sana maana wapo bize na kazi zao huku kilimo kinatembea.. kama hutaki kupigiwa pigiwa simu na kuulizwa sijui madawa, mara nini.. we nipe tu laki 4 kwa kila ekari nami nitakupa laki 5 kwa kila ekari baada ya kuvuna, hapo ikitokea sijui mafuriko au mvua ndogo hela yako ipo palepale,. na nitawajibika, KARIBU
Hapa sijakuelewa mimi nikupe laki nne wewe uzalishe unipe laki tano? Ina maana baada ya miezi kama sita faida laki moja kwa eka? Au fafanua mengine ya gharama za kulimia uko poa
ndugu Raelish ekari tano za matikiti itakuwaje,ziko eneo la dakawa morogoro,na yakikomaa soko unaweza kutafuta wewe?
Mkuu nipe hela ya ekari tano kama nilivyosema hapo juu, maana yake ni tsh.2,000,000/= msimu ukifika we kaa mkao wa kula tu.. soko kila kitu nafanya mimi., we unasubiria chako tu
Ekari 50 ufuta gharama zitakaa vp? na mwisho itakuaje matokeo kama kusipotokea balaa lolote.
Ukipotea tutakutafutia wapi?
Hilo ndio la msingi zaidi. Una ofisi?
Huo mchanganuo kaka si uandae ili ukalime mwenyewe? Jukwaa letu linasisitiza siku zote watu kufanya wenyewe kwa usimamizi wa karibu la sivyo mtaumia.
ekari 15, kuandaa shamba namaanisha kukata miti na kusafisha shamba ekari ni 1 tsh.100,000/=, kupiga matuta kwa ekari moja matuta yatakuwa 70+ ni tsh.70,000/=,(kama hutaki matuta hiyo itakuwa haipo, japo matuta ni mazuri zaidi), kupanda kwa mstari ekari 1 ni tsh.60,000/=, kupalilia ekari moja ni tsh.60,000/= mpaka hapo heka moja ina wastani wa laki 3, bado madawa, kuvuna.. na ekari moja mahindi umekosa sana yaani sana gunia 10 hapo umekosa sana sana sana, gunia kumi ukiuza hukosi milioni tayari faida mara 2... kwa hiyo kama ekari moja imetumia kama laki tatu hivi (toa madawa na uvunaji), ekari 15 inatakiwa tsh.4,500,000 kulima na kupanda tu,. tena naenda kukupigia mkoani hii unapata faida ya kutisha mkuu.. LAKINI USISAHAU KUNA GHARAMA ZA KUKODI SHAMBA KAMA WE HUNA