Je unataka kulima na upate faida?

Raelish

JF-Expert Member
Jul 17, 2013
489
162
Habarini waheshimiwa.!!

kutokana na watu kuwa bize sana na kazi zao na kushindwa kufanya kilimo japo wanapenda. mimi nimeamua kuwasaidia watu wa namna hiyo, yaani hivi tunakubaliana unataka ulime zao gani na kwa ukubwa gani wa shamba na unafikiri ukubwa huo wa shamba kiuhalisia unaweza kutoa mazao kiasi gani, tunafanya tathmini kisha unanipa mtaji wako wa kilimo mi naingia shamba, nakupigia kazi hadi muda wa mavuno nakukabidhi mazao yako kama tulivyokubaliana alafu we unanilipa (kadri tutakavyokubaliana).

Mashamba naweza kulima hadi mikoani na nakufanyia shughuli zote za shamba nakukabidhi mazao na malipo ni kama nilivyosema.

Makubaliano haya yote tunayafanya mbele ya chombo kinachotambulika kisheria ili wewe usitapeliwe hali kadhalika nami pia. kwa mawasiliano zaidi ni-pm nikupe namba yangu. "karibu ujenge uchumi wako".
 
ekari 15 mahindi unaweza kulima kwa sh ngapi?

ekari 15, kuandaa shamba namaanisha kukata miti na kusafisha shamba ekari ni 1 tsh.100,000/=, kupiga matuta kwa ekari moja matuta yatakuwa 70+ ni tsh.70,000/=,(kama hutaki matuta hiyo itakuwa haipo, japo matuta ni mazuri zaidi), kupanda kwa mstari ekari 1 ni tsh.60,000/=, kupalilia ekari moja ni tsh.60,000/= mpaka hapo heka moja ina wastani wa laki 3, bado madawa, kuvuna.. na ekari moja mahindi umekosa sana yaani sana gunia 10 hapo umekosa sana sana sana, gunia kumi ukiuza hukosi milioni tayari faida mara 2... kwa hiyo kama ekari moja imetumia kama laki tatu hivi (toa madawa na uvunaji), ekari 15 inatakiwa tsh.4,500,000 kulima na kupanda tu,. tena naenda kukupigia mkoani hii unapata faida ya kutisha mkuu.. LAKINI USISAHAU KUNA GHARAMA ZA KUKODI SHAMBA KAMA WE HUNA
 
Nina hekari 20 huku rundugai yaani ukiwa pale kwasadala au boma pale HAI kwa chini kulee kuna milima ambapo ndio reli ya kwenda arusha imepita.
njoo tufanye kazi
 
Nina hekari 20 huku rundugai yaani ukiwa pale kwasadala au boma pale HAI kwa chini kulee kuna milima ambapo ndio reli ya kwenda arusha imepita.
njoo tufanye kazi

haina shida nipm nipe mawasiliano yako tuongee zaidi
 
Wazo zuri sana mkuu.swali mfano kuitokea majanga labda mazao kusombwa na mafuriko hafu tusipate faida yoyote hapo ina kuaje?

wazo zuri kama unaogopa hilo, unanipa mimi laki 4 kwa ekari moja alafu mi nakupa laki 5 kwa kila ekari baada ya kuvuna, ikitokea mafuriko au chochote hela yako ipo palepale, mimi nawajibika..
 
Wakuu mi nimefanya na wengi mpango huu, na wengi wapo maofisini na wanafaidika sana maana wapo bize na kazi zao huku kilimo kinatembea.. kama hutaki kupigiwa pigiwa simu na kuulizwa sijui madawa, mara nini.. we nipe tu laki 4 kwa kila ekari nami nitakupa laki 5 kwa kila ekari baada ya kuvuna, hapo ikitokea sijui mafuriko au mvua ndogo hela yako ipo palepale,. na nitawajibika, KARIBU
 
Hapa sijakuelewa mimi nikupe laki nne wewe uzalishe unipe laki tano? Ina maana baada ya miezi kama sita faida laki moja kwa eka? Au fafanua mengine ya gharama za kulimia uko poa

Mkuu hiyo laki 1 kama utalima ekari moja tu, mi najitoa mhanga hapo ikitokea mafuriko,magonjwa n.k nawajibika kama kawaida na wew laki 5 yako ipo palepale, kwa hiyo faida kubwa utapata kadri unavyoongeza ekari,. ukinipa hela yalo ya ekari 10 au 20 kadri ya uwezo wako unakuwa umemaliza sehemu yako, mi nafanya kila kitu nakukabidhi chako tu mkuu,
 
ndugu Raelish ekari tano za matikiti itakuwaje,ziko eneo la dakawa morogoro,na yakikomaa soko unaweza kutafuta wewe?

Mkuu nipe hela ya ekari tano kama nilivyosema hapo juu, maana yake ni tsh.2,000,000/= msimu ukifika we kaa mkao wa kula tu.. soko kila kitu nafanya mimi., we unasubiria chako tu
 
Huo mchanganuo kaka si uandae ili ukalime mwenyewe? Jukwaa letu linasisitiza siku zote watu kufanya wenyewe kwa usimamizi wa karibu la sivyo mtaumia.

watu wako bize mkuu wanatamani kusimamia lakini hawawezi, ndo maana tunajitokeza kuwasaidia watu wa namna hiyo
 
ekari 15, kuandaa shamba namaanisha kukata miti na kusafisha shamba ekari ni 1 tsh.100,000/=, kupiga matuta kwa ekari moja matuta yatakuwa 70+ ni tsh.70,000/=,(kama hutaki matuta hiyo itakuwa haipo, japo matuta ni mazuri zaidi), kupanda kwa mstari ekari 1 ni tsh.60,000/=, kupalilia ekari moja ni tsh.60,000/= mpaka hapo heka moja ina wastani wa laki 3, bado madawa, kuvuna.. na ekari moja mahindi umekosa sana yaani sana gunia 10 hapo umekosa sana sana sana, gunia kumi ukiuza hukosi milioni tayari faida mara 2... kwa hiyo kama ekari moja imetumia kama laki tatu hivi (toa madawa na uvunaji), ekari 15 inatakiwa tsh.4,500,000 kulima na kupanda tu,. tena naenda kukupigia mkoani hii unapata faida ya kutisha mkuu.. LAKINI USISAHAU KUNA GHARAMA ZA KUKODI SHAMBA KAMA WE HUNA

Magunia 10 ya mahindi utapata millioni je gunia moja ni Tzs 100,000/= bei ya wapi, kwa Tanzania gunia haizidi 60,000/= hadi 72,000/=
 
Magunia 10 ya mahindi utapata millioni je gunia moja ni Tzs 100,000/= bei ya wapi, kwa Tanzania gunia haizidi 60,000/= hadi 72,000/=

nazungumzia gunia la debe 10 mkuu, yaani kilo 200
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom