Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Je, unakumbuka nini kutoka kwa baba yako?

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,198
Binafsi nakumbuka siku moja hivi tuko kijijini na mzee tumepanga kesho yake tukamtembelee babu, baba yake mdogo baba ambaye alikuwa anaishi kilometa kadhaa kutoka tulipo (KM 7).

Wakati huo nilikuwa na Miaka 6, mkubwa kabisa, Sasa wakati wa safari tumetoka vizuri mimi na mzee mtu Bee (wawili) tu pale nyumbani kuelekea kwa babu.

Wakati tuko njiani nilikuwa namdekea sana baba yangu, Sasa baada ya kama Nusu safari hivi nikamrukia mzee na kumwambia nimechoka anibebe.

Mzee alinitazama usoni na kutabasamu kisha akasema unataka nikubebe mpaka wapi,mi nikamjibu mpaka kwa babu.

Mzee kweli akanichukua na kuniweka begani mpaka tumefika kwa babu, huku tukipiga story. Huwezi amini mzee alinibeba tena begani mwake wakati wa kurudi mpaka nyumbani.

Wala sikuwaza kwamba nilikuwa namuumiza mzee wangu na wala sikuwaza kwamba ipo siku nitakumbuka na kumisi moment ile.

Nakupenda sana Baba yangu, Nakuombea kwa Mungu akujalie Afya na Nguvu ili uweze kuishi miaka mingi hapa Duniani.

CC Zero IQ
 
Zile stick zile alizokua anakatia. Bila zile mm nisingekua hapa nilipo. Yaani ningepotea vibayaa.

Angenilea ki dady dady kama hawa watoto wetu leo? Aisee angekua anasitika sana sawa na ule msemo wa majuto ni mjukuu.
 
Nakumbuka mimi nikiwa form one na mdogo wangu grade 2 tumeshuka kwenye school bus tunatembea kuelekea nyumbani. Ghafla njiani akatokea mkaka jirani yetu akaanza niambia kwanini unanikataa huku ananipiga akinituhumu najisikia sababu sisi tunapelekwa shule na gari.

Mdogo wangu akakimbia hadi nyumbani kumwambia baba na mimi nilifanikiwa kumchomoka yule kijana nikakimbilia nyumbani kufika nalia baba akinichukua hadi nyumbani kwao yule kijana, ile tunaingia tu na yule kijana kafika kwao aiseeeeee alipigwa makofi na mshua nikajua yameisha tunaenda nyumbani.

Mara baba akasema tunaenda polisi kufika polisi nikaandika maelekezo na hivi nilikuwa under age ikachukuliwa defender pale kuja kumkamata yule kijana yeye alikuwa mkubwa tukaenda polisi alichapwa fimbo na polisi jamani baadae wakanipa fimbo na mimi nijirudishie hehehehe. Tangu siku ile hakuna kijana mtaani kwetu alitusogelea kuongea ujinga.

Nakupenda sana baba, Mungu akupe maisha marefu.
 
Namkumbuka kwa mengi hasa jinsi alivyokuwa ananihamasisha kusoma, japo alikuwa mkali, viboko kwa sana ila nashkuru kwa hayo sasa naona matunda yake.

Pia ni mtu poa sana na yuko social, hii imetusaidia kumzoea na kuongea nae mengi. Mungu ambariki sana na amlinde.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitabu kinaitwa "SOMA KWA HATUA".
kitabu sikipendi Kileee kimeniliza sanaa
Dingi akitoka kazini anaanza kunifundisha.
Nikikosea tu bakora za maana..
Kipindi hicho baba kanunua TV na deki..
Nikirudi mchana mimi tv tu nacheki mikanda.
Phantom solder,eastern condors,Rambo anold baba jeni..
Ila usiku ukianza kuingia nakuwa mpole maana najua baba akirudi ataniita anifundishe na bakora juu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe kwann wanao unawadekeza kama mayai ?
Mm wa kwangu siwadekezi ila tu nimepunguza kiboko hapo kwakua malezi na changamoto za malez kwa enzi zile ni tofaut na sasa.

Zamani unakuta nyumba familia ni extended .watoto wa uncle na shangaz na wengine kibao.Baba mmoja na mama mmoja ila watoto kama 20 hiv ndani ya nyumba.
So unahitaji ukatil kidogo na ukali ili kuwa mudu.follow up ya mtu mmoja mmoja ilikua ngumu.

Pia kwa kwa malez yetu yale wazee wote walikua wanaweza kukuadhibu ukikosea sio mzaz wako tu.Hivyo hii ilitufanya mazingira hatarishi kwetu yasiwe makubwa sana kuharibika kimaadili.
N.k N.k

Ila kwa sas unakuta nalea wanangu tu.watoto wa 3.Nawafuatilia kwa ukaribu.maongez kwa sana toka wakiwa wadogo kiasi kwamba unajikuta hakuna haja ya fimbo maana unawa mudu.

Pia sasa hiv mtoto wa mwenzio sio wako.So unajikuta kama sio ww kuwajibika moja kwa moja kwa watoto wako then no body else can do that for you.malez ya sasa yamekua gharama hivyo unajikuta unalazimisha kutengeza friendly enviroment kwa watoto ili wakasaidie kwa wao kuwa transparent..wasiwe waoga.hapa automatically fimbo inakaa kando.

So haiwi kuwalea kimayai lakin unajikuta unawalea kwa akili sana kuliko kutumia nguvu
 
Me nakumbuka alinilipia ada ya mitihani ya kumaliza sec huku akiwa anaumwa hoi na akihitaji wa pesa pia ili aendelee na matibabu
Masikini Baba yangu saa chache baada ya kumaliza mitihani furaha yangu ikakatizwa 😭😭😭 baada ya kurudi home na kukuta msiba😭😭😭
 
The hustles! Vile mzee alipambana kuhakikisha anaweka msosi mezani, ada zinalipwa, tunalala pazuri na mengineyo. Wakati tumeshiba tunaimba 'nani kama mama', mzee yuko maporini huko usiku wa manane analinda mipaka ya nchi ili tukipate hicho chakula. Fathers are the most underrated humans!
 
Mungu amlaze pema huko aliko ...sikubahatika sana kukaa na mshua nafikisha miaka 4 mshua akavuta du , but always nina mmisi sana najua angekuwepo , na ndoto alizo kuwa nazo juu ya watoto wake ...lkn haikuwa

Always iwill miss u

sent from HUAWEI
 
Daima nitamkumbuka mzee wangu kwa kujitolea kila alichonacho kuhakikisha watoto wake hawakosi. Kanipa elimu bora kadri ya alivyoweza japo yeye mwenyewe hakulijua hata darasa moja. Inasikitisha tu kuwa hakuishi kuja kuona japo kidogo ya matunda ya jitihada zake kwangu. Wengi wetu tulichukulia poa kila tulichopewa na wazazi , kutokutambua ni jinsi gani walijihini ili sisi tupate.
Rest in peace pa, Allah akuweke katika daraja lillo bora zaidi huko ulipo. Amiin.
 
Back
Top Bottom