Je! Unajuaulivyo wa thamani? ... ebu soma hapa.

Je! Unajuaulivyo wa thamani? ... ebu soma hapa.

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Amani iwe nanyi enyi nyote wana JF,
Ukiwa na Kitu cha thamani husababisha mambo kadhaa mfano:

  • · Gharama kubwa na Umakini sana wa kukitunza(Mfano Ikulu, Nyumba kubwa za Dar zina geti zinazo gharimu kiwango cha kujenga nyumba nyingine ndogo, Rais wa Nchi, Bank Kuu ya Nchi, Kambi za Kijeshi)
  • · Tabia ya Mwenye cha thamani hubadilika( Mfano: Kupata fedha kubwa kwa mara ya kwanza na uko ndani ya daladala kumfanya mtu hataki/anashituka-shituka kila mara Mtu akimgusa, pia imeandikwa ‘pale hazina ilipo na moyo upo hapo..Matt.6:21- Maana pale ilipo hazina yako, ndipo pia utakapokuwa moyo wako yaani ingawa hazina hii inazungumzia maisha yajayo lakini pia inatoa picha namna hazina-kitu cha thamani kinavyoweza husiana na moyo-ambako ndani utoka tabia kadhaa zinazoweza mbadilisha Mtu kwakua na kile kitu cha thamani)
Mipango mizito na mikubwa huwekwa kwa ajili ya kukiendeleza/Kikuza hicho kitu cha thamani-(Mfano mgodi wa dhahabu, Wanyamapori, Misitu, Mtoto mwenye bidii Shuleni na nidhamu kwa Wazazi)

  • · Uvumilivu wa kuchukuliana na mharibifu au asiyejali hicho cha thamani ulicho nacho, hua ni mdogo sana, ni rahisi kumchukulia hatua za kinidhamu au kisheria tena haraka bila kuchelewa (Mfano: Kiwanja/Duka/Hotel yako kutumiwa/chezewa na mwingine bila ruska yako, Shamba lako la mazao kuchungiwa mbuzi)
Kama ‘’Thamani’’ ni Kitu kinachoweza pelekea mambo mazito hayo, basi ni Kitu cha ajabu sana na kukosa kukifahamu, ni hasara ktk maisha haya na yajayo kama marekebisho hayatafanyika kuuondoa ujinga kwa mtu haraka sana ili atambue thamani yake/Kitu alichonacho.Ni huzuni kubwa, masikitiko na hasara isiyosemekana kwa uchungu, Mtu kutojitambua thamani yake au ya kitu alichonacho. Katika mambo ya Kiroho na Imani, tunatambua thamani ya jinsi tulivyo na yale tuliyonayo kwa kusoma na kutafakari Neno ili kujua KWELI zilizomo kutuhusu sisi..Yohana.8:31-32.. 31Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.( Zingatia hao aliwaambia hilo Neno ni Watu waliokua wamemwamini Tayari-Wameokoka lakini bado anawaambia…Wakikaa NDANI ya –NENO lake ndipo Watajua KWELI halafu WATAWEKWA HURU-Kumbe kuna uhuru zaidi baada ya Kuokoka yaani kua huru toka shetani-kisha kuna uhuru tena kadri tunavyoifahamu KWELI.
Mifano na hasara ya Kutotambua thamani ya kitu:-

  • · Watoto wadogo wa chekechea, shule ya msingi, miaka ya karibuni wanapomaliza shule, nao huvishwa kofia na majoho kama yale ya Wanaomaliza Chuo Kikuu matokea yake leo hata kuyavaa ukimaliza Degrees hayana upako wake kama zamani
  • · Kabila fulani Afrika lenye ardhi yenye dhahabu nyingi karne za nyuma, walikua wanachezea dhahabu bila kujua, Wazungu walipokuja wakawapa gorori, wao wakatoa dhahabu
  • · Msichana/Mke kujiachia bila kujijali ktk usafi na urembo, anakosa wachumba au upendo wa mume, anamlaumu shetani na Mungu
  • · Mrithi wa mali-kitu cha thamani- akiwa mtoto hawezi kujali thamani sasa ili hasi haribu, huwekwa chini ya uangalizi-Wagal.4:1-2.. (Basi, nasema hivi: mrithi, akiwa bado mtoto, hawi tofauti na mtumwa ingawaje mali yote ni yake. 2 Wakati huo wote yuko chini ya walezi na wadhamini mpaka wakati ule uliowekwa na baba yake)
Ahsante kwa kusoma, ubarikiwe maisha yako yote!
 
Tuwakumbushe waturudishie kama zamani mkuu;

^^
Nadhani itakuwa vema Tutor B sijui wame experience kitu gani admin, mpaka ikawalazimu kuitoa? I hope it must be a genuine reason.
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
Nadhani itakuwa vema Tutor B sijui wame experience kitu gani admin, mpaka ikawalazimu kuitoa? I hope it must be a genuine reason.
^^

Tuwasubirie kwanza labda watakuja na majibu sahihi kuhusu hili.
 
Back
Top Bottom