Napata shida kufanya tathmini kwamba Hillary Clinton alishinda majority votes kwa tofauti ya kura zaidi ya laki moja, lakini swala la electoral votes yenye idadi ya 270 votes bado sijaelewa vizuri na nina hakika Watanzania wengi hawafahamu zaidi ya kushabikia tu.
Sisi tusioelewa lakini mashabiki wa siasa tunahitaji msaada hapa na tuone application ya hii electoral votes kama ingetokea Tanzania, naambiwa Magufuli angekuwa kama Hillary.
JIBU
Maana Halisi ya Electoral Votes
Sisi tusioelewa lakini mashabiki wa siasa tunahitaji msaada hapa na tuone application ya hii electoral votes kama ingetokea Tanzania, naambiwa Magufuli angekuwa kama Hillary.
JIBU
Maana Halisi ya Electoral Votes
Ni hivi Mkuu;
Uchaguzi wa marekani una kitu wanaita Electoral Collage, hii ni ile 'mechanism' ya kumtambua/kumchagua mgombea urais ambaye anakuwa ameshinda kwa kuzingatia jimbo kwa jimbo!
Sasa iko vipi? Wamarekani wanapokuwa wanapiga kura ni kwamba wanakuwa wanapiga kura kuchagua watu wanawaita 'electors'! Hawa electors ndio wanaopiga kwa niaba ya jimbo lao. Sasa vyama vyote viwili wanakuwa na electors ambao wanachagulia siku ya convention ya kumpitisha mgombea wa chama au wakati wa Primaries.
Kwa hiyo wamarekani wanapopiga kura kwenye jimbo tuseme kwa mfano California na ikaonekana Trump ameshinda California kwa hiyo ina maana kuwa electors wa Republican ndio pekee watakaopiga kura kwa niaba ya California na hii inamaanisha kuwa kura zote (electoral collage) za urais kwa jimbo la California zitaenda kwa Trump.
Na kwa nyongeza tu kwamba majimbo yote ya Marekani ukiacha jimbo la Nebraska na Maine wanatumia mfumo wa aliyepata kura nyingi za wananchi anapewa electors/electoral Collage wote (Winner takes all).
Ingawa kuna jambo moja la msingi la kulifahamu ni kwamba hawa electors hawabanwi na Katiba kumchagua mtu wa chama chake. Anaweza kumchagua mgombea yeyote but kinachowabana ni kwamba kipindi anachaguliwa kama elector anatakiwa aweke 'pledge' kuwa atamchagua mgombea wa chama chake.