UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA KUTOKA BANDARI YA TANGA-TANZANIA HADI ZIWA ALBERT UGANDA.
Ni kweli umbali wa kutoka bandari za Kenya hadi Uganda ni karibu zaidi kuliko bandari za Tanzania.
Lakini nini kinawasukuma waganda kuamua ujenzi wa bomba hili ufanyike bandari ya Tanga-Tanzania hadi ziwa Albert Uganda?
Wataalamu toka Tanzania & Uganda wametoa Sababu zifuatazo:-
1. Gharama kubwa za ujenzi wa bomba kutoka Kenya hadi Uganda. Hii inatokana na mradi kupita sehemu zenye makazi ya watu wengi. Pili, mradi unapita maeneo mengi yenye miinuko hivyo kuongeza gharama za kupampu.
2. Ukitokea Tanga mradi haupiti sehemu zenye makazi ya watu wengi na unapita maeneo ya tambarare hivyo kupunguza gharama za kupampu.
3. Bandari ya Tanga ina kingo za asili hivyo kuweza kusafirisha mafuta mwaka mzima tofauti na bandari za Kenya.
4. Usalama wa uhakika nchini Tanzania tofauti na Kenya ambapo Al Shabab wamekuwa tishio.
Kukamilika kwa mradi huu wataalamu wanasema utatoa ajira za moja kwa moja zipatazo 1,500 na zisizo za moja kwa moja takribani 15,000.
Tuweke siasa kando tuache wataalamu wazungumze.