Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Si muumini sana wa hii imani ila kuna kipindi fulani ilinibidi kuamini kuwa uchawi upo baada ya kila siku asubuhi kukuta damu mbichi chumbani kwangu.....yaani leo nitaikuta kwenye shuka nililotandika, kesho shuka nililojifunika, keshokutwa nitaikuta ukutani, siku nyingine sakafuni..... It was one of worse experience I ever had in my life!
Duuuh,, pole
 
Si muumini sana wa hii imani ila kuna kipindi fulani ilinibidi kuamini kuwa uchawi upo baada ya kila siku asubuhi kukuta damu mbichi chumbani kwangu.....yaani leo nitaikuta kwenye shuka nililotandika, kesho shuka nililojifunika, keshokutwa nitaikuta ukutani, siku nyingine sakafuni..... It was one of worse experience I ever had in my life!
Poleee
 
Ahahaaha, ndugu yangu vile mnavyoviita vimondo mara nyingi siyo vimondo.....ni Wanga wanaruka....
 
Habari za muda huu tulivu wapendwa wangu wa Jf,

Niende moja kwa moja kwenye mada husika, ilikuwa siku moja nilikuwa natoka kuwatafuta rafiki zangu mitaani maana wao waliwahi kurudi nyumbani mimi waliniacha shule nikiwa nawasaidia walimu kusahihisha mitihani ya kidato cha pili,sasa niliporudi nyumbani sikuwakuta kwani tulipanga ktk nyumba moja.

Baada ya kuona hawapo nikaamua kipita mitaani kuwatafuta kwa bahati mbaya niliwatafuta kwa muda mrefu sana bila mafanikio, ilipofika saa tatu ya usiku nikaamua kuanza kurudi nyumbani tu maana wao sikuwaona

Sasa nikiwa njiani kuelekea nyumbani nilipofika karibu na kanisa nikashangaa nimemulikwa na mwanga mkali sana toka juu ya mti nilioupitia jirani yaani huo mwanga sijawahi kuuona tangu nizaliwe mpaka leo hii na huo mwanga baada ya kunimulika ulipotea juu kwa juu na kutoweka ghafla.

Kwa kuwa nilikuwa peke yangu ikabidi nianze kukimbia kwenda nyumbani aisee niliona nyumbani ni mbali kama naenda urusi hivi sijui wenzangu kama mmeshawahi kukutana na matukio ya ajabu ajabu kama yalivyonikuta mimi.
Nimewahi kuona moto chini ya mti, asubuhi ilibidi nirudi kuona majivu, wala sikuona.
 
mimi huwa nataka kukutana na mtu aliyelogwa au kuwekwa msukule au kufanyiwa jambo lolote la kilozi, au anayeweza kuloga aniloge mimi... coz kila anayeelezea mambo haya huwa anarefer rafiki/ndugu ama mtu anayemfahamu........

BTW kwa hiyo story yako inaonesha ww ulitafsiri kama uchawi kumbe mtu alitaka kukutisha kwa kukumulika na zile tochi za betri 12:D:D:D:D:D.... sasa kwa taharuki na woga adrenaline ikashusha ujumbe mzito ambao ukafanya ubongo wako ukkolapse na kushindwa kukadiria umbali... ndo maana ukaona nyumbani mbali:D:D:D:D:D
 
Wanawake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ni wahanga wa tuhuma za uchawi ambapo wengi wanatumikia kifungo jela, kwasababu uchawi ni uhalifu kwa sheria za nchi. Je wewe unaamini uchawi upo?. Papo kwa Papo 02.08.2018.
 
binafsi siamini huu upuuzi..

nashukuru Mungu elimu imenikomboa..

kuna wzkat najiuliza kwanini zinaitwa "Iman potofu"?

niliacha kuwaza haya mambo tangu nikiwa kidato cha nne baada ya kusoma kile kitabu cha THIGS FALL APART.
 
binafsi siamini huu upuuzi..

nashukuru Mungu elimu imenikomboa..

kuna wzkat najiuliza kwanini zinaitwa "Iman potofu"?

niliacha kuwaza haya mambo tangu nikiwa kidato cha nne baada ya kusoma kile kitabu cha THIGS FALL APART.
Hayajakukuta ndio maana unaongea hivyo.ila omba Mungu usikutane na haya mambo
Ila kama unaamini Mungu yupo basi amini uchawi upo,ila kama huamini uwepo wa Mungu basi uchawi haupo
 
Uchawi ni imani muflis kuwa watu fulani wana nguvu fulani yenye uwezo wa kudhuru wengine. Hili jambo ni imani tu na imani hizo zimejikita katika jamii kweli kweli. Hao waliokuwa wakiitwa au wanaoitwa wachawi katika jamii huwa ni watu dhaifu sana, maskini na waoga wanaodharauliwa sana na jamii. Mara nyingi watu hao wakiitwa wachawi, hawakatai wala kukubali, kwani wengine hufikiria kuwa watu wakimuona ana nguvu hiyo ya ajabu (yaani uchawi) itakuwa ni sababu ya kuheshimiwa na kuogopwa.

Wengi wao hujiingiza katika matendo ya kufanya viinimacho au mazingaombwe ya kuwasadikisha watu kuwa wao kweli wanazo hizo nguvu na wana uwezo wa kudhuru. Kutokana na hilo, wakazaliwa watu wanaoitwa wachawi au walozi. Hawa watu wameanzisha utamaduni wao, kama zilivyo dini. Tofauti yao ni kuwa wao mambo yao hufanyika kwa siri, kwani lengo ni kuwadanganya watu waamini kuwa kweli wanazo nguvu za ajabu.

Hizi jamii za kichawi, kama secrete societies zingine hutoa sadaka na kufanya vitimbi vya hapa na pale vyenye lengo la kuwaaminisha watu kuwa wao wana nguvu zisizoonekana.

Lakini ukweli ni kuwa kama zilivyo jamii zote za siri, mambo haya yanagundulika na walio wengi kuwa si kweli. Wale wanaodanganyika wanabaki kuishi kwa hofu na wakati mwingine enzi hizo watu walilazimika kutoa kitu kidogo kwa wachawi ili wasirogwe. Huo ndo uchawi.

Ukiogopa vitimbi vyao, utajisalimisha kwao na kuwapa kitu kidogo ili wakulinde na uchawi.

Jamii ya wachawi ina umri mrefu kuliko hata dini zetu nyingi, ambazo nazo zimetumia mbinu kama zile zile wanazotumia wachawi kupambana nao. Mbinu wanayotumia wachawi ni kutangaza uwezo wa kudhuru watu kwa kutumia "magic". Dini zinatumia "nguvu za kimungu" kupambana na wachawi. Nguvu zote hizo ni 'supernatural'.

Kwa mtu mwenye scientific knowledge ya mwili wa binadamu na mazingira yake, uchawi ni kama hadithi za riwaya kwake na hauna madhara yoyote!

Huo ndo uchawi!
Yaani hata hueleweki, umeanza thread yako vzuuuuuri kwamba huamini ktk uchawi, lkn ktkt ya thread yako umeeleza jinsi uchawi ulivyo na matumizi yake, Ni kweli uchawi Ni nguvu zisizo onekana kwakuwa wachawi Kama wachawi nguvu zao ziko kiroho kuliko kimwili kwa Hali kawaida huwezi kuziona na umekiri ktk mstari wako wa mwisho kwamba huo ndo uchawi, Sasa hebu jipambanue zaidi....maana hata wanasayansi wako hao wanaokudanganya CERN hawana jipya lakuanza ktk project yao yoyote ile mpya lazima watoe kafara ya mtu, hii inaonyesha ktk kuamini nguvu flani zitokanazo na ushirikina...mungu mwenyewe ushirikina kauzungumzia, Sasa hebu jipambanue wewe unaamini ktk lipi...
 
Hayajakukuta ndio maana unaongea hivyo.ila omba Mungu usikutane na haya mambo
Ila kama unaamini Mungu yupo basi amini uchawi upo,ila kama huamini uwepo wa Mungu basi uchawi haupo
Mr Masodas naungana na wewe
Nikweli kama hayaja kukuta unaweza ukaamini hayo mambo hayapo lakini kama yamekukuta kama mimi apa unaweza ukakubali bila ubishi hayo mambo yapo
Mfano mimi mwaka 1999 majila ya saa 09 usiku nilikuwa nimelala nikabanwa haja ndogo ikabidi nitoke nje, baada yakutoka nikapiga hatua kazaa kulikuwa kalibu na shamba la mahindi nikasimama ile nataka kujisaidia nikaona kama paka ananijia
Maraghafla huyo paka akabadilika na kuwa binadamu tena wakike akiwa uchi niliogopa sana ilikuwa usiku wa giza. ile kujihami ikabidi nipige kelele huku nikiludi nyuma
Huyo mtu akapotea ghafla namimi nikakimbilia ndani siku hiyo sikupatwa na usingizi.
Kesho yake ashubuhi tulipo enda kuangalia sehemu lilipo tokea tukio hatukuona hata unyayo
Baada ya siku 3 nikaugua sana
Ndo nikaamini uchawi upo
Ukiona mtu ana bisha jua hayajamukuta
 
Siku ukibahatika kuwa na jicho la tatu angalau kwa dk. chache ungeona ulimwengu wa roho na ungeamini. Mbona dunia nzima inaongozwa na ulimwengu wa roho? Dini ni fix tu kukupumbaza
 
serikali lazima iseme haitambui uchawi kwani kesi ya uchawi ushaidi wake hauwezi kuwa rahisi kutolewa waziwazi lazima matendo ya kichawi yatumike sasa unafikiri hakimu atkubali kushuhudia vimbwanga mahakamani?
Mh hawezi kabisaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom