Siku nyingi nimekuwa siamini kama kweli kuna uchawi katika Tanzania hii, achilia mbali huko kwa wengine. Nimekuwa siamini kwa sababu makosa yote hapa nchini yana adhabu zake isipokuwa la uchawi hii ikimaanisha kuwa Serikali inaamini kuwa hakuna uchawi.
Hatahivyo, siku za hivi karibuni imani yangu imeanza kupungua baada ya Kiongozi mmoja katika Serikali hiyo hiyo inayoamini kuwa hakuna uchawi kudai kuwa amegundaua mbinu kuwa anarogwa ili awe zoba auwawe kirahisi.
Sasa nikajiuliza, huyu mtu yumo ndani ya Serikalini inayoamini kuwa hakuna uchawi, akiwa pekee yake kuna uchawi, inakuwaje hapa?
Aidha, jana tarehe 28/03/2011 nilikuwa nasikiliza Redio Wapo FM kuanzia saa 1.30 jioni kipindi cha "yaliyotufikia" nikasika kuwa kuna fisi ameshambulia watu huko Mto wa Mbu, akauawa na askari wa wanyama pori, baada ya kuuawa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereni.
Je, huyu fisi alikuwa anashiriki mashindano ya "Miss Mto wa Mbu" au ni fisi wa wachawi?
Sasa wana JF wenzangu ni kweli kuna uchawi? Au ni njama za wajanja kutishia wenzao.