Je unaamini kuna siku michepuko itaisha ?

Je unaamini kuna siku michepuko itaisha ?

Mgegedo

Member
Joined
Jan 19, 2018
Posts
91
Reaction score
89
Kuna huu msemo unaosema kwamba "mwanaume by nature yupo kwaajiri ya wanawake wengi" na ndio maana ni ndoa chache sana ambazo hazihangaiki na michepuko

Siku hizi kama mwanaume yupo kwenye ndoa hana mchepuko basi inawezekana mkewe akawa na mchepuko au asiwe nao, hayo yote yanawezekana.

Makala nyingi sana zimeandikwa kuwasihi wakinadada watafute waume zao wenyewe ili wasitembee na waume za watu kitu ambacho kwa namna moja au nyingine naweza sema ni kama kumpigia mbuzi gitaa kwa dunia ya sasa.

Wapo wanawake ambao akigundua kwamba unamtongoza wakati una mke hawezi kukubalia ombi lako na wapo wanawake ambao hata ukimwambia kwamba umeoa na una watoto yeye hajali na anachojali zaidi ni maslahi yake hasa ya kiuchumi.

Kuna wanawake wengine huenda mbali zaidi ya kuomba hata apangishiwe nyumba na mume wa mtu na anakua hajali chochote kile kwamba jamaa ameoa au la.

Je kwa mtazamo wako wewe kama kijana mwenzangu, kuna siku unahisi michepuko itaisha kabisa na watu kutulia kwenye ndoa zao ?

Karibuni tuweze kubalishana mawazo
 
Lamda wanawake waishe lakini sio kuchepuka.

Kama kuchepuka kulianza zamani henzi za manabii wa Mungu ni ngumu kuisha kwa dunia ya sasa!
 
Lamda wanawake waishe lakini sio kuchepuka.

Kama kuchepuka kulianza zamani henzi za manabii wa Mungu ni ngumu kuisha kwa dunia ya sasa!
Unaweza hata ukachepuka kwa mwanamke aliyeolewa so hata waliosingle wakiisha bado game litaendelea
 
Back
Top Bottom