Je, Una maoni gani juu ya mahari?

Je, Una maoni gani juu ya mahari?

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,508
Reaction score
13,975
Wadau MMU heshima kwenu,

Je, wewe binafsi unakubali watu waoane kwa kulipia mahari,au waoane Free of charge?"Mahakama ya juu zaidi nchini Uganda imesema kuwa utamaduni wa kurejesha mahari baadaya talaka katika ndoa za kitamaduni unakiuka katiba na utamaduni huo unapaswa kupigwa marufuku.

Uamuzi huo wa majaji saba katika mahakama hiyo umetolewa baada ya wanaharakati wa haki za wanawake kuwasilisha kesi mahakamani wakisiema kuwa utamaduni huo unawanyima wanawake haki zao.

Jaji mkuu wa Uganda Bart Magunda Katureebe amesema kuwa ikiwa utamaduni huo utaruhusiwa kuendelea itakuwa na maana kuwa wanawake ni kama bidhaa zinazouzwa sokoni.

Lakini idadi kubwa ya majaji hao walikubaliana na uamuzi kwamba utamaduni wa utoaji mahari unapaswa kuendelea na kwamba haukiuki katiba.

Hata hivyo mmoja wa majaji hao alisema kuwa utamaduni huo unawadhalilisha wanawake na kwamba mahakama inapaswa kulifanya swala la ulipaji mahari kuwa chaguo na wala sio sharti."

Chanzo: BBC Swahili
 
iweee free tu banaa ilii tukizinguana hakunaa mtu anaumia moyo wake kwa kutoa
ela yake hvyooo iweee freee tuu
 
Kurejesha mahari baada ya talaka???

Hao waganda wazima kweli????

Arejeshewe mahari...na ule utamu wa kukeshea k ataurejesha????

Loh

Anyway mahari ni kautamaduni...mradi isiwe ya kukomoana
 
Kurejesha mahari baada ya talaka???

Hao waganda wazima kweli????

Arejeshewe mahari...na ule utamu wa kukeshea k ataurejesha????

Loh

Anyway mahari ni kautamaduni...mradi isiwe ya kukomoana

We mndenge nini?
 
kwa hiyo kumnunua mtu wameona ni sawa haivunji au kushusha utu wa mwanamke!!!
maana siku hizi tunauziwa na sio kuozeshwa.
mtu unaambiwa sijui mbuzi wa mjomba 200000!
hivi kweli kuna mbuzi wa laki mbili??
hapo bado hujapangiwa ng'ombe sijui takataka gani zingine!!

mpaka vijana wanaogopa kuoa
 
Nna swali moja kuhusu hii kitu Mahari: Ni kweli kwa baadhi ya makabila, mahari huamuliwa na msichana anayeolewa na si wazazi?
 
Yaani binti wa watu umtoe usichana wake then akurudishie mahari mkiachana!!hao madishi yameyumba basi nao wadai usichana wao pia wakiachika
 
mahari ni lazima na inahesabika tu kama shukran kwa wazazi na kamwe c kumnunua msichana.
 
kwa mtazamo wangu mahari iendelee kwa maana ni utamaduni wetu. wazee wa zaman waliipitisha hii sheria ili kuwafanya watu wajue kwamba ndoa sio kitu cha lele mama. na pia kuepusha yale mahusiano ya chipsi funga au ndoa za madanguro. sema katika suala mahari serikali inatakiwa kusisitiza kwamba mahari hata hutoe kiasi gani hairudi na suala la mahari liwekwe kwenye katiba ili kuepusha migogoro but for me bride price is the big idea
 
Mahari ni zawadi kutoka kwa mume anamzawadia mkewe na hakina limit kiasi gani,anaweza kumpa hata pete inategemea na uwezo wake,lakini sema sikuizi ndio kuna sijui mkaja,kilemba,bado sijui nini,few weeks ago rafiki yangu brother wake alipewa list ya mahari wallah nyengine hata sikuvijua ilibidi niulize ndio nini? KIBANI,MAJEMBE,MKAJA WA MAMA,BIBI WA BINTI,MJOMBA WA BINTI,SHUKA,BLANKET,KONDO,NG'OMBE,FEDHA YA NDANI, yani imekuja karibuni m7 manake wana ta kwa number nikajiuliza majembe anakwenda kulima? au blanket sijui shuka yani vitu Weird why wasinge sema tunataka just 7m full stop..yani niliishia lijiuliza jibu sikupata tuka changa nikawaachia na majembe na mashuka yao..
 
Nna swali moja kuhusu hii kitu Mahari: Ni kweli kwa baadhi ya makabila, mahari huamuliwa na msichana anayeolewa na si wazazi?

Kwa upande wa waislam mahari ni maelewano ya wanaooana tuu. hakuna cha hela ya babu wala nn. Labda tuu mtu ataoe kwa upendo wake. Ila msichana ana uhuru ata wa kusema mi nakwenda buree
 
Kwangu mahari inafaa kua zawadi kutoka kwa muozwa kwa familia anayeolewa. Kwa hivyo inafaa kuwa chochote kile anachoweza, akileta kidogo aibu kwake, akileta kikubwa sifa kwake. Cha msingi ni kwamba aape kuwa atamtunza bibi.
 
Yaani binti wa watu umtoe usichana wake then akurudishie mahari mkiachana!!hao madishi yameyumba basi nao wadai usichana wao pia wakiachika
Binti umtoe usichana? Huyo binti wa kutoa usichana utampata wapi?
 
Binti umtoe usichana? Huyo binti wa kutoa usichana utampata wapi?
binti wa mwenye nyumba, mara nyingi ukipanga unakuwa unamuona still yuko mbichi akiiva unawahi, unatumbua jipu then utakuja oa na baba mkwe atakukatia kiwanja, hii imewata baadhi ya vijana
 
Mahari ni utamaduni unaopaswa kuendelezwa. Kinachoiudhi jamii nyingi zimefanya mahari kama dili.
Tangu nakuwa na akili sijawahi kusikia mahari imezidi laki tano kule Moshi kijijini kwetu. Hivi majuzi jamaa yangu amechumbia Rombo - K'njaro binti amesomeshwa mpaka shahada, na anafanya kazi, ila ametozwa laki tisa tu (tena ana uhuru wa kulipa kidogokidogo).
Sasa kuna baadhi ya jamii, kama Wahehe, Wabena, watu wa kanda ya ziwa, ...) wanatoza mahari ya milioni kadhaa.
Kuna jamaa yangu ametozwa 3.2 m huko Njombe, tena kijijini. Fedha ambayo mtu ananunua kiwanja na kujenga nyumba ya heshima maeneo hayo.
Mbaya zaidi, ukweni wakipata matatizo wanataka mchangie, ili hali waliwahadhibu kwenye mahari.
Kuna jamii mpaka sasa, japo wameelimika, wanahisi mahari itawapunguzia ugumu wa maisha.
Ikumbukwe kwa asilimia kubwa mahari hulipwa na mwoaji, si familia ya anayeoa.
 
Sitaki kutolewa mahari.

Wengine tuko na watu wa utamaduni tofauti, mimi ndo wa kulipa. Nimemwambia nikitoa mimi nitakuwa nakudunda...
 
DINI ZOTE ZIMEWEKA UWEPESI KWENYE SUALA LA MAHARI, SI VEMA KUOA BILA MAHARI MAANA MAHARI NI KAMA ZAWADI AMBAYO MUOAJI ANAMPA ANAYETAKA KUMUOA KAMA ASANTE YA KUBALI KUOLEWA NAE. SIKU HIZI MALI IWEKUWA MRADI WA WAZAZI WA BINTI SO IMEFANYA SUALA LA KUOA KUWA GUMU WAKATI DINI INASEMA UNAWEZA KUOA HATA KWA PETE YA CHUMA CHA MSINGI UTOE KITU CHOCHOTE.
 
Back
Top Bottom