Je, umewahi kutafakari baada ya kuondoka kwako duniani?

Aandike tu wosia kuwa siku akifa basis pro box yake ndo iwe jeneza,mmbona Kule nijeria watu wanazikwa na magari yao.

Kuhusu msambwanda hata asiwaze maana bado yuko hai lakini bado wanamgongea.
Haahaaa Aseee


Kwenye msambwanda umeua ....ni wanamgongea akiwa hai
 
Amani ya mwenyezi Mungu iwe nanyi wapendwa
Naomba nianze na kisa hiki kilichonipelekea kuandika haya hapa. Nina ndugu yangu alifariki miaka kadhaa nyuma akaacha watoto wanne wadogo wadogo wa kwanza akiwa darasa la kwanza. Wakati wa kifo chake nilikua shule hivyo sikuhudhuria mazishi na baada ya kuuliza kchanzo cha kifo chake nikaambiwa ilikua ghafla ikabaki hvyo.
Sasa basi hapo majuzi nilipata wafadhili wa kusaidia wale watoto wakahitaji uthibitisho wa cheti cha kifo nikamuuliza mume wake akanipa. Baada ya kupitia kile cheti nikaona chanzo cha kifo kikiwa ni kutoa mimba, hii nadhani alifanya hivo kutokana na aibu ya watoto wadogo wadogo aliokua nao na kwa bahati mbaya ndio ikaondoa uhai wake.
Kile cheti kimenipa kutafakari sana. Tafakuri yangu naomba mimi na wewe tunaoamini kuwa kuna kufa na kuna siku ya hukumu ambapo kila mmoja atasimama mbele ya mola wake kupewa hesabu yake.
Je umewahi kujiuliza kila unachokifanya duniani ukiondoka nani atakisafisha kikiwa kibaya? Je hizi account za social media nani atafuta picha chafu tunazoweka? Je comment tunazozitoa mfano kusifia uzinzi, ulevi refer yule jamaa aliekua anajisifua tarehe falani atafikisha miaka 15 na mchepuko wake? Je hili bandiko nani atalifuta akitangulia mbele ya haki? Picha za ngono zinazopostiwa nani atazifuta? Cheti cha kifo ambacho hutokiano lkn tunaobaki tutakisoma je cheti hiki kitaoneaha umekufa kwa kifo kipi? Kujiua? Kujinyonga? Kutoa mimba tena sio kwa sababu za kiafya bali tu huhitaji mtoto? Mungu atusaidie.
Hakika hiche cheti cha ndugu yangu kimeniumiza sana
Sad
 
Jaribu kutokuwaza Mambo ambayo huezi badilisha kwenye maisha yako..itakusaidia sana
Shukrann Ila ktk kutafakari mambo ndipo mambo mapya huzaliwa ambayo yanaweza kukufanya uwe Bora zaidi ya ulivyo
 
Back
Top Bottom