Je, umewahi kusikia Parallel Universe na story ya A Man from Taured?

ALEX_ANDER

JF-Expert Member
Jul 8, 2014
570
812
Katika Sayansi ya anga,Ulimwengu na Teknolojia zake kuna kitu kinaitwa "Paralle Universe" au Ulimwengu sambamba, huu ni ulimwengu "dunia dhahania" ,ambao unasemekana kuwepo ingawa haugunduliki.

Ulimwengu sambamba unasemekana kuwa na mfanano wa mambo fulani na ulimwengu huu wetu asilia lakini kuwa na utofauti wa njia na misingi ya kikanuni "laws of universe"

Man From Taured.

Mnamo 1954, Mtu mmoja akiwa kama msafiri mfanyabiashara,aliwasili katika uwanja wa ndege wa Tokyo na passport iliyotolewa na nchi iitwayo "Taured" ambayo kiuhalisia haipo katika ulimwengu wetu.

Alidai kuwa nchi yake ina miaka 1,000 na pia alikuwa na rekodi zinazoonyesha kwamba alikuwa ametembelea Japan mara kadhaa hapo awali.Lakini Polisi hawakuridhika na maelezo yake hivyo walimuweka chini ya uangalizi wa uhamiaji ndani ya chumba chenye uangalizi mkubwa wa usalama kwa ukaguzi zaidi,ila alipotea katika mazingira tatanishi na hakupatikana tena. Simply wataalam walisema kwamba alikuja kutoka "Parallel Universe".

Kwa hiyo unaweza kukuta kuwa kuna kopi ya mtu kama wewe kwenye ulimwengu sambamba mwingine / parallel universe

 
MKUU UKITAKA KUFAHAMU VEMA MASUALA YA PARALLEL UNIVERSE NA TIME TRAVEL TAFUTA SERIES ZINAITWA
1.THE FLASH
2.DARK
MKUU UTAENJOY SANA ILA ANDAA KICHWA CHAKO VEMA HASA HIYO DARK.
 
Back
Top Bottom