Je, umepitia changamoto katika maisha yako, lakini baadae ukaona si changamoto bali ndio maisha yako halisi

truth1990

Member
Jan 8, 2022
26
53
Unajua kuna tofauti kati ya kukata tamaa na kukubali matokeo.

Katika maisha unaweza ukazaliwa mzima kabisa yaani sio mlemavu wa kiungo chochote cha mwili, na ukaona mtu aliyezaliwa mlemavu labda ni kama ana wakati mgumu kidogo maishani tofauti na wewe kumbe sivyo.

Sasa kuna wakati mtu unapitia changamoto nyingi saana kwenye maisha yako na unapambana saana
Lakini bado mambo yanakuwa magumu,, inafika kipindi unajiuliza 'ivi hii ni changamoto au ndio maisha yangu halisi'

Back to the topic,, kama vijana wengine wengi, mimi pia nilikuwa na ndoto zangu,,

Nimepitia changamoto nyingi saana za kunikatisha tamaa,, changamoto za kuniumiza,, za kunirudisha nyuma na hadi sasa nipo katika middle 20's, lakini kila nikijitathimini bado sioni muelekeo mzuri wa maisha yangu.

Nimejihidi sana kumuomba Mungu, (namshukuru sana Mungu kwa hapa aliponifikisha) lakini bado changamoto haziishi na kibaya changamoto ni zile zile,,sasa inafika muda kama binadamu nachoka.

Naanza kuhisi labda haya ndio maisha yangu,, lakini inakuwa vigumu kukubali.

Nafanya sana kazi, najituma sana, lakini bado siendelei na ikitokea nimepiga hatua basi ni kidogo sana na kwa nguvu kubwa sana. Changamoto ni nyingi saana siwezi kuziweka zote hapa

Kwa kweli inahuzunisha sana.

Kama na wewe unapita changamoto kwa muda mrefu hadi unahisi labda ndio maisha yako,, unaweza ukashea nasi, karibu..
 
Mara ya kwanza, nililima tikiti eka 3, kilimo kilinigharimu Sana, mwisho mazao yapo tayari kuvuna, wenyeji wakaiba usiku, ulikuwa usiku wa mbalamwezi, full moon, sitosahau, nikaapa, sitolima kilimo cha kuagiza. Na nikajifunza, mazao yakikaribia kuvunwa naweka mlinzi wa mchana na usiku, namlipa hela ndefu, labda wiki 100,000 au laki na nusu, na simwambii mtu lini navuna, wenyeji wanashtukia Tu mzigo unaondoka!

Mikoa ya wavivu, wacheza hao, watoto wao ni wezi Sana!
 
Maisha ni safar ndefu sana....mm nipo late 30s lkn bado bila bila na nina degree 2 za chuo kikuu! Life sometimes unaweza ukajitupia kamba kama ukizingatia sana changamoto zinazokukabili.....kikubwa ni kupiga moyo konde na kuendelea kupambana pamoja na kumuomba Mungu bila kukata tamaa iko siku utafanikiwa.
 
Maisha ni safar ndefu sana....mm nipo late 30s lkn bado bila bila na nina degree 2 za chuo kikuu! Life sometimes unaweza ukajitupia kamba kama ukizingatia sana changamoto zinazokukabili.....kikubwa ni kupiga moyo konde na kuendelea kupambana pamoja na kumuomba Mungu bila kukata tamaa iko siku utafanikiwa.
Daaah aisee mkuu acha tu,, kweli inasikitisha sana
 
HAKUNA SIKU CHINI YA JUA UTAKAYOMALIZA SHIDA ZAKO ZOTEE...TUPAMBANE KUTATUA CHANGAMOTO MUHIMU
Uko sahihi! Shida tumezikuta na tutaziacha, na ni ukweli usiopingika, tupambane kutatua changamoto muhimu, mengine unapotezea! Maisha ni matamu na ndiyo haya haya!
 
Kuwa imara sn.Safari bado ndefu.Wakati mwingine usiseme nimeshindwa bali maisha ni jino kwa jino sawa ee.


Me nimekuwa na roho mbaya sana sasa,ni kutokana na hali halisi niliyopitia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom