Je, umekosea au umeshindwa?

Meizon

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
279
105
Habari zenu wakuu, tunaonana kwa Mara nyingine. Inasemekana kusoma kitabu au hata jarida na nakara yoyote ni sawa na kupiga story na muandishi husika, hivyo ukisoma kitabu cha Donald Trump basi unapiga nae story pia, ukisoma Bible?

Ok leo unapiga story na mimi mtanzania mwenzenu, Leo tugusie sehemu nyingine muhimu inayo athiri sana dira ya mafanikio yetu, KUKOSEA. kukosea ni sifa ya binadamu wote kutokana na kwamba hakuna binadamu alie kamilika. Hakika tutaitazama sifa hii ya binadamu kwa mtazamo chanya, lakini kabla ya hilo nitoe ushuhuda mfupi; Mada hii imenilazimu kuiandika Mara mbili kwani nilishaiandika kirefu na kiufasaha sana, nilichukuwa zaidi ya dakika 40 kuiandika ila kwa bahati mbaya ikajifuta yote hivyo nimejaribu kuirudia kifupi japo imenichosha sana. Nilikosea ila Sikushindwa.

Zifuatazo ni faida au taswira chanya za kukosea;


KAMA HUKOSEI BASI UNAKOSEA:Inaweza kuwa ngumu kuelewa, ili ujue unachokifanya kinafanyika kiusahihi basi hunabudi kukabiliana na makosa. Mtoto anaejifunza kutembea huanguka Mara kadhaa na kuanguka kwake kutokana na makosa huwa mwalimu wake. Nasema hivi kwasababu huwezi jua jambo lolote na kulifanya kwa ubora bila kukosea.
2d2dabcd7b5c8b052541ad6ff8ca5eb6.jpg

KUNA TOFAUTI KATI YA KUKOSEA NA KUSHINDWA: Hapa wengi huchanganya ila leo tutajua tofauti iliyopo; Kukosea kutakuonesha udhaifu uliopo katika kile ukifanyacho wakati kushindwa ni kukubaliana na udhaifu huo. Hivyo Mara nyingi kama si zote tunakosea kabla ya kushindwa, tatizo wengi wakikosea wanafikiri wameshindwa.

Wanaofanikiwa hugeuza makosa yao kuwa chachu iwapayo tamaa ya kurudia kwa ufanisi zaidi. Wanaoshindwa hugeuza makosa yao kuwa sababu ya kukata tamaa.



PENDA KUFANYA MAKOSA MAPYA: Kama tukikosea tutasikitika na kusahau basi haisaidii, ila kama tutakosea kisha kutafakari na kusoma kosa hapo hujakosea kabisa, kutenda kosa si kosa Bali kurudia kosa.

A life full of new mistakes is a life full of knowledge intakes. Shame is not in making a mistake but in not trying at all.


Mara nyingi kabla ya kufikia mafanikio huwa kuna mlolongo wa makosa njiani, hivyo kila aliefanikiwa ni lazima alikosea lakini si kila anaekosea hufanikiwa.

Tofauti huja baada ya kukosea na si kabla. Mwanajeshi hodari si Yule asieanguka kabisa bali yule ambae kila akianguka husimama na kusonga mbele.

Never GIVE UP, always GET UP


Tukutane wakati mwingine tena.
From Ardhinyeusi.wordpress.com
 
Back
Top Bottom