Je uliwahi kufika bar ya Lubumbashi kuzimu ya Dar sehemu ya 2,je unafahamu nyumba nyeupe?,Nani alimpa bastola God kichaa

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,665
Kwanza kabisa nikuombe IGP na waziri wa mambo ya ndani au wa njinsia na watu wenye elemavu mtenge muda mtembelea eneo la mbezi Louis (shule) mjionee kinachoendelea! , Risasi nje nje , bangi, ukahaba na ulevi uliopituliza 24/7

Nyumba nyeupe (pichani) ilijengwa miaka ya 1990 ila aliyeijenga inadaiwa na majirani aliuwa watu na kupora pesa zao kisha na yeye akauawawa kulipiza kisasa,sasa kila anyajalibu kuishi hupata mauzauza na kukimbia so haina mkazi ipo wazi geti la nyuma ,hili ni eneo la kufanyia biashara za mauzo ya madawa ya kulevya hasa heroine,bangi na cocaine huku wanaojiuza hutumia pia .

Mmiliki wa bar ya Gods pub,amekuwa akitishia watu na bastola na mara nyingi amekuwa anapiga watu kama alivyofanya wiki iliyopita,mamlaka zimpokonye hiyo bastola Maana anaugonjwa wa akili ,msisubili mpaka aue mtu


Mitaa iyozunguka hii nyumba imejaa madanguro ya machangudoa wanapopishana kwa shifti kila uchao,

Nyuma ya bar ya san siro kuna kikundi cha vijana wafanya mazoezi ya kubeba vyuma karibu na hapo kuna nyumba (guest) bubu , ndio walinzi kile kikundi cha machangudoa,kikundi hiki kinapaswa kuvunjwa kwani ndio chimbuko la wale machangudoa wale vijana ndio wakusanya pesa na wazima njia za kuingia huko wanakoishi machangudoa ,polisi wakipige marufuku

NINI KIFANYIKE

1.Wenye nyumba wote waliowapangisha wabainishwe na kuchukuliwa hatua ikiwa kuwafukuza wapangaji wote wanaojiuza eneo hilo.

2.kufanya msako wa machangudoa hasa mida ya kazi na usiku mkali ili kulinda kizazi cha sasa (watoto )ambao hapo kuna shule mbili kubwa za mbezi na upendo.

3.kuondoa vizuizi vyote vya mawe na magogo walioweka kuziba eneo lao lisifikiwe na mamlaka

4.Polis wavunje kikundi cha vijana wafanya mazoezi ya kubeba vyuma wanaowalinda hao machangudoa

5.Eneo lote kuwekewe muda maalum wa zuio la Mtu yeyote kuonekana kuanzia saa 6 usiku ,bar zote zifungwe na asionekane changudoa angalau mwezi mmoja

USSR
IMG_20230507_130129_473.jpg
 
Kitaa changu unakiandama sana, haya yapo kabla hata Magufuli hajawa Rais umefika Makaburini na Dubai?

Bar unazozitaja mbaya kimuonekano, chafu toka zamani hazina parking, malaya wapo toka kale japo walijikita zaidi kabatini
 
Mwezi uliopita nilienda dar nikawa maeneo ya sinza na tabata,niliyoyaona hakika nilijisemea dar sio sehemu salama tena kuishi na familia,malaya wamejaa mpaka kwenye makazi ya watu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom