Je, uko tayari kufa kwa ajili ya dini?

Je, uko tayari kufa kwa ajili ya dini?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Wengi wetu tumezaliwa na kupewa Dini aidha Uislamu (uarabu) au Ukristo (Uzungu), sasa Je, uko tayari kufa kwa ajili ya hiyo Dini?
 
Wafia dini walikuwepo kitambo wakati dini bado ilikuwa ya kweli
 
Hata makabila nayo hutokana wazazi wetu ila pia watu hujivuniya niyo na wengine hubagua wenzao kutokana hayohayo makabila.
 
Mimi siko tayari kufa kwa ajili ya dini, sababu ni hizi hapa;
1. Yesu mwokozi alishakufa, hivyo nife mimi ili nimwokoe nani?
2.Dini nimezikuta na hata nikafa bado wataziendeleza tu iwe kwa haki au kwa ulaghai kama wafanyavyo baadhi ya watumishi wa shetani huku wakitumia Neno la Mungu.
3.Siendeshwi kwa mihemko bali Neno ambalo ndilo taa kwangu.
 
Kama huwezi kufia imani yako basi huwezi kufia kingine chochote
 
Mimi siko tayari kufa kwa ajili ya dini, sababu ni hizi hapa;
1. Yesu mwokozi alishakufa, hivyo nife mimi ili nimwokoe nani?
2.Dini nimezikuta na hata nikafa bado wataziendeleza tu iwe kwa haki au kwa ulaghai kama wafanyavyo baadhi ya watumishi wa shetani huku wakitumia Neno la Mungu.
3.Siendeshwi kwa mihemko bali Neno ambalo ndilo taa kwangu.
 
id.jpg
 
niko tayari kufa kuitetea imani yangu lakini sio dini. wenye kujua nadhani wamenielewa
 
Mimi siko tayari kufa kwa ajili ya dini, sababu ni hizi hapa;
1. Yesu mwokozi alishakufa, hivyo nife mimi ili nimwokoe nani?
2.Dini nimezikuta na hata nikafa bado wataziendeleza tu iwe kwa haki au kwa ulaghai kama wafanyavyo baadhi ya watumishi wa shetani huku wakitumia Neno la Mungu.
3.Siendeshwi kwa mihemko bali Neno ambalo ndilo taa kwangu.
Walioishi kabla ya ujio wa Yesu na kifo chake je wao inakuaje?
 
Nitaifia nchi yangu tu.

Hayo mengine yakwende huko.
 
Kwa dini big no. Ila kwa ajili ya YESU HATA SASA NIKO TAYARI.
Dini si inatoa mafundisho yake kwenye biblia? na wewe hizo habari za Yesu pia si umezitoa humohumo kwenye biblia?
 
Ni makosa kuchambua kuwa Uislam ni uarabu na Ukristu ni uzungu.. Hao ni waliofanikiwa kuzifikisha hizo dini hapa nchini kwetu Tz lakini sio kuwa ni wao ndio waliosambaza hizo dini duniani kote pia sio kuwa hizo dini ni za kwao, dini ni za M. Mungu.
 
Back
Top Bottom