Je, uko tayari kufa kwa ajili ya dini?

Je, uko tayari kufa kwa ajili ya dini?

Mimi siko tayari kufa kwa ajili ya dini, sababu ni hizi hapa;
1. Yesu mwokozi alishakufa, hivyo nife mimi ili nimwokoe nani?
2.Dini nimezikuta na hata nikafa bado wataziendeleza tu iwe kwa haki au kwa ulaghai kama wafanyavyo baadhi ya watumishi wa shetani huku wakitumia Neno la Mungu.
3.Siendeshwi kwa mihemko bali Neno ambalo ndilo taa kwangu.

Yesu alikufa kwajili ya imani na sio dini.
 
Mkuu mimi swali lako sijalielewa. Dini ni imani tu, ni njia inayotumika kuwasiliana na mungu, ni jambo la rohoni zaidi na wala siyo 'kitu'. Sasa labda unambie, au nipe mfano, kufa kwa ajili ya dini kivipi?

Wanaokufa kwa ajili ya dini nadhani ni wale 'wajinga' ambao hudhani 'dini' ni kama gari, pikipiki, mtu, n.K. Kumbe ukifa dini inaendelea kuwepo na hata ukiwa hai dini ipo tu na haiwez kufa kwa sababu inaishi kwa msingi wa kiroho.

NB: wanaokufa kwa ajili ya dini ni sawa na wale wajinga wanaonunua biblia na kuzichoma wakidhani biblia ikiungua na dini inakufa, kumbe wakichoma copy 1000 zinachapishwa zingne milioni 1. Teh!
 
Naamini MUNGU ni mmoja ila dini ni mfumo wa maisha ili kupunguza maovu duniani.

imaNi ni kuwa na yakini moyoni kwa kitu amabacho hakipo.......

Dini ni zao la mwarabu na mzungu.....

Before kuja hao waatu... mababu zetu walikua wanaishi kwa utamaduni wao mwingine na maisha yalisonga....

Huu tunaoishi sasa ni utamaduni wa kuiga amabao unatuletea madhara meengi saaana..... kuliko faida.

Ishi kwa akili yako na sio kusukumwa na maono ya wachache.....
 
Walioishi kabla ya ujio wa Yesu na kifo chake je wao inakuaje?
Wao watahukumiwa kwa matendo ya mwilini(sheria).Watakuwa wanahesabiwa mema yao na mabaya yao na kisha kufuata hukumu.
Kwa kizazi ambacho kimekuja wakati na baada ya Yesu hukumu itapitishwa kwa Haki/imani/ muhuri wa Kristo ndio utakaowatenga watu automatically.
 
Fafanua mtoa mada.
Unakufaje kwa ajiri ya dini ?
Una maana gani.
Toa sababu zinazosababisha mtu afie dini ili ueleweke.
 
,,,walokole wanaoheshimu wachungaji kuliko hata waume zao,waislam wanaopenda kuita wenzao makafiri wakati wao pia mikafir....

Hawa ndo watafia dini zao...
Really men and really women hutenda matendo mema sio waonekane makanisan na misikitini.......
 
Naamini MUNGU ni mmoja ila dini ni mfumo wa maisha ili kupunguza maovu duniani.

imaNi ni kuwa na yakini moyoni kwa kitu amabacho hakipo.......

Dini ni zao la mwarabu na mzungu.....

Before kuja hao waatu... mababu zetu walikua wanaishi kwa utamaduni wao mwingine na maisha yalisonga....

Huu tunaoishi sasa ni utamaduni wa kuiga amabao unatuletea madhara meengi saaana..... kuliko faida.

Ishi kwa akili yako na sio kusukumwa na maono ya wachache.....
Kuna vitabu vya Qur'an na Biblia,na hizi dini mafunzo yao huyatoa humo kuanzia kuelezea kuwepo kwa mungu na maelezo yenye kuhusu huyo mungu.

Je,kwa mababu zetu hali ikoje?
 
Wao watahukumiwa kwa matendo ya mwilini(sheria).Watakuwa wanahesabiwa mema yao na mabaya yao na kisha kufuata hukumu.
Kwa kizazi ambacho kimekuja wakati na baada ya Yesu hukumu itapitishwa kwa Haki/imani/ muhuri wa Kristo ndio utakaowatenga watu automatically.
Kwahiyo kizazi hiki hakihesabiwi maovu yao bali ukiamini tu Yesu mambo yameisha?
 
Mimi sifi kwa sababu za kipumbavu kama hizi! eti dini!!!
 
Back
Top Bottom