Je, Ukioa kuna kupata mafanikio ya maisha haraka?

Je, Ukioa kuna kupata mafanikio ya maisha haraka?

Umomi

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
677
Reaction score
994
Habari zenu wadau!

Leo nimewrudi tena kutafuta msaada wa mawazo yenu. Mimi ni kijana nina miaka 26 kwa sasa namshukuru Mungu kuwa napiga sana kazi na kuingiza kipato. Tofauti na siku za nyuma nilikuwa nakaa tuu na kulalamika kwa wingu.

Sasa niingie kwenye mada. Katika kupiga kazi huwa nakutana na watu mbalimbali hasa wanawake huwa tunapiga story za hapa na pale. Wengi wao huwa wananishawishi kuhusu kuoa na kuniambia kuwa nikioa maisha yatakuwa mazuri kwa sababu wengi wao hudai kuwa mimi naonekana ni mtu wa kuchapa sana kazi na hivyo nisipo kuwa na mke wa kunishauri kuhusu pesa niitapayo itakuwa ni bure.

Mimi nawambia sijawa tayari kuoa kwa sababu mwanamke atakuja kunivurugia malengo yangu, sina pesa ya kutosha ya kumhudumia mwanamke, na umri wa kuoa naona kama sijafikia make nilipanga kuoa nitakapo fikisha miaka 30.

Naombeni ushauri wadau
 
Kuna ukweli Fulani hapo kuhusu kuoa lakini inategemea huyo utakae muoa

Ila naweza kusema ni kweli kabisa
Asante kwa mchango wako mzuri, na wengi wanasema ukioa et hata pesa utaitumia kwa uangalifu sana je, n kweli?
 
Asante kwa mchango wako mzuri, na wengi wanasema ukioa et hata pesa utaitumia kwa uangalifu sana je, n kweli?

Ndio kuna ukweli kwasababu wanawake inasemekana wana uwezo mkubwa sana wa kuhifadhi au kutunza vitu na kisha kuvimultiplie

Ndio maana ukiona mwanamke ambaye anajua basi anajua kweli

Wanawake ambao wanajielewa ni viumbe bora sana kwenye maisha ya mwanaume yoyote

Ndio maana kuna msemo unasema kila kwenye mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke

Ni kweli kabisa na Mimi nimeshuhudia hili
 
Sawa sawa kiongozi
 
Wakati sahihi utafika, na vichocheo vyote vya mwili vitakuelekeza kuoa.

Vema uoe ukiwa na utayari kutoka ndani yako na sio nje.

Kuhusu mafanikio, inategemea na mwenza utakatempata (mwerevu au la/mfujaji au la n.k).

Mtangulize Mungu katika kila jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amina sana kiongozi. Umetoa ushauri mzuri wa kumtangulza Mungu
 
Umejua kumuumbua

Sent using Jamii Forums mobile app
Man tambueni kuwa maisha yanabadirika na angalia hyo tarehe nilioandika huo uzi. Kwahyo yawezekana mawazo yenu mliyochangia ktk huo uzi yalinifanya nikaanza kuchapa kazi. Na ktk pitapita zangu ndo nakutana na mambo kama haya niliandika leo

Kwahyo uzi wa April hawez kuwa kama ushahidi mkuu
 
Inategemea na Malengo yako.

For My Self
Kwangu mimi mafanikio kwangu ni kuwa uwezo mkubwa kifedha (Uhuru wa kifedha).

Kuna mipango kadhaa ya Malengo nimeshaipangilia kufikia huko, na katika Lengo moja wapo ili kutumia SAVING ni moja wapo ya njia nilizozipangilia kufikia kila lengo.

Kufanikiwa kwa Saving
_Kwangu kufanikiwa 100℅ ya saving zangu ili kutimiza Malengo yangu hususani kipindi hiki itanihitaji nisiww na mzigo wa majukumu hata kidogo (wazazi & Familia), wazazi ni jukumu la lazima siwezi epuka nitaji Balance tu niaitobolewe kilamara ila kwenye Familia nina uwezo wa kutooa kwasasa siwezi kuoa nikauwa 50℅ ya nachotaka Save kupeleka kuhudumia Familia.

Hitimisho; siwezi kuoa kwasasa hata mtu aniambie kitugani, nitaoa mpaka pale uchumi wangu utakuwa Stable, Saving itachukua muda mrefu kidogo kwenye mipango yangu ila jinsi uchumi utavyoanza kuji-Stable nitapunguza ila kwasasa hapana inabidi niwe solid ku-Save hivyo sitaki wataonifelisha.

Ila yote kwa yote kuna uwezekano nikaoa Before 30 age but ina depend na uchumi kwanza.
 
Habari zenu wadau!

Leo nimewrudi tena kutafuta msaada wa mawazo yenu. Mimi ni kijana nina miaka 26 kwa sasa namshukuru Mungu kuwa napiga sana kazi na kuingiza kipato. Tofauti na siku za nyuma nilikuwa nakaa tuu na kulalamika kwa wingu.

Sasa niingie kwenye mada. Katika kupiga kazi huwa nakutana na watu mbalimbali hasa wanawake huwa tunapiga story za hapa na pale. Wengi wao huwa wananishawishi kuhusu kuoa na kuniambia kuwa nikioa maisha yatakuwa mazuri kwa sababu wengi wao hudai kuwa mimi naonekana ni mtu wa kuchapa sana kazi na hivyo nisipo kuwa na mke wa kunishauri kuhusu pesa niitapayo itakuwa ni bure.

Mimi nawambia sijawa tayari kuoa kwa sababu mwanamke atakuja kunivurugia malengo yangu, sina pesa ya kutosha ya kumhudumia mwanamke, na umri wa kuoa naona kama sijafikia make nilipanga kuoa nitakapo fikisha miaka 30.

Naombeni ushauri wadau
Cha kujiuliza ni kuwa, wewe binafsi una mwamko wa maendeleo? Ukumbuke utakuwa kiongozi wa familia, na majukumu yatahusu familia tatu. Mke atafuata na kushauri pale wewe utakapoonesha njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAMA UNAONA KWAKO NI SAWA KUOA UKIFIKISHA 30 YEARS WELL IN GOOD, STICK WITH YOUR PLAN, VIGAGULA WASIKUTOE KWENYE RELI
 
Back
Top Bottom