Je, ukilipiwa kila kitu ili uweze kutembelea nchi moja kwa wiki mbili kila mwaka uirejee mpaka kifo chako,utaenda nchi gani?

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Swali ni jepesi tu;

Ikiwa utalipiwa kila kitu, yaani tiketi ya kwenda na kurejea unapoishi, malazi kwenye hotel ya hadhi nzuri kwa wiki mbili, chakula na fedha ya ziada kwa ajili ya kutalii, ukaambiwa uchague nchi ambayo kila mwaka utakuwa unakwenda hiyo hiyo bila kubadili mpaka kifo chako, utachagua nchi gani? Naomba ujibu kwa kuandika jina la nchi na sababu ya chaguo lako.
 
Nchi : USA
City : Sanfransinco Calfonia

Sababu
Ni mji wenye historia kubwa ya wajasiliamari wakubwa, wabunifu wakubwa, wawekezaji, mabilionea wakubwa pia makampunia makubwa yote yenye mafanikio yapo huko...napendelea mambo hayo.

Nawasilisha.
 
Kula vizuri au vibaya kunaweza leta mawazo tofauti na watu wasikuelewe.😆😆😆
Jibu swali, mbona ni rahisi tu, wewe unachagua nchi gani na kwa nini umechagua nchi hiyo? nitakujibu nimekula nini ukinijibu, mbona wataka kunitoa kwenye mada.
 
Nchi : USA
City : Sanfransinco Calfonia

Sababu
Ni mji wenye historia kubwa ya wajasiliamari wakubwa, wabunifu wakubwa, wawekezaji, mabilionea wakubwa pia makampunia makubwa yote yenye mafanikio yapo huko...napendelea mambo hayo.

Nawasilisha.
Asante sana ndugu. Umejibu vema, ngoja na wengine tuwasikie wanachagua nchi gani.
 
Japan
Kwa sababu wanamfumo mzuri wa elimu, ningependa watz tuige mfumo wao wa elimu ili kutengeneza wahitimu wenye kukidhi mahitaji
 
Back
Top Bottom