Je, ukikutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Magufuli utamwambia neno gani?

famicho

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,948
2,000
Habari wakuu,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, je utakuwa na neno gani la kumwambia mkuu wa nchi endapo utapata bahati ya kualikwa au kupata fursa ya kutoa dukuduku, maoni au ushauri juu ya mustakabali wa taifa kwa ujumla.

Tuache siasa,... Karibuni
 

ezma

JF-Expert Member
Dec 6, 2014
1,464
1,500
Hali ya uchumi ni mbaya sn wtz sasa tunamkumbuka Kikwete,, abadilishe mfumo wa kuongeza nchi uchumi hauhitaji mbwembwe za majukwaan na media
 

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,776
2,000
Anapoamua kuwa msema kweli, awe msema kweli, kweli na si vinginevyo maana akitumia kauli hiyo bila kuitendea haki ni kumdhihaki Mungu.

Ikowapi miezi miwili ya uhakiki aloyoahidi kwa sauti ya unyenyekevu? Sasa inaenda miezi mi5.

Ikowapi mikopo aloahidi wanafunzi wa elimu ya juu ktk kampeni? Sasa ni vilio kila kona.
 

MWAMFUPE

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
814
1,000
Habari wakuu,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, je utakuwa na neno gani la kumwambia mkuu wa nchi endapo utapata bahati ya kualikwa au kupata fursa ya kutoa dukuduku, maoni au ushauri juu ya mustakabali wa taifa kwa ujumla.

Tuache siasa,... Karibuni
mkuu mbona umechelewa kuleta uzi? NTAMWAMBIA ASIACHIE KITUFE, AKISHIKIE HIVYO HIVYO MPAKA MAJIZI NA MAFISADI YAISHIWE DAMU.
 

silasc

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
3,356
2,000
Anipatie kazi usalama wa taifa ili nitimize ndoto zangu za kulitumikia Taifa kiusalama.
 

abdallahtase

Member
Aug 20, 2013
37
95
Wakazi wa Mbagala tunapata tabu, wananchi wa eneo hii tunachangia pato kubwa katika taifa ila tunahisi kudharauliwa. tunasikia mipango ya usafiri wa treni kama wenzetu wa Gongongolamboto au wa mabasi ya mwendokasi kama wenzetu wa Kimara. kinachoshangaza kila siku ya Mungu barabara inatifuliwa na kuwekwa viraka viraka kama suruali ya tahira, isitoshe katikati ya barabara mbili tuliona panajazwa kifusi na kushindiliwa kiasi kwamba tukawa na matumaini lami inawekwa kukomesha foleni sasa imekuwa kinyume chake wameka vigingi vya zege na kusababisha taabu Zaidi kipindi cha dharura inapotokea ajali, sio hivyo inazuia magari ya dharura kama zima moto, polisi kama inatokea ujambazi, na magari ya wagonjwa ( Ambulance).
  1. Nakuomba mheshimiwa Rais utukumbuke wakazi wa Mbagala kwa kututengenezea barabara mbadala itakayotuunganisha na Yombo na Tandika.
  2. Hao wanaotifuatifua barabara kila siku wanajiwekea mazingira ya kula hela kifisadi, uchunguzi ufanyike na ikibidi watumbuliwe.
  3. Hivyo vigingi vya zege viondolewe kwa sababu sioni sababu ya kuzuia matumizi ya hiyo barabara inayotenganisha barabara mbili za lami. vigingi vinaleta usumbufu kipindi cha dharura
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom