Je, ukiambiwa tuma CV unapaswa kutuma na vyeti?

Habari wadau wa ajira,.

Naomba kuuliza hivi mtu akikuambia umpe CV yako yaani Curriculum vitae ana maanisha hiyo CV na vyeti au unaweza kutuma CV pekee yake?
Kwanini usimuulize uyo aliekuambia utume? Au ndo uoga kwamba itakushushia point? We uliza tu kwasab waajiri wanatofautiana.

Japo mimi nadhan umeagizwa straight kwamba utume cv, vyeti havipo ndani ya cv.
 
Tuma CV tu cheti utatuma baada ya kuona CV yako na kuridhika na wasifu wako
 
CV broo ni doc yenye taarifa za MTU katika kuelezea utambulisho wako(jina mahala ulipozaliwa mwakaetc) na taaruma yako sasa swali linakuja ndio umejieleza ktk CV yako lakin Huyo mwajili wako atathibitisha vip kama taarifa hizo ni za kweli bila kuweka vyet?
 
Vyovyote iwavyo ukiweka vyeti haisaidii kitu kama umeambiwa weka c.v. pekee...

Ni muhimu ukatambua yafuatayo.

1. Hakikisha c.v yako inaendana na vyeti ulivyonavyo au zaid.

2. Hakikisha kama umesoma taaluma zenye leseni kama Daktari, ufamasaia, uwakili, uhandisi nk vinaonekana kwenye c.v yako

3. Hakikisha kwenye CV kuna taarifa zako za kutosha kuhusu historia yako binafsi kama tarehe ya kuzaliwa, jinsia, anwani zako pamoja na uzoefu wako kitaaluma kulingana na kazi unayoomba.

Mungu akutangulie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom