Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,421
Ikiwa leo Disemba 09, 2018 ni kumbukizi ya uhuru wa Tanganyika miaka 57 iliyopita, nimeshangaa kuona wananchi hawaipi kipaumbele siku hii. Wapo kimya kama vile ni siku za kawaida. Sitaki kuamini kama tulipata uhuru kwa SILVER PLATE ndiyo maana hatuithamini siku hii.
Nimewaza sana, kwa mfano ikatokea WAKRISTO wakafuta sherehe za KRISMASI ama WAISLAM wakafuta sherehe za IDD EL FITRY, sielewi itakuwaje. Kwa maoni yangu, UHURU ni zaidi ya SHILINGI BILIONI MOJA.
Najiuliza, hivi watoto wadogo wanaochipukia wataelewa UHURU wao ni upi na watakuwaje WAZALENDO kama hawaoni harakati na shamrashamra za uhuru?
Hata yale MAGAZETI pendwa ya leo ya THE TANZANITE na JAMVI LA HABARI hayajaipa kipaumbele siku kuu ya leo.
Tusubiri tuone UHURU wetu wakati WAPINZANI wakisherekea hivi leo.