Je, Uhamiaji Tanzania wana mamlaka haya?

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
4,128
5,236
Habari wakuu,

Napenda kufahamu kutoka kwa wajuzi mbali mbali humu jf.

Je, mamlaka ya uhamiaji Tanzania inaweza kumchukulia hatua za kisheria mbongo yeyote aliyeamua kujiripua nje ya nchi,
kutafuta maisha,mfano alitoka hapa bongo akaenda Kenya akachukua passport ya Kenya akaenda DENMARK, alipofika kule akaomba hifadhi kama mkimbizi akakubaliwa akaendelea kuishi kule miaka zaidi ya nane.

Je, uhamiaji wanaweza kuwa na mamlaka ya sheria juu ya mtu huyu kuweza kumchukulia hatua zozote kama raia aliyetoka Tanzania?

Naomba kufahamu zaidi ikiwa mtu huyu aliondoka bongo kwa njia anazojua yeye na akaacha familia,ndugu na jamaa Tanzania.

ASANTE.
 
Kwa hiyo uhamiaji hawana mamlaka nae.....sasa kwa mfano uhamiaji wakimtuhumu ndugu yake kwamba kuna mashaka na uraia wake,je huyo ndugu anaweza kuwa na hatia kupitia historia ya safari ya ndugu yake aliye nje ya nchi kama aliondoka kihalali au alifoji ili afike nje?
Huyo sio mtanzania tena
 
Mkuu usisahau nchi yetu kwa mjibu wa sheria za uhamiaji haiutambui uraia pacha yaani uwe raia wa Kenya halafu wakati huo uwe raia wa Tanzania haitambui kitu kama hicho.Huyo jamaa yako kama amejiripua akapata pasipoti ya Denmark akitaka kuja Bongo nahisi atatakiwa kuwa na viza japo sina uhakika kama nchi zote wakitaka kuja Bongo lazima wawe na viza.Sasa huyo jamaa yako akikutana nao wale manjagu wa uhamiaji ataulizwa maswali Elfu 10.na hela watamtoza.
 
Atakuwa siyo mtanzania, kwa hiyo hata kuingia Tanzania ni kwa ruhusa.
vipi hawezi kuwaletea shida ndugu aliyowaacha hapa nchini kama aliondoka kwa njia za ukimbizi au alichukua pasi ya nchi jirani hali ya kuwa yeye alikuwa raia wa Tanzania?
 
Mkuu usisahau nchi yetu kwa mjibu wa sheria za uhamiaji haiutambui uraia pacha yaani uwe raia wa Kenya halafu wakati huo uwe raia wa Tanzania haitambui kitu kama hicho.Huyo jamaa yako kama amejiripua akapata pasipoti ya Denmark akitaka kuja Bongo nahisi atatakiwa kuwa na viza japo sina uhakika kama nchi zote wakitaka kuja Bongo lazima wawe na viza.Sasa huyo jamaa yako akikutana nao wale manjagu wa uhamiaji ataulizwa maswali Elfu 10.na hela watamtoza.
Asante......nilitaka kujua kama hao maafisa uhamiaji wanaweza leta sheria zao kwa kuwa aliondoka kwa njia za kufoji kama kutumia kigezo cha ukimbizi au pasi ya nchi jirani hivyo kuweza kuwatuhumu familia yake kwamba nyie sio raia kwa kuwa ndugu yenu aliondoka hapa bongo bila pasi au alitumia ya nchi jirani au alienda kwa njia zisizo halali?
 
Uhamiaji hawana mamlaka yoyote ya kisheria juu ya mtu alieamua kujilipua nje ya nchi.

Kwani mara nyingi raia hao huwa hawana pasi ya kusafiria ya Tanzania na zoezi la kujilipua likiiva basi hupewa hadhi ya ukimbizi na kisha pasi ya kusafiria ya nchi hiyo.

Ila wapo raia wa Tanzania ambao wamejilipua wakiwa bado wanahodhi pasi ya kusafiria ya Tanzania.

Sanasana huyo mtu ataandamwa na Uhamiaji endapo tu atakuwa "subject to national interest" na huyo mtu pia atakuwa "personal of interest".

Na ikiwa hivyo basi wapo Interpol ambao watasaidia kumtafuta kwa kuombwa na Uhamiaji na polisi.

Vinginevyo uhamiaji na serikali hawana shida na raia wake ambao wametokomea huko nje.

Lakini, huyo raia wa Tanzania huko nje aliko akivunja sheria za uhamiaji na akakutwa anamiliki pasi ya kusafiria ya Tanzania, basi mamlaka za uhamiaji za huko zitagharamia safari yake ya kurudishwa Tanzania kwa nguvu.

Wakifika Tanzania watamkabidhi raia huyo kwa Uhamiaji na mchezo utaishia hapo.

NB:

Suali lako naona linamlenga mtu fulani.

Ngoja tuone litavyokolezwa na maoni mbalimbali.
 
Uhamiaji hawana mamlaka
Ni uamuzi wa mtu binafsi kuikana nchi
Wala uhamiaji hawana mamlaka ya kuwasumbua ndugu zake
Kwanza uhamiaji wanapshwa kuwa na vithibitisho kama cheti cha kuzaliwa au passport otherwise ni kupoteza pesa za walipa kodi
Watasumbua wangapi?
 
````````````````

Nimekusoma mkuu........kama ikionekana alitumia pasi ya Tanzania kuvukia boda kisha huko alikoenda akaishi kama mkimbizi inakuaje hapo kwa ndugu zake kisheria?
 
Uhamiaji hawana mamlaka yoyote ya kisheria juu ya mtu alieamua kujilipua nje ya nchi.

Kwani mara nyingi raia hao huwa hawana pasi ya kusafiria ya Tanzania na zoezi la kujilipua likiiva basi hupewa hadhi ya ukimbizi na kisha pasi ya kusafiria ya nchi hiyo.

Ila wapo raia wa Tanzania ambao wamejilipua wakiwa bado wanahodhi pasi ya kusafiria ya Tanzania.

Sanasana huyo mtu ataandamwa na Uhamiaji endapo tu atakuwa "subject to national interest" na huyo mtu pia atakuwa "personal of interest".

Na ikiwa hivyo basi wapo Interpol ambao watasaidia kumtafuta kwa kuombwa na Uhamiaji na polisi.

Vinginevyo uhamiaji na serikali hawana shida na raia wake ambao wametokomea huko nje.

Lakini, huyo raia wa Tanzania huko nje aliko akivunja sheria za uhamiaji na akakutwa anamiliki pasi ya kusafiria ya Tanzania, basi mamlaka za uhamiaji za huko zitagharamia safari yake ya kurudishwa Tanzania kwa nguvu.

Wakifika Tanzania watamkabidhi raia huyo kwa Uhamiaji na mchezo utaishia hapo.

NB:

Suali lako naona linamlenga mtu fulani.

Ngoja tuone litavyokolezwa na maoni mbalimbali.
Sawa mkuu.....akivunja sheria za uhamiaji za huko aliko ndio anaweza kurudishwa bongo....vinginevyo kama si maslahi ya taifa huku hawataweza mgusa kisheria?
 
Yes, kama nilivyoeleza.

Na mara nyingi akirudishwa nchini hufikia mahakamani Kisutu ili kujibu mashataka ya kutoroka kwenda nchi za watu na kisha kuvunja sheria za uhamiaji za huko.

Kwenye maslahi ya taifa angalia mifano ya nchi kama Russia na China wanavyowashughulikia raia wa aina hiyo khasa wale wanoitwa "defectors".

Au usiende mbali sana mfano tunao wa jirani zetu Rwanda na kisa cha bwana Paul Rusesabagina.
 
Sawa mkuu.....akivunja sheria za uhamiaji za huko aliko ndio anaweza kurudishwa bongo....vinginevyo kama si maslahi ya taifa huku hawataweza mgusa kisheria?
Atawajibishwa kwa kuichafua inchi na kukana uraia wake.Mi Mwenyewe mgeni tusubiri wajuzi waje.
 
Ndugu hawana kosa lolote lile lakini kwa hapa kwetu na hizi sheria za kidikteta wanaweza kabisa kuwabambikia makosa ndugu wa muhusika.

Back
Top Bottom