Je tupo peke yetu? Are we alone?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,659
3,572
Miongoni mwa tafiti tata zinazofanywa na watafiti wa Marekani ni hii ya kutaka kujua je kuna viumbe wengine kama binadamu.

Utafiti huu kwa sasa unatumia 3D modeling huku ukihusisha kemia ya anga hewa ili kuangalia uwezekano wa maisha katika sayari.

Tafiti kama hizi ndizo zinazotengeneza gap kubwa sana kati ya tafiti nyingine duniani huku zikitengewa fungu la kutosha.
Itakuwa,vyama tukiendelea kupeana taarifa juu ya kinachogundulika kwa sababu utafiti huu umedumu kwa kitambo sana.
 
Attachments

  • a01_jd_02mar_planet2-630x815.jpg
    a01_jd_02mar_planet2-630x815.jpg
    82.6 KB · Views: 1
Ni hatari Kaka
Wameshaanza kugawa watu kwenye makundi type 0 to 4 depending on how people harness energy from the planet earth.
 
Wanatumia mabilioni ya dollar kufanya upuuzi huo kusema hayo mafungu ya pesa yangepelejwa kusaidia watu wasio jiweza..
Hivi binaadamu tukoje?

Anyway kila mtu anakipaumbele chake
 
Nilishawahi kuangalia hiyo documentary (Are we alone ) ilikuwa inaonyeshwa na discovery Chanel kusema kweli ni makala nzuri sna na ina mambo ya kustaajibisha na kutisha pia, ila nilipata kujua ulimwenguni kuna mambo mengi yanayoendelea ila ss hasa Africa hatujui chochote. Kikubwa kinachowaumiza kichwa hawa jamaa(wanasayansi) ni mabilioni na bilioni ya sayari zilizopo angani halafu sayari yetu tu (Earth) iwe na viumbe hai pekee.Wao wanahisi na kuamini kuna sayari fulani zina viumbe na binadamu kam ss (Alliens) na maisha yanaendelea kama hapa duniani
 
Wanatumia mabilioni ya dollar kufanya upuuzi huo kusema hayo mafungu ya pesa yangepelejwa kusaidia watu wasio jiweza..
Hivi binaadamu tukoje?

Anyway kila mtu anakipaumbele chake
Wazungu wana ubongo na wasojiweza wana ubongo. Achilia mbali pipo with various disabilities. Iweje wasojiweza waishi kwa kutegemea msaada toka kwa hao wazungu?
 
Hapo wazungu wanataka kuona mambo ya alien.....just imagine waguse sehemu ambayo sio sahihi hao alien (kama wapo) wacharuke na waje kutuadabisha patakuwa padogo mbona...
Na ndio kitakachotupata tena kama wako vizuri kitechnolojia itakula kwetu maana inawezekana wapo na wanakula good time zao sasa from now where ss tunajipendekeza kutaka kuwajua kiundani
 
Mimi siamini Kama kuna sayari zingine Hawa wana sayansi wana tudanganya tu.wanatwambia Kwamba walishawahi kufika mwezini toka mwaka 1969 lakini mpaka sasa hakuna alie enda tena huko mwezini,ukiwauliza kwanini wanakwambia gharama zake nikubwa sana kwani kutengeneza kifaa cha kwenda huko kinahitaji technology Kubwa kukitengeneza.kwahiyo Mwaka 1969 na mwaka huu 2019 upi technology ipo juu?au tuseme 1969 walikuwa wanahela sana kuliko mwaka 2019?dunia sio duara na wala haizunguki Kama wanavyo tudanganya mpaka kwenye masomo.
 
Subiri elon musk atue mars.
 
Miongoni mwa tafiti tata zinazofanywa na watafiti wa Marekani ni hii ya kutaka kujua je kuna viumbe wengine kama binadamu.

Utafiti huu kwa sasa unatumia 3D modeling huku ukihusisha kemia ya anga hewa ili kuangalia uwezekano wa maisha katika sayari.

Tafiti kama hizi ndizo zinazotengeneza gap kubwa sana kati ya tafiti nyingine duniani huku zikitengewa fungu la kutosha.
Mimi nahisi kuna viumbe wengine kwenye sayari nyingine la shida inakuja pale wanaanga na wanasayansi wanapokuwa wanatafuta viumbe hao kwa kufikiri wako kama sisi yani wanahitaji maji, oxygen kuishi.
Mimi uwa ninawaza kuwa kuna viumbe ambao mfumo wao ni tofauti kabisa na sisi, yani hawahitaji maji wala oxygen kuishi. Naona wakiwa wanascan sayari, habitable zones, ni zile zenye hali inayoelekeana na kufanana na dunia. What if hao viumbe wengine hawahitaji hali kama hiyo kusurvive?
 
Back
Top Bottom