Uchaguzi 2020 Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais?

wahid1

JF-Expert Member
Jun 26, 2014
225
279
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliyapitisha majina matatu kati ya wachukua fomu takribani saba waliogombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.

Kisha wajumbe wa Baraza Kuu walipigia kura majina hayo na jina la Tundu Antiphas Mughwai Lissu likaibuka na ushindi wa kishindo wa kura 405 kati ya 442.

Majina mengine mawili ni Lazaro Nyalandu aliyepata kura 36.

Mwanasiasa huyu kihistoria alikuwa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Alihudumu katika nyadhifa hiyo kwa mihula minne mfululizo tangu mwaka 2000, hadi alipotangaza kuondoka mwaka 2017 na kuhamia Chadema.

Waziri huyo wa zamani wa Maliasili alijiuzulu kwa kile alichoeleza; kutoridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini pamoja na ukiukwaji wa haki za binaadamu, ongezeko la vitendo vya dhulma dhidi ya baadhi ya Watanzania.

Jina la tatu ni Dkt. Mayrose Majige aliepata kura 1.

Alikuwa mwanamke pekee kati ya wanaume hao wawili. Jina lake sio maarufu katika siasa za Tanzania, na huenda sio maarufu hata ndani ya Chadema.

Lakini amekuwa ni mwanaharakati wa kuheshimika akiongoza mapambano dhidi ya ufisaidi.

Kwa hesabu hizo, Tundu Lissu anakuwa mpeperushaji wa bendera ya chama chake, pindi tu mkutano mkuu utakapo mpitisha rasmi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo na mwanasheria kitaaluma kukiwakilisha chama chake kugombea urais.

Mmoja kati ya atakaochuana nao hapo Oktoba ni hasimu wake kisiasa na Rais wa sasa Dkt John Pombe Magufuli wa CCM. Kama ni kabumbu tungesema mtanange huu hatumwi mtoto dukani.

Kipi kimempa nguvu?
Katika nyakati hizi ambazo kukosoa-kosoa kunaonekana kuhatarisha nafasi ya mtu kuendelea kubaki uraiani.

Mtu kama Lissu ambaye hajawahi kuogopa kukosoa kabla na hata baada kushambuliwa, anatazamwa kama shujaa kwa wale ambao wanatamani kufumbua midomo yao kwa kutoridhishwa na baadhi ya mambo ya utawala lakini wanaogopa.

Upinzani wake wa kusema bila kuogopa ndiyo karata iliowashawishi wajumbe kumpa kura nyingi dhidi ya wagombea wengine. Kwa Chadema huyu ndiye mgombea imara na sahihi zaidi kwa kuiangalia ramani ya siasa za sasa.

Si hivyo tu, upinzani wake kwa utawala unampa mvuto pia kwa raia ambao hawaridhishwi na namna mambo yalivyoendeshwa kwa miaka mitano. Anapata uungwaji mkono hadi kutoka kwa wafuasi wengine wa vyama vya upinzani na wanaharakati ambao hawako katika vyama.

Wapo wanaodhani kutokuwepo nchini kwa takribani miaka mitatu akiwa nje kwa matibabu kumeathiri ushawishi wake wa kisiasa. Ukweli wa mambo ni kinyume chake, kushambuliwa na kwenda ughaibuni kumezidisha ushawishi wake ndani ya Chadema na nje ya chama hicho.

Bado ana mvuto na ushawishi mkubwa ambao ni tishio kwa wagombea wengine hasa yule wa chama tawala.

Kupitishwa kwake ni salamu za wazi wazi kwa wagombea hao wanaokitaka kiti cha Urais, kwamba wasitegemee shughuli kuwa nyepesi katika kinyanganyiro hicho.

Ni jambo lisilo na uhakika ikiwa vyama vya upinzani hasa kile cha ACT Wazalendo kitashirikiana na Chadema au la. Ikitokea wakikubali kushirikiana na wakamkubali Lissu kuwa mgombea wao wa urais, nguvu na kitisho chake vitazidi maradufu.

Kabla ya kupigwa risasi alikuwa ni mkosoaji hai wa utawala wa Rais Magufuli, hivyo kupambana na mgombea huyo wa chama tawala katika sanduku la kura, kwake itakuwa ni mbinu nyengine katika muendelezo wa mapambano yake dhidi ya mtawala anayemkosoa kwa sera na utendaji wake.

Changamoto zinazomkabili
Moja ya changamoto kubwa inayomkabili ni kuirudisha imani ya wapiga kura na wafuasi wa Chadema.

Miaka mitano iliyopita wafuasi wengi wa vyama vya upinzani kikiwemo cha kwake, wamepoteza imani na vyama hivyo kwa sababu ya utitiri wa wanasiasa waliokuwa wanavihama na kwenda CCM.

Wapo Wabunge, madiwani na hata mgombea wao wa urais katika uchaguzi wa 2015 ndugu Edward Lowassa.

Katika mazingira hayo Lissu atakuwa na kazi ya ziada kuwashibisha imani wafuasi kwamba wagombea wa ngazi zote wanaopitishwa watathamini kura za wafuasi wao. Wala hawatoifanya Chadema kuwa daraja la kuelekea Bungeni kisha wakabadili muelekeo angani.

Usalama wake ni changamoto nyengine inayomkabili. Waliotekeleza mpango wa kutaka kumuua hakuna taarifa za kukamatwa kwao, tafsiri yake ni kwamba bado wako huru kama yeye alivyo huru. Hakuna ajuaye ikiwa dhamira yao ya kumuua wameibatilisha ama bado iko pale pale.

Pia lipo swali kuhusu afya ya mguu wake uliojeruhiwa kwa risasi za moto; atakuwa na nguvu ya kuvinjari katika mizunguko ya kampeni za nchi nzima? Kwa maslahi mapana ya kisiasa na mbio zake za urais atahitajika kuwathibitishia kivitendo wafuasi wake kwamba anao uwezo huo bila ya tatizo lolote.

Lissu na Chadema
Lissu aliyezaliwa Januari 1968 ni makamo mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia chama hicho kinachofuata nadharia za mrengo wa wastani wa kulia.

Chadema kipo hai tangu uchaguzi wa kwanza 1995 baada ya mfumo wa vyama vingi kurejea tena nchini. Kimekuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania bara tangu uchaguzi wa 2010. Kimeitikisa vyema CCM.

Kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Utafiti ya Twaweza ya jijini Dar es Salaam, ya mwaka 2017, inakielezea Chadema kama chama kinachowavutia zaidi vijana na wasomi.

Hiyo ikiwa ni tofauti na chama tawala ambacho ripoti ilieleza kinavutia zaidi wazee.

Swali la ikiwa Lissu atashinda uchaguzi au la, hilo halina jawabu kwa sasa.

Sio kwake tu, bali hata kwa wagombea wengine wa nafasi hiyo, hakuna mwenye jawabu kuhusu nani atashinda.

Lenye uhakika ni kuwa ushindani utakuwa mkubwa hadi pale mshindi atakapo tangazwa.

Je, Tundu Lissu ataandika historia ya kuipindua meza ya CCM na kuking'oa madarakani chama hicho kikongwe?

Ama atapita na kukiacha kama walivyopita wengine?

Hayo yote hayahitaji utabiri, ni kusubiri na kuona kile kitakachotokea katika uchaguzi wa mwaka huu.

Chanzo

Je, Tundu Lissu ana nguvu gani dhidi ya wagombea wengine wa urais? - BBC News Swahili

_113800432_lissu.jpg
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
 
Binafsi, naona hao jamaa wamefanya vizuri kumpa nafasi huyo Tundu Lissu. Wameutendea haki ule usemi wa UKITAKA KUKIKATA KICHWA CHA KOBE………
Kwa sasa KICHWA KIMETOKA NJE! Wakati wa Lissu ni huuuuu!
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
 
Wanao hamahama ni wasasiasa uchwara hununuliwa na kuuzwa kirahisi 'cheap policticians are easily bought and sold'
 
Uchambuzi mwanana, Ila ujue tu siasa sasa inaanza na TL anashida pia ya kuuhakikishia uma kwamba hajatumwa na Wazungu .. Hii ni propaganda ndogo lakini kwa aina ya mtanzania inamnyima kura.
Na hii ndio itakayompoteza mazima. Mtu akisikia tu jamaa katumwa na mabeberu basi kwisha kazi

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Wasiposhindana leo kesho hawatakuwa vichwani mwa watu hivyo kufika 2025 inaweza kuwa wamepotea so hii ni strategy sahihi zaidi
 
Na hii ndio itakayompoteza mazima. Mtu akisikia tu jamaa katumwa na mabeberu basi kwisha kazi

Senti bai yuzingi tecno T301
Si karata ya kutegemea ikubalike as long as anajua kujitetea alikuwa katika matibabu nothing more
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Kama hata 2025 itabaki ni ushindani bora washindane kuanzia sasa tu maana kama huna uhakika wa safari ya kesho safiri leo utajua huko huko mbele
 
CDM kuweni tu makini bao la mkono lisifungwe, nini uhakika ushindi ni wenu mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2015.
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Kwani kuna ubaya gani akigombea mwaka huu na iwapo akashindwa agombee tena mwaka unaoutaka mkuu??
 
..kwanza, TL ana HISTORIA ya kutetea wananchi tangu akiwa kijana mdogo, tena akiwa hana ulinzi wala cheo.

..hiyo ni tofauti na wale wanaotetea wananchi baada ya kupata ulinzi, walipokuwa hawana ulinzi walikuwa upande wa madhalimu.

..pili, TL ktk macho ya jamii ni SHUJAA. tukio la kumshambulia limemuongezea imani, huruma, na mapenzi ya wananchi.

..tatu, ni msomi na ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye kipaji cha kujenga hoja. TL akianza kuongea siyo rahisi kumchosha msikilizaji wake kwani huwa hatabiriki.

..nne, ni muelewa wa mambo mengi sana ya kisheria, kiutawala, na kiuongozi. hili ni eneo ambalo amewazidi wanasiasa wengi. kama utagundua siku hizi wanasiasa wengi wamejificha kwenye dini na maandiko ya misahafu. TL ni tofauti kabisa.

..kwa maoni yangu, upinzani haujawahi kuwa na mgombea mwenye vigezo vingi vizuri, imara, na maarufu, kama Tundu Lissu.
 
Nyalandu mzuri lakini ugeni ndio umemuharibia, na aliyofanya Lowassa ndio yaka maliza.
Chadema wakagundua chako ni chako tu.
 
Atakuwa ni 'Mshindani' mzuri kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ila ' Timing' ya ujio wake na 'Kujikita' zaidi katika Kuutaka Urais kwa manoni yangu kama GENTAMYCINE umekuja wakati mbaya. Siyo Siri japo Rais Dkt. Magufuli ana 'Changamoto' zake kadhaa za 'Kiuongozi' na hata 'Kitabia' ila katika Kuisukuma Tanzania katika 'Maendeleo' ya Kimsingi kabisa amefanya mengi, makubwa na yanayoonekana labda ni kwa 'Mpumbavu' tu pekee.

Nilisema mahala hapa hapa JamiiForums kuwa sishauri Mheshimiwa Tundu Lissu 'agombee' Urais wa Tanzania kwa mwaka huu bali 'nilipendekeza' kuwa angejengwa na kujijenga zaidi kwa mwaka 2025 ambao kwa Mimi 'Mtazamo' wangu naona kuwa ndiyo unaweza kuwa 'Anguko' kubwa la CCM ( kama nayo isipojitathmini ) kutokana na kwamba kuna 'Matabaka' makubwa, Chuki kubwa na hata Kuhasimiana Kwingi ila kwa sasa Mweyekiti Taifa ( CCM ) anajitahidi 'Kufunika' hilo 'Fukuto' kwa Mamlaka yake.

Pamoja na kwamba nimesema huenda kwa mwaka 2025 ingekuwa ni vyema na wakati sahihi kwa Mheshimiwa Tundu Lissu 'Kugombea' na angeweza kuwa na 'impact' kubwa nchini kwakuwa Rais Dkt. Magufuli ( CCM ) atakuwa anaondoka, lakini ubaya ( hasara Kwake na kwa CHADEMA ) ni kwamba hata kwa mwaka huu 2020 ambapo Lissu atakuwa 'Flag Bearer' wa CHADEMA bado CCM watafaidika na kuzidi ' Kujiimarisha' zaidi Kisiasa hasa kwa 'Changamoto' ambazo atakuwa akizitoa / akizinadi Jukwaani wakati wa Kampeni.

CHADEMA imemuharakisha sana Tundu A. Lissu 'Kugombea' kwa mwaka huu ila kwa mwaka 2025 nina uhakika angeleta 'Ushidani' ule ninaoutaka.
Pumba tupu
 
Mtazamo wako, waachie wengi wafanye mitazamo yao
 
Ninaheshimu mtazamo wako kwakuwa uko kwenye ukweli zaidi kuliko mambo ya mahaba niue. Ni kweli huenda Lisu amewahi, japo sio kuwahi sana, maana tayari ni mzoefu wa siasa zetu. Kwangu naamini kabisa iwapo kutafanyika kosa la kiufundi la kumuacha Magufuli na washindani dhaifu, ni dhahiri atapita kwa kura nyingi. Hali hiyo kwa vyovyote itamfanya yeye binafsi, au wapambe wake kutaka akae madarakani zaidi ya miaka 10.

Lakini iwapo atakutana na ushindani stahiki safari hii, atajikuta ana nafasi finyu ya kutaka kujiongezea muda, kwani anajua fika atakiongoza yeye binafsi na chama chake kwenye matatizo makubwa sana ya kukaa madarakani.

Ni kweli Magufuli kafanya vyema kwenye miundombinu, lakini kwenye maeneo mengine kama ya uchumi, ajira, rushwa, kuitawala, hasa utawala ubora, uhuru wa kujieleza na habari, ana maksi za chini sana. Hivyo namfananisha na mwanafunzi anayepata maksi A+ kwenye somo moja, lakini akiwa na F kwenye masomo mengine. Ni vyema kuwa na rais aliye na wastani mzuri kwenye masomo/maeneo yote, kuliko kuwa kiongozi aliye na nguvu kwenye sehemu moja zaidi.
 
Wakati nasoma bandiko hili, nilikuwa najipanga nami kutoa mawazo yangu, lakin baada ya kusoma chanzo chake kuwa ni BBC Swahili NEWS, nikaacha kuweka nilichokuwa nataka kuweka kwani chanzo chenyewe ni cha utata na ni wale wale wanaounga mkono USHOGA NA USAGAJI, hivyo nikaona siwezi kubishana na type hiyo kwani msimamo wao kwa nchi yetu kwa ujumla unaeleweka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom