Je, tunawezaje kunufaika na 'Kunguru wa Zanzibar'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, tunawezaje kunufaika na 'Kunguru wa Zanzibar'?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by SMU, Dec 2, 2008.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  ‘Kunguru wa Zanziba’r kwa hakika ni kero kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam. Baadhi ya kero za kunguru hao ni kuchafua nguo zilizoanikwa, kupora maandazi, vifaranga vya kuku, bata, na wengine kushambulia watu wanaopanda kwenye miti yenye viota vyao. Pia kunguru hao wameripotiwa mara kadhaa kubeba vijiko, nguo za ndani na kuchafua mazingira kwa kutoa vinyesi vingi maeneo wanayolala. Pengine hata wewe, kwa namana moja ama nyingine, umewahi kukumbana na madhila ya kunguru hawa. Swali langu hata hivyo ni je, tunawezaje kunufaika na Kunguru wa Zanzibar?

  ‘Kunguru wa Zanzibar’ ni mojawapo ya aina sita ya kunguru duniani. Kunguru huyu ana rangi nyeusi ikitapakaa sehemu kubwa ya mwili na rangi ya majivu kwenye shingo na kifuani, wana macho ya kahawia wakiwa wakubwa. Vifaranga vya kunguru vinafafana na kunguru wakubwa (i.e. ‘Kunguru wa Tanzania’ - wale wenye baka jeupe kifuani), lakini wana macho meusi na mdomo wa ndani huwa unakuwa na rangi ya pink. Kwa jina la kisayansi anajulikana kama “corvus splendens”. Kunguru ni huyu wa Zanzibar ndiye kunguru mdogo kuliko wengine katika jamii yao.

  Kunguru hawa kwa mara ya kwanza walipelekwa katika visiwa vya Zanzibar kutoka katika mji wa Bombay na serikali ya India mwaka 1891 mara baada ya kuombwa na Sir Gerald Herbert Portal. Waliletwa kunguru 50 Kwa ajili ya kudhibiti uchafu na takataka zinazoweza kuliwa na ndege hawa katika sehemu ijulikanayo kama “Stone Town.” Ulipofika mwaka 1917 uzalianaji wa kunguru uliongezeka sana na kufanya waonekane kama ndege waharibifu sehemu ya stone town.

  Kwa mara ya kwanza, kunguru wanaokera jijini Dar es Salaam waliletwa wachache kutoka Zanzibar kwa lengo la kula mizoga. Kutokana na jinsi kunguru wanavyozaliana kwa wingi na upatikanaji wa chakula chao kwa urahisi, ndivyo polepole wanavyozidi kutapakaa sehemu tofauti za nchi ya Tanzania, ikiwemo Morogoro, Pwani, Tanga na kwingineko utaona kunguru mmoja, lakini baada ya miaka michache watakuwa wengi pia. Na inasadikika kuwa kutokana na kunguru kuweza kuishi kwenye hali ya hewa tofauti tofauti, basi katika miaka ijayo mikoa yote ya Tanzania watapatikana iwapo hawatadhibitiwa.

  Kunguru siyo tu wanadhibiti takataka zinazooza tu, bali pia wanakula wanyama wadogowadogo (kama panya), mazao ya mbegu, matunda na mazao mengine. Lakini pia kunguru wanashindana na aina nyingi za viumbe tofauti kwa chakula. Na katika sehemu za viota vya ndege moja kwa moja wanakula vifaranga na mayai kutoka kwa ndege wengine. Huu ni ukweli kuwa sehemu ambayo wanapatikana kunguru, ndege wametengeneza viota sehemu ambayo kunguru hatofikia, na siyo rahisi kukuta ndege amejenga kiota kwenye mti, tofauti na sehemu ambayo hakuna kunguru utakuta ndege wamejenga kiota kwenye miti na sehemu nyingine ya wazi kabisa. Idadi kubwa ya kunguru wenye rangi nyeusi na nyeupe ambao wamekuwepo hapa jijini wamekimbilia katika mikoa mbalimbali, hivyo kuwaacha kunguru weusi hapa jijini Dar es Salaam.

  Miaka ya hivi karibu serikali kupitia Kitengo Cha Wanyamapori (Wizara ya Maliasili na Utalii) imekuwa ikifanya jitihada za kuwaondoa kunguru hawa jijini Dar es Salam kwa kutumia sumu. Hata hivyo, kwa maoni yangu, jitihada hizi hazijafanikiwa kwani ndege hawa wanaendelea kuongezeka na kusambaa nchini Tanzania. Sijui ni kwanini kampeni haikuelekezwa kwenye kuangamiza viota na mayai yao.

  Nadhani kuna haja ya kufikiria namna bora zaidi ya kuwatokomeza au ‘kuwatumia’. Kwa mfano kutumia ‘mitego’ ambayo inaweza kunasa kunguru wengi kwa mara moja (hapa nafikiria ‘Kuvuna Kunguru’!) na hivyo kutumia ‘minofu’ yao kama chakula cha wanyama (au binadamu - wapo watakaotaka kuonja!). Je wewe unasemaje? Tufanye nini?
   
Loading...