Je tunaweza kutenganisha polisi na siasa?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,747
Kwa namna ambavyo wanasiasa hasa wa upinzani wanavyojenga taswira kwamba Jeshi Letu la Polisi ambalo limeundwa kwa sheria ya Bunge kwamba ni wanyanyasaji na wavunjaji haki za binadamu ni kama vile kuwa wakishapata madaraka watalivunja jeshi la polisi na kuja na kitu kingine.

Sasa ni muda muafaka wa kuangazia maslahi ya kisiasa V/s misingi ya utawala bora.

1. Kutenganisha siasa na Polisi

Tunawezaje kutenganisha siasa na jeshi la polisi? Kuna mapungufu gani katika sheria iliyounda Jeshi la Polisi ambayo yanapaswa kurekebishwa ama kuboreshwa?

Katika sheria ya maadili ya viongozi wa Umma, inawezekana kuwepo masharti ya kisheria yanayowsbana viongozi wa umma kutotumia jeshi la polisi kwa manufaa yao nje ya utaratibu wa kisheria?

2. Haki za binadamu

Jeshi la polisi kuboresha utendaji wake hasa kutovunja haki za binadamu wala katiba ya nchi. Hapa tunaona umuhimu wa kuijenga Tanzania na jeshi linaloheshimu utu na haki za raia.

Kesi wanazozichubguza ziwe na mashiko na siyo za kubambika ama mashinikizo.

3. Kuboresha sheria ya utawala bora

Sheria ya usalama wa Taifa ilibadilishwa ambapo waliondolewa kwenye operesheni wakawa wakusanya na wachakataji taarifa ambapo watekelezaji au wakamataji ni polisi.

Kinachotakiwa ni kuboresha sheria hiyo na kuruhusu Usalama wa Taifa kushughulikia threats ambazo zipo kwenye level ya kuhatarisha usalama wa Taifa na waweze kuchukua hatua badala ya kusubiri polisi ndo wachukue hatua.

Pia sheria hii iwabane wanausalama kutovuka mipaka yao na kuonea watu. Ofcourse tunajua kwamba wapo makini sana ni mara chache saana wanaenda nje ya lengo

4. Waziri wa Polisi.

Itungwe sheria ya kuunda permanent Home Affrairs Ministry. Ambapo waziri wake asiwe Mbunge bali mmoja wa majenerali waliopo kazini au wastaafu ili masuala yote ya usalama wa ndani ya nchi yaendeshwe kitaalam.

Hii itaepusha bias kwenye matumizi ya jeshi la polisi. Jeshi letu na mengine yatakuwa bora na yenye kuwajibika kwa katiba na sheria za nchi yetu sasa na vizazi vijavyo.

Tulisaidie Jeshi letu la Polisi litimize wajibu wake bila kuvuka mipaka ya utu na haki za raia.

Je hili linawezekana?

Kivipi?

Wewe una maoni gani?

Msanii JF

IMG-20191223-WA0073~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom