RRONDO
Platinum Member
- Jan 3, 2010
- 59,419
- 135,060
Nakumbuka nikiwa darasa la kwanza tulikuwa tukipewa madaftari mapya pindi la zamani likijaa
Nakumbuka tulikuwa tukipewa uji wa buluga saa nne
Nakumbuka nilikuwa nikipanda UDA saa 1 kamili bila bughudha kama ya daladala
Nakumbuka nilikuwa nikipenda kusubiri basi la IKARUS
Nakumbuka nikiwa sekondari(day) tulikuwa tukipewa chai na mikate na baadae lunch ya wali na nyama/maharage na matunda
Nakumbuka mtaani kwetu na mitaa jirani kulikuwa na taa za barabarani na lami kila mtaa
Nakumbuka magari maalum ya taka yalikuwa yakipita kukusanya takataka kila baada ya siku kadhaa
Nakumbuka nilikuwa nikiamka asubuhi kuwahi mikate ya SIHA na maziwa kibandani
Nakumbuka sikuwahi kusikia maji au umeme ukikatika
Nakumbuka tulikuwa tukicheza mpira na kubembea garden
Leo hii
watoto wanashinda njaa asubuhi hadi jioni
watoto wananyanyaswa na makondakta wa daladala
usipokula ukashiba huwezi kupanda daladala
mitaa mingi haina taa wala dalili ya lami
madimbwi ya maji mtaa mzima wakati mabomba yameota kutu
takataka zinatupwa kila kona
maji na umeme kukatika ni sehemu ya maisha
mitaa yetu haina hata sehemu za watoto kucheza kila kona baa/garage bubu
Hivi tunasonga mbele au Tunarudi mwaka 47??