Je, tunajenga Taifa la aina gani?

Je, tunajenga Taifa la aina gani?

Mimi naogopa sana na mtu yeyote mwenye akili aje hapa anisaidie kutafakari. Sisi sote tunaongozwa kwa misingi ya katiba na sheria na hakuna kiumbe yupo juu ya sheria.

************
Ni hivi Mkuu yapo machache yakufikiria, kuwaza na kuwazua kujua kinachoendelea

Labda tujiulize machache dhidi ya katiba ile ambayo wengi mmelua mkishadadia kwamba tulikua tunaendeshwa kwa misingi ya SHERIA na katiba;

1. Sheria ilikua wapi mkuu tulipokua tunatoa magogo Tanga kuyapeleka Mombasa kisha kuyarudisha tena Tanzania ili yaonekane ni imported?

2. Sheria ilikua wapi wale Twiga walipokua wanapanda ndege kwenda ughaibuni?

3. Katiba ilikua wapi bandari ilipogeuka chumo la wezi na walarushwa?

4. Sheria ilikua wapi Mafuta yalipokua yanatolewa Bandarini kwa kibali cha transit yakapelekwa hadi Mbeya kisha yakarudishwa Chalinze kumwagwa kwenye petrol station?

5. Katiba ilikua wapi kuwamulika waliozifanya ofisi za Serikali kama vibanda vyao binafsi vya kujitajirisha?

ANGALIZO
Naomba usiniletee stori za Serikali ilikua ni ya CCM.

Sasa basi kinachofanyika ni kile wazungu wanachosema THE END JUSTFIES THE MEANS kwa ukiritimba na umangimeza wa Sheria tulizonazo Rais Magufuli asingeweza kufanya hata 1/10 ya alichokifanya Kama angehitaji kufuata mlolongo wa sheria.

Mfano mdogo tu PPRA Act inasema hakuna manunuzi yoyote kufanyika bila kupitishwa na Bunge moja lakini mbili lazima kuwe na Proforma invoice tatu za kuonyesha ushindani na the lowest bider ndiye atakayepewa tenda.

Unadhani ingeichukua Serikali muda gani kupitisha?

1. Ununuaji wa Ndege
2. Ujenzi wa SGR
3. Ujenzi wa Bwawa la Umeme mto Rufiji
4. Ujenzi wa vituo vya afra na hospitali za Wilaya na mikoa pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi?
5. Unadhani ingehitaji malumbano kiasi gani kupitisha ujenzi wa Daraja la mfugale, Ubungo, salenda, kivuko cha Mwanza, ujenzi wa meli nk?

Kama sheria ilikuwepo na haikusaidia kupambana na uhalifu vipi Kama Sheria haitatumika kuzuia maendeleo ya nchi hiyo hiyo?

Tatizo ninaloliona Mimi ni kwamba uwepo wa Sheria nzuri si kinacholeta maendeleo bali uwepo wa kiongozi imara ndio kunakoleta maendeleo.

NADONDOSHA MIC
Tunahitaji kubadili mfumo wetu wa kujiendesha...tuwe na Sheria nzuri na Bora kuanzia hapo mwelekeo wetu kama taifa utakuwa ktk njia sahihi.

Hizi Sheria za kujiwekea makongwa si nzuri kwa ustawi wa taifa letu maana unatoa upenyo kwa kiongozi kufanya jambo lolote.

Kiongozi mzuri na imara ni yule anaye tokea ktk mfumo sahihi.
 
Unaonaje akitokea mwingine anayeweza kusimamia hayo kisha akaenda kumtoa madarakani hata leo ili yeye afanye vizuri zaidi yake? Maana hata nafasi aliyonayo kaipata kisheria, vinginevyo itumike njia ya shortcut kumtoa madarakani. Wakoloni tuliwatoa madarakani, sio kwakuwa hawakujenga reli, viwanja vya ndege, bandari au la, lakini hawakuwa watu sahihi. Msitake kuhalalisha uvunjwaji wa sheria kisa kuna miradi kadhaa. Lengo la haya maelezo yako ni kukingia hii nia ovu ya kutaka kupitisha sheria ya kukinga watenda maovu kwa kichaka cha miradi kadhaa.
Tatizo lako hujibu hoja unahemkwa tu, kwakua maslahi yako na au wadau wako yameguswa.

Ingekua vyema kama ungejibu hoja na kuweka Manung'uniko pembeni!
 
Tunahitaji kubadili mfumo wetu wa kujiendesha...tuwe na Sheria nzuri na Bora kuanzia hapo mwelekeo wetu kama taifa utakuwa ktk njia sahihi.

Hizi Sheria za kujiwekea makongwa si nzuri kwa ustawi wa taifa letu maana unatoa upenyo kwa kiongozi kufanya jambo lolote.

Kiongozi mzuri na imara ni yule anaye tokea ktk mfumo sahihi.
Ungejibu hoja Sheria ya uhujumu uchumi ilikuwepo mbona tulikua tunatoa magogo tanga na kuyapeleka Mombasa kisha kuyaleta dar es salaam kuyauza kwa bei ya importation?

Tatizo sio kuwepo kwa Sheria tatizo lipo kwenye usimamizi wa Sheria.

Kama tuliweza kufumba macho alipobakwa unaonaje tukifunba macho leo akiolewa?
 
Hata majumbani kwetu tuna taratibu. Tunaswali kwanza kabla ya kula. Tunanawa kwanza kabla ya kula, n.k. Huwezi kuruka taratibu kwa kisingizio cha kuharakisha mambo.
Mnanikera kwakua mnajifanya ku reply comment yangu wakati mnaandika malalamiko badala ya kujibu hoja
 
Tafsiri take kwamba kuna viongozi wanavunja sheria huku wakifahamu fiks ndio wanatafuta Kings kwa makosa wsliyokwisha fanya na wanayotarajia kuyafanya.
 
Back
Top Bottom