Je, tukianza mchakato wa Katiba mpya utapenda wajumbe wa Tume ya Katiba mpya na wale wa BMK wabaki walewale au tupate wapya?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,957
141,946
Karibu kwa majibu tafadhali hapo tupo kitaifa zaidi so itikadi za vyama tuziweke pembeni.

Je warudi wote au wengine wabadilishwe?........kwanini?!

Maendeleo hayana vyama!
 
Karibu kwa majibu tafadhali hapo tupo kitaifa zaidi so itikadi za vyama tuziweke pembeni.

Je warudi wote au wengine wabadilishwe?........kwanini?!

Maendeleo hayana vyama!
Kwanza lazima kuwepo na sheria itakataza mtu yeyote atayeshiriki katika huo mchakato kutogombea cheo chochote kwa muda wa miaka 20. Mchakato huo uanze baada ya 2020 na utumike 2025. Hapo tutapata katiba ya maana
 
Kwani kuna mjumbe wa Tume ya Warioba aliyegombea uchaguzi wa kisiasa?!
 
Lisitumike bunge la kawaida tena. Badala yake wawakilishi wa vyama, taasisi, NGO makundi maalumu. Waangaliwe watu huru na mawakili binafsi na kura ziwe za siri.
 
Hivi mchakato huu ndo uliotuletea...
1. Polepole
2. Kalamagamba
Sijui tumemkosea nini Mungu
 
Pia wajumbe wa bunge maalumu la katiba nao wawe wapya - hapa nasemea wale wa kuteuliwa.....Kwa wabunge na amini wengi waliokuwepo kipindi kile hawatakuwepo tena 'watakua wameshapoteza nafasi zao na wengine kustaafu siasa'
 
Back
Top Bottom