econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,751
- 21,740
Waziri wa katiba na sheria ameshatangaza rasmi kwamba mchakato wa katiba mpya utaanza mwezi wa Saba mwanzoni. Nilikuwa na ushauri kwamba makosa yaliyopelekea mchakato wa katiba mpya mwaka 2014 kukwama yasijirudie.
Nimeanisha makosa Kama yafuatayo:
1. Tume ya katiba ndio ipewe mamlaka ya kisheria ya kuandika rasimu ya katiba itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge la Katiba. Tusirudie kosa la kuliachia bunge la Katiba kuandika rasimu yake na kuitupa kapuni ile ya Tume ya Katiba.
2. Kabla ya kuanza mchakato wa katiba mpya, ningeshauri tuanze na kura ya maoni ili wananchi waamue ni mfumo gani wa muungano wanaoutaka. Je wanataka mfumo wa Unitary, Federal au confederation. Wananchi wengi wakikubali mfumo mmojawapo, basi rasimu ya Tume ya Katiba itengenezwe kwa kufuata muundo ulioamuriwa Kwenye kura ya maoni.
3. Rais asioneshe upande wake Kwenye rasimu ya katiba. Ili kosa alilifanya Mh Rais Mstaafu Kikwete. Aliposimama Kwenye bunge la Katiba na kuonesha kwamba yeye anataka katiba ya aina gani, hivyo kupelekea wajumbe wa chama chake kufuata maelekezo yake. Mwisho wa siku katiba mpya haikupatikana. Rais ajitenge kuwapelekesha wanachama wa chama chake wafuate maoni yake baadala yake awaachie Uhuru wa kujadili.
4. Tuangalie mahitaji ya Sasa na sio misismamo ya chama. Tunapoenda kuandika katiba mpya tushughulike zaidi ya matatizo yanayotukumba Leo na namna ya kuyaondoa na sio kuangalia vyama vinataka Nini. Ufisadi, maadili, Uhuru katika uchaguzi, mfumo wa kiuchumi, mamlaka ya bunge, haki jinai, sera ya kimataifa, vyombo vya ulinzi, Uhuru wa mahakama, mamlaka ya Rais, ajira, mfuko wa mapato ya gesi na mafuta, mikopo ya wanafunzi iwe Ruzuku sio mkopo, vyama vya siasa, Tume huru, shirika la Taifa la habari etc.
5. Spika au Mwenyekiti wa bunge la Katiba asitokane na chama Cha siasa. Ateuliwe jaji wa mahakama ya Rufaa ambaye atasimamia bila upendeleo bunge la katiba. Tukiweka watu wa vyama sampuli ya Tulia Akson tutapata bunge la hovyo na litakalo toa rasimu ya hovyo na ya kichama.
NB:Tukirudia makosa hatutapata katiba mpya kamwe, na Kama hatupo tayari kuandika katiba mpya ni Bora kuacha kuliko kufanya maigizo.