Give me a break.Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchngu, watu kibao wamechafuliwa kule. Ila siku itakapokuwa zamu yako ama ya ndugu wako wa karibu ndio utajua kuwa ile web haifai.
Picha zimetumwa kwenye e-,ail tangu jana na watu walioona tumezikuta asubuhi kwenye email address zetu
nimeiona hiyo picha ni mbaya na ni chafu,hajamdhalilisha mh.Rais tu bali watanzania wote walio wastaarabu na wanaojiheshimu,NAMLAANI huyo aliyetengeneza hiyo picha,imeniumiza na imeniogopesha ,amewezaje kuthubutu kufanya jambo la aina hiyo,Watanzania wenzangu tunaenda wapi?hii new technology mbona tunamisuse namna hii?huu uhuru na mani tuliyonayo mbona tunaipaka matope tena kwa bila huruma wala haya tena bila kumuogopa Mungu,jamani hata vitabu vya Mungu imeandikwa HESHIMUNI MAMLAKA MLIYOPEWA NA MUNGU,kweli leo hii imefikia kutengeneza picha ya kumchafua Rais wa nchi ,???????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Wewe uliyetengeneza picha hiyo JK amekukosea nini kikubwa hata ufikie hatu uliyofikia?imagine ingekuwa wewe ungejisikiaje?Tanzania nchi inayosifika kote ulimwenguni kwa amani na utulivu,eti watanzania ni wakarimu na wana upendo,kweli????????????????nimeumia roho kupita kiasi,huu uhuru tulionao sasa tunautumia vibaya.Huyu aliyetoa picha hiyo ALAANIWE YEYE NA KIZAZI CHAKE!!!!!!!!!NA UKOO WAKE WOTE NA WALA ASIPATE BARAKA ZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKE YOTE!!!!!!!!!!
Give me a break.
We are talking about THE PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA for christ sake.
Huyu si mtu tu ,hata kama anamapungufu.
RAIS NI TAASISI.
UKIMTUKANA RAIS,UMELITUKANA TAIFA.
Huyu si kama Insia,Mengi au wengineo unawajua wewe.
TUNALAANI.
Sikiliza Mwanakijijinimeshasema hili na kuandika kwenye Cheche na hata Tanzania daima; huwezi kuwa na standards tofauti ndio maana watu wanapush the envelope. Ile habari ya kusagana iliyoandikwa kwenye Ijumaa endapo ingekuwa na kichwa cha habari "Waziri x afumwa Geto akisagana au Akiliwa uroda" na ikawa describe vile nadhani serikali ingechukua hatua.
Kuna mtu haelewi maana ya uhuru wa maoni.
Acha ukute huyo aliyeweka ni ndugu yako na wewe utalaaniwa.kama kulaaaniwa Alaaniwe yeye aliyeweka na wala sio mtu mwingine.Kweli utandawazi unatupeleka pabaya.SIJUI JK ATAKUWA AMESHAIONA AU ATAKUWA AMEAMBIWA.ILA UTASHANGAA NAE NI MPENZI MKUBWA WA HIYO BLOG,watu wanaichukia wakishatolewa huko.
Where is your patriotism my brother.Please! Kwa watu wengine wanauchafuliwa sio binadamu? Hawana familia? hawana baba na mama? Kushabikia ujinga ndo matokeo yake haya! Eti chombo cha kurekebisha tabia! Aya sasa!
asante mkulu.imekuwaje ze utamu akakutumia email? Kama si ze utamu aliyetuma basi kuna tatizo pia kwa wale wanaotoa picha kwenye globu ya ze utamu na kuanza kuzisambaza. Mwambie huyo aliyekutumia picha hiyo/hizo kwamba si halali kufanya hivyo na pia ni kinyume na maadili ya kitanzania!
Avatar yako inajieleza wewe ni mtu wa namna gani.All ya grow up, mbona masela kibao tu wanatolewa kule tokea kajamba nani mpaka mawaziri wa serikali, so itakuwa president? Ile ni site ya kikubwa anayeona inamzingua aache kuitembelea.
Ni mtazamo tu.
heshima mbele!tusiige utamaduni ambao hatukuwa nao hapo mwanzo.Inasikitisha kuona hii blog ya ze utamu inaendeleza libeneke la kuchafua watu sasa mpaka wamefikia hatua ya kumchafua Rais wa nchi!!!!!najiuliza maswali mengi ni kwamba hakuna wa kuzuia hili ?hakuna sheria yoyote ya nchi inayokataza uchafuzi unaofanywa na media!!!???Nampa pole mh.Rais pamoja na familia yake,lakini ni wakati muafaka sasa serikali kufatilia hili jambo na kufika muafaka!!
Nimekosa la kuandika.Ni kweli nami nimeona hii picha si nzuri kwa raisi wa nchi kama binadamu mwingine. Watu wengi wamewekwa mle bila wao kujua lakini hakuna lililosemwa! SASA AMEWEKWA MKULU WATU WANAPIGA KELELE. Lazima kuwa na maadili kwa watu wote situ eti kwakuwa huyu ni kiongozi na huyu ni mtu wa kawaida.
kisale,unasema JK ni mpenzi mkubwa wa hiyo blog,mimi naona weye mwenzetu si bure umekunywa maji ya choo