Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Katika ulimwengu wa taaluma, ulinzi wa tasnifu (thesis defense) ni tukio la heshima na ukomo wa safari ya mwanafunzi wa shahada ya Uzamili au Uzamivu, Master's pamoja na PhD.
Ni hapa ndipo mwanafunzi huwasilisha matokeo ya utafiti wake mbele ya jopo la wasomi na kujibu maswali ya kina, ili kuthibitisha ubora na ubunifu wa kazi yake. Kwa kawaida, ni hatua ya mwisho kabla ya kupewa shahada kubwa inayobeba heshima ya juu kitaaluma.
Hata hivyo, mijadala ya hivi karibuni nchini Tanzania imeibua swali la iwapo ulinzi wa tasnifu unapaswa kuwa tukio la wazi kwa jamii nzima au kubaki kama jambo la ndani ya chumba cha wasomi pekee.
Vyuo vikuu kama Kilimanjaro Christian Medical University College (KCMC), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Mzumbe, na Chuo Kikuu cha Mwenge vimeanza kuandaa mikutano ya wazi, mara nyingine hata kutoa matangazo ya umma kuhusu ni nani ameweza kutetea tasnifu yake kwa mafanikio.
Katika vyuo hivi, si jambo la ajabu kuona matangazo kwenye tovuti au mitandao ya kijamii ya chuo yakialika wananchi kushuhudia ulinzi wa tasnifu huku wakiweka na links za watu kuingia mubashara kwebye tukio lote.
Wadau wa sekta ya elimu, wanafunzi wa ngazi za chini, na hata waandishi wa habari hupewa fursa ya kushiriki. Hali hii si tu kwamba huongeza uelewa wa jamii kuhusu tafiti zinazofanyika, bali pia huimarisha uwajibikaji wa kitaaluma.
Kwa mfano, SUA imekuwa ikitangaza hadharani tarehe, muda na ukumbi wa kila ulinzi wa tasnifu, na baada ya tukio, hujulisha umma iwapo mwanafunzi husika amefaulu. Hii imejenga imani kwamba shahada hizo si tu makaratasi, bali ni matokeo ya mchakato thabiti na wa kitaalamu.
Kinyume chake, vyuo vikuu vikubwa zaidi nchini kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) havijaweka utaratibu wa namna hiyo. Ulinzi wa tasnifu mara nyingi hufanyika ndani ya kumbi za mihadhara bila ushirikishwaji wa jamii. Mara chache sana kuna taarifa za umma kuhusu nani ametetea, nani amefeli au kufaulu.
Hali hii imewafanya baadhi ya Watanzania kuhoji: Je, shahada hizi kubwa zinatolewa kwa uwazi wa kutosha? Je, kuna uwezekano wa nepotism michongo ama mambo ya upendeleo, undugu au urafiki—kuingia katika mchakato wa kutoa shahada hizo?
Wachambuzi wa elimu wanasema kuwa, wakati vyuo vikuu vingine vinajitahidi kuondoa dhana ya usiri kwa kufungua milango ya matukio haya, kutokufanya hivyo kwa vyuo vikuu vikubwa huacha pengo la imani.
“Ukiwaalika wananchi, unawapa nafasi ya kushuhudia kwamba utafiti uliotetea ni wa kweli, umefanyiwa kazi kitaalamu, na unastahili shahada husika.”
Kwa upande wa jamii, uwazi huleta heshima. Wazazi na wanafunzi wa shahada za chini huona mifano ya kuigwa, wakati wadau wa sekta fulani wanaweza kutumia tafiti hizo katika maendeleo ya kitaifa.
Kwa mtazamo wa kitaaluma wa kimataifa, ulinzi wa tasnifu mara nyingi huwa wa hadharani. Nchi kama Ujerumani, Marekani na hata baadhi ya mataifa jirani kama Kenya, zimeweka utaratibu wa wazi ambapo yeyote anaweza kushuhudia bila vizuizi vikubwa. Hii husaidia kudumisha hadhi ya shahada hizo na kuondoa shaka za upendeleo.
Kwa Tanzania, inaweza kusemwa kuwa vyuo vinavyoendesha mikutano ya wazi vinatengeneza dira mpya ya uwajibikaji na heshima ya taaluma. Hata hivyo, vyuo vikubwa kama UDSM na UDOM vinabaki kuwa na mzigo mkubwa zaidi wa kutetea hadhi yao mbele ya umma, kwa sababu ndiko chimbuko la wasomi wengi maarufu nchini.
Swali kubwa ni hili: Je, shahada za Uzamili na Uzamivu ni jambo la mtu binafsi pekee au ni mali ya jamii nzima? Kwa kuwa tafiti nyingi hufadhiliwa na fedha za walipa kodi na hutazamiwa kuchangia katika maendeleo ya taifa, jamii ina haki ya kushuhudia mchakato mzima wa kuzaliwa kwake.
Kama vyuo vikubwa vitabaki nyuma katika uwazi huu, basi shaka na dhana za upendeleo zitaendelea kuenea. Lakini iwapo vitajiunga na wenzao katika uwazi, basi heshima ya shahada za Tanzania itaimarika kitaifa na kimataifa.