Je Teknolojia inatumika Tanzania?

Travis Walker

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
323
334
blob.jpg

Habari ya hapo ulipo,natumai umzima wa afya.​
Teknolojia ni tawi moja katika matawi ya sayansi linalohusiana na elimu ya ufundi kwa maana ya kuvumbua kitu kipya ili kurahisisha maisha ya wanadamu kuwa rahisi mno.Nathubutu kusema Tanzania vipo vipaji au kuna watu waliosoma kuhusu Teknolojia lakini mbona hatuoni uvumbuzi wowote hapa nchini?
MASUALI
1.Kwa nini sisi kiwango chetu cha Teknolojia hakionekani?
2.Kwa nini serikali haina msaada wowote na hili, wana hisi nini hasa?
3.Jee,serikali inahisi elimu ya Teknolojia ni ugaidi?
4.Jee kama serikali itawahamasisha watu kama hawa kukamilisha ndoto zao ajira itapanda au itapungua?
4.a Jee ajira itapopanda serika hatofaidika?
5.Unahisi umaskini unasababishwa na nani hapa nchini?

6.Kwanini sisi tusiweze kwani wazungu ni nani na sisi ni nani?

Wana Wa JF naomba majibu yenu katika kuchangia uzi huu ili kukuza technolojia Tanzania

tunao vijana wazuri sana kwenye hii nchi...kinachotokea ni ufuatiliaji...wenzetu wakikuona unajua kitu au umevumbua kitu wanakuchukua na kukiendeleza kipaji chako...hapa kwetu ni kukamatwa na kufungwa ndio maana watu wamekua waoga kujitokeza hadhari na kuishia kunakili walichofanya hao uliowataja hapo juu
 
Nakusupport
 
Ufuatiliaji hakuna, na pia support kutoka serikalin hakuna. Vijana wenye vipaj wapo.. lakin wanapoibuka kuna watu wanazima ndoto zao kwa kuwawekea vikwazo
 
Ufuatiliaji hakuna, na pia support kutoka serikalin hakuna. Vijana wenye vipaj wapo.. lakin wanapoibuka kuna watu wanazima ndoto zao kwa kuwawekea vikwazo
Jee ww unahisi ni njia ziweze kutumika ili kuhakikisha vipaji vya vijana hawa ndoto zao zinafika kwenye ukweli
 
Jee ww unahisi ni njia ziweze kutumika ili kuhakikisha vipaji vya vijana hawa ndoto zao zinafika kwenye ukweli
Kwanza serikali itoe support kwa vijana hawa... ikiwemo kifedha... kiushauri.
Na pia kuwe na kama mashindano ya kuvumbua technology mpya hii itachochea vijana wengi wenye vipaj vya uvumbuz kujitokeza.
 
pkwanza kusiwe na mambo ya vitisho...tuviwezeshe vipaji vinavyopatikana...km wanavyofanya kwenye mpira wa miguu kwa sasa...mfano makongo wanavyofanya kutafuta vipaji..sasa isiwe michezoni tu...tuna vijana wabunifu sn...tena mno...DIT kule ...veta wapo na hata mavyuoni...kwa sasa wanvyofanya vyuoni ni ku..retain wale wazuri na kua walimu..
.bila kua na uzoefu wa aina yoyote practically....nilizungumza na mwanafunzu mmoja toka japan anasema ili uwe mwalimu hasa wa sayansi lazima upitie industrial areas for practical for at least two years minimum...sas hapa kwenu wanaenda practical wk 4 halafu hizo wk zenyewe wanaenda cheza karata kwenye computer...hatari sn hii kwa nchi yetu
 
Ungeanza intro bro xo kila MTU anaijua io tech kama Mimi nlivoona picha ndo mmehisi kitu lakini cjajua inahusu mini so kama vipi tubangie ka intro kidogo
 
Hebu nifafanulie zaidi kwa kauli yako hii
Mathalani unapokuwa na simu ya landline na ukasema uzalishe zingine 50 za aina hiyo. Hiyo si teknolojia. Ni kukopi. Ni utandawazi. Umechukua hapa ukaweka pale kwa kuwa uliona na ukaona utaalamu uliotumika kutengeneza. Ila unapoona kandline kusha ukatengeneza mobile phone hiyo ni teknolojia. Umeboresha kilichopo na kufanya kiwe tofauti na awali. Sasa uniambie, tuna teknolojia gani?
 
Katika teknolojia hapa nchi naona kama haina nafasi ya kuendelezwa naweza sema wakati mwingine ni uadui.

Alitokea mtu mmoja sehemu akaunda redio yake kwenye eneo lake lakini TCRA walipokuja kumtia mbaroni kama vile gaidi.

Watu kama hao ndio wanatakiwa waeleze ujuzi wao ili kuwapa wengine mwanga na kuwapa moyo watafiti ambao wanakesha kubuni kitu ambacho si cha kawaida ( hata wenzetu walianza hivyo) wasingetuthubutu basi nadhani hadi sasa tungekuwa tunatumia barua
 
Kwenye miaka ya 1998-99 kuna dogo alikua at a hajui kusoma lkn aliunda mtambo wa redio na alikuwa na uwezo was kuzia matangazo ya radio station zingine . Nakumbuka Makuburi yote ubungo na sehem za tabata Dogo alizima mitambo ya redio zingine , ukiwasha redio hupat kitu ni hip redio take. Cjui aliishia wap
 
Kwenye miaka ya 1998-99 kuna dogo alikua ata hajui kusoma lkn aliunda mtambo wa redio na alikuwa na uwezo wa kuzuia matangazo ya radio station zingine . Nakumbuka Makuburi yote ubungo na sehem za tabata Dogo alizima mitambo ya redio zingine kama siku NNE ivi
, ukiwasha redio hupat kitu ni hio redio yake. Cjui aliishia wap
 
[HASHTAG]#Trump[/HASHTAG]: Nchi yetu ni mfano wa ndege bora kabisa ulimwenguni ya Air Force one. Nitahakikisha tunaendelea kuwa taifa kubwa linalokua kwa kasi kiuchumi na kijeshi kama Air Force one.

#Shinzō_Abe: Taifa letu linakua kwa kasi katika teknolojia kama treni ya umeme. Dunia sasa inajifunza teknolojia kwetu. Japan itaendelea kuwa na kasi katika teknolojia mfano wa treni ya umeme.

[HASHTAG]#JPM[/HASHTAG]: Nchi hii ni kama Lori. Na kawaida dereva wa lori hasikilizagi kelele za abiria. Mimi nakanyaga tu ili mradi lori lifike.!
 
Mathalani unapokuwa na simu ya landline na ukasema uzalishe zingine 50 za aina hiyo. Hiyo si teknolojia. Ni kukopi. Ni utandawazi. Umechukua hapa ukaweka pale kwa kuwa uliona na ukaona utaalamu uliotumika kutengeneza. Ila unapoona kandline kusha ukatengeneza mobile phone hiyo ni teknolojia. Umeboresha kilichopo na kufanya kiwe tofauti na awali. Sasa uniambie, tuna teknolojia gani?
Ni kweli bro, ila mimi nahisi hata ugumu wa maisha unachangia kutowaza na kufikiri vizuri.Mawazo yetu yanakuwa ni dumanza sana.
 
Katika teknolojia hapa nchi naona kama haina nafasi ya kuendelezwa naweza sema wakati mwingine ni uadui.

Alitokea mtu mmoja sehemu akaunda redio yake kwenye eneo lake lakini TCRA walipokuja kumtia mbaroni kama vile gaidi.

Watu kama hao ndio wanatakiwa waeleze ujuzi wao ili kuwapa wengine mwanga na kuwapa moyo watafiti ambao wanakesha kubuni kitu ambacho si cha kawaida ( hata wenzetu walianza hivyo) wasingetuthubutu basi nadhani hadi sasa tungekuwa tunatumia barua
Hakika uko sahihi Raphel, Ila mimi nahisi viongozi wetu wa Tanzania hawajui umuhimu wa sayansi katika biashara.
 
Back
Top Bottom