Je, Tanzania zipo Boards za Architecture?

Architecture ni kozi nzuri sana. I am not one but I know one when I see one. Nikiangalia kazi kama za Zaha Hadid (RIP), Renzo Piano nk..unaona ubunifu uliotukuka.

Again, ninachokiona Tanzania ni ngumu kuwa na wataalam ambao they can think outside the box. Mfano Nenda Ardhi University. Ni vigumu sana mtu kuku-convince kwamba hapa ndo wanazalisha wasanifu majengo wa taifa letu. Kwa sababu majengo yenyewe yamechooooka kuliko maelezo. Sasa unajiuliza mwanafunzi anayesomea humo, anaweza kweli kuwa architect mzuri? Ok, as always, wahusika watasingizia kwamba bajeti haitoshi..serikali haipeleki hela na bla blah kibao..lakini hata lile jingo jipya la administration lililojengwa hizi karibuni mbona halina any creativity in it?

Kuna watu nawajua wamesoma pale they are good. Lakini Kiukweli...kwa mazingira ya vijana wanayosomea ni ngumu sana hawa watu uwape kazi utegemee matokeo chanya. exposure is zero!

Kifupi vijana wengi hawajiongezi. Unamiliki simu ya million mbili unashindwa kwenda Masaki na Oybay (among other places-kama huna uwezo wa kwenda nje kutembea) kuangalia majengo ya maana au mahoteli makubwa makubwa upitie uone kinachofanyika.
Penye miti hapana wajenzi
 
Umetiririka vizuri sana mkuu nimependa...ila ningekuomba ukipata muda fika Ardhi pale uone vijana wanachofanya nakuhakikishia utakuwa amazed, tatizo hayo yote huwa yanaishia kwenye makablasha tu. Tukija huku kwenye real world situation wengi huwa wana timiza matakwa ya ma clients.

Jambo moja unalotakiwa kujua ni kwamba architects wanatimiza matakwa ya clients hivo whatever the clients wants wanampatia na mengineyo yanakuwa ni uwezo binafsi au creativity ya architect.

Kwa ishu ya jengo la admistration block yao pale inaweza ikawa haina hyo creativity ya kuonyesha kwamba architects wazuri wa Tanzania wanatoka hapa lakini kwa wakati huo huo likawa limetimiza matakwa ya matumizi kwa nyanja karibia zote na hapo aliyesanifu hilo jengo anakuwa ametimiza wajibu wake.
 
Mkuu nakuelewa kabisa hoja yako. Na wala kuandika hivi siyo kwamba nadharau wasomi wa pale. Far from that. Ninachojaribu kuangalia ni namna tunaweza kuwasaidia vijana wetu wakawa creative katika kupambana na Changamoto za hii dunia inayobadilika kwa haraka mno. Na hatuwezi kufanikiwa kama vijana wetu wanasomea kwenye madarasa kama ya shule yangu ya msingi kijijini miaka hiyo...na leo unategemea aje ku-design majengo yanayoendana na changamoto za karne ya 21.

By the way mimi siyo Architect lakini napenda sana architecture. Hata nikisafiri nina-kabajeti ka kununua Architecture books and magazines! Kote nilikotembea nimejifunza kitu. I believe Architecture is not about drawing. It is about thinking! It is about imagination! It is about creativity. You have to have ideas before you pull your pencil to draw. And I may add. Passion! Mpaka leo naamini Architects you are blessed. You deal with people ambao hawana matatizo! Unlike lawyers. medical doctors etc! Clients amechuma millions (halali au kwa ufisadi) ..anakuja u-design his or her dream house! What a blessing? My question is: how do you achieve this kama hata hujui definition ya "quality"?

Mkuu..unajua wengine tumehangaika huko duniani sana..kwa hiyo maybe inawezekana tuna-demand standards za juu ambazo kwa lugha yetu ya kiTanzania tuliyozoea ni "haiwezekani kwa hapa bongo". But mimi ni katika wale wanaooamini kwamba we can have our own Zaha Hadid or Renzo Piano here in bongo. (I hope unajua kwamba Zaha ni mzaliwa wa Iraq na aliingia UK kutafuta maisha! Lakini angalia juhudi zilipomfikisha)

Again, ni kupeana challenge.

On a lighter note! Lakini Kiongozi tukubali tuu. Ukienda Ardhi mtu akakwambia this is a University where Architects, QSs etc are produced lazima utajiuliza mara mbili mbili. Ningetegemea hata kama Mshoro hana pesa lakini akipata hela kidogo..anahakikisha....zinaongea lugha ya kile chuo!

Pamoja sana Mkuu!
 
Well said mkuu...
 
Hello JF,

Nimeona mtandaoni, kuna Boards za Architecture, je Tanzania zipo?, I wish kama haipo, ianzishwe sasa wasanifu majengo wote waorodheshwe.

Pia wawe na uwezo wa kuweka portfolio za kazi walizofanya, ili mtu yeyote anaetembelea tovuti ya Board ajue amchague yupi na pia kuwe na sehemu ya rating/reviews za hao mafundi.
Usanifu Majengo (Architecture ) ni taaluma(profession).

Msanifu Majengo(Architect) ni Mtaaluma(professional) aliyesajiliwa na bodi ya wasinfu na wakadiriaji majengo

Unaweza kusoma architecture na ukagruaduate lakini usiwe architect

Marketing – kazi nyingi za professional kama lawyer , doctors, engineers na architects ni unethical kujitangaza katika mfumo wote wa matangazo, kazi zako ndio zinatakiwa zikutangaze , kushirika kwenye tenda mbali mbali kwa upande wa client wa mashirika ya serikali, ya umma au binasfi, na kwa upande wa individual client huwa tunagemea client networking yaani client anakuunganisha na client mwngine hivyo hivyo unatengeneza clients networks.

Client kama unatafuta architect- unashauri uangalie completed project sio picha tu au kazi za makaratasi unaweza unao kitu kizuri katika karatasi lakini physically majanga

Kupitia AQRB unaweza pata contact za individual architect pamoja firms kwa ushauri wasiliana architects kwa idadi utakayo weza tembelea project zao zilizo kamilika ukiwa satisfied chagua mmoja
 
Ipo inafanya kazi
 
mkuu nilikua nashauri hio board inaweza kabisa regulate wanachama wake wa act with intergrity,
yaani hakuna Architecture ambae ataweka kazi ambazo si zake,na akikiuka masharti then awe penalized,
hii database iwasaidia watu ku make choices,hamtaki kuwekwa hewani sababu mnazijua wenyewe.............tuko karne ya 21bado architect anaogopa kufanya business online?

n
 
labda udefine vizuri unamaana gani ya kufanya business online( mi nafikiria wewe unawaza marketing online, kupublish drawings katika website, facebook, instagram n.k kama ndio hivyo kampuni nyingi tu hapa zina website ambazo unaweza visit na ukaona wanachofanya lakini sio kudisplay kazi indetail )

kwa kifupi professional business sio kama biashara za vitu kama mashati unaanza kutengeza shati kwanza ndio unatufatu mteja, unahitajika kukaa kwanza na kuelewa hizi professional ambazo ziko regulated na boards kwa mfano daktari anatibu pale mgonjwa anapokuja au kama daktari mzuri utapata sifa zake kutoka kwa watu aliowatibu,hivyo hivyo kwa lawyer na hivyo hivyo architects pale anapopata client ndio kazi inapoanzia huanzi kazi kwa kubandika michoro kwenye website(gh kama mashati ili client waje.
katika professional ya architecture kila project iko unique kuanzia client mwenyewe, kimahitaji, kimazingira, technology , ukubwa, shape, viko vitu vingi vya kuaangalia, ndio maana watu wanadowload michoro still kujenga site inabidi ifanyiwe marekibisho na ipitishwe architect.
 
mmmnh mkuu mimi siko huko kwenye marketing,
niko kwenye uhakiki na uwazi wa huduma zenu,
huoni kukiwa na database inayowaorodhesha wasanifu majengo wote nchini kutakua na 'nidhamu' Fulani kwenu na kumpa mtu anayetaka kujenga chaguo,achague yupi/ramani/mchoro gani anaoupenda?
sasa unataka karne ya 21,tushikane mashati,tukaone nyumba ipi nzuri,uombe kujua ni nani alisanifu jengo? na wakati angeweza kuangalia portfolio za hao wasanifu majengo mbali mbali kwenye mtandao,kiganjani kwa simu?
trust me tukifanikiwa hili,mtapata client kibao,itakua inawabenefit wote,raia anayetaka kujenga na architecture atafaidika pia kutumia huo mtandao,(well wale marchitecture wazuri watapata oda,wale wengine ndio watakufa kibudu,lol)
 
Watanzania tuna ufinyu wa taarifa
Ni kweli, ila serikali pia na mashirika mengi hawatoi taarifa zao sehemu husika, sijui ni kutokujua au ubahili wa kuchapisha leaflets.
Ni lazima kila sehemu kama mahospitali, wizara zote na makampuni kuweka leaflets ambazo kuna anuani na maelezo ya mambo husika yanayoendelea

TRA nimeona wanajitahidi kwa leaflets lakini lazima iwe kila sehemu kuna vipeperushi kujua kinachoendelea kwa wakati huo.

Hata stand za bus yaani ni shida
 
Www.spacearchitects.co.tz EA.
Visit our website to see our works. Karibu kama una kazi . 0754542940
Hello JF,

Nimeona mtandaoni, kuna Boards za Architecture, je Tanzania zipo?, I wish kama haipo, ianzishwe sasa wasanifu majengo wote waorodheshwe.

Pia wawe na uwezo wa kuweka portfolio za kazi walizofanya, ili mtu yeyote anaetembelea tovuti ya Board ajue amchague yupi na pia kuwe na sehemu ya rating/reviews za hao mafundi.
 
mmmnh mkuu mimi siko huko kwenye marketing,
niko kwenye uhakiki na uwazi wa huduma zenu,
huoni kukiwa na database inayowaorodhesha wasanifu majengo wote nchini kutakua na 'nidhamu' Fulani kwenu na kumpa mtu anayetaka kujenga chaguo,achague yupi/ramani/mchoro gani anaoupenda,
sasa unataka karne ya 21,tushikane mashati,tukaone nyumba ipi nzuri,uombe kujua ni nani alisanifu jengo? na wakati angeweza kuangalia portfolio za hao wasanifu majengo mbali mbali kwenye mtandao,kiganjani kwa simu?
trust me tukifanikiwa hili,mtapata client kibao,itakua inawabenefit wote,raia anayetaka kujenga na architecture atafaidika pia kutumia huo mtandao,(well wale marchitecture wazuri watapata oda,wale wengine ndio watakufa kibudu,lol)

dada yangu watu wamekuambia kuna AQRB kuna data za architects na firm zote, kama hujui AQRB , kama hujui architects wewe unawaita marchitecture, mi sidhani kama naweza na kuelewesha biashara ya architecture inavyofanya kazi kwa sasa inahitaji muda kwa sababu ni pana sana na hii biashara sio michoro tu ina mambo mengi sana.
 
mkuu siku njema,sidhani kama tunaelewana,hio website nimeiingia,nimeona list ya ma architectures na mambo mengine,ila hamna kazi zao,wala feed back ya customers wao,ubaya huoni faida ya kitu ninachokisema,nimejaribu kukuelewesha nimeshindwa,ngoja niache,lol
 
unachotaka hakuna dunia nzima hata ARB architects registration board UK hawana
 
idea yako nzuri lakini iko kwenye architectural forums nyingi kwa miaka mingi jinsi gani ya kumarket architectural products hasa kwa wanaoanza kupractice
Sheria za hizi professions kama architecture n.a. law. Zinalimits advertisements. Unaruhusiwa kujitangaza Kwa njia ya kuelimisha jamii.
Kazi zako ndo advertisement.
 
Back
Top Bottom