Je Tanzania tutafaidika na gesi? Tayari sheria zina harufu za ufisadi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Tanzania tutafaidika na gesi? Tayari sheria zina harufu za ufisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Honolulu, Jul 23, 2012.

 1. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  KAMATI ya Nishati na Madini ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imekubali wazo la wadau kuhusu rasimu ya sheria ya gesi kuwa na mapungufu makubwa ikiwemo waziri kupewa madaraka makubwa ya maamuzi.
  Pia kamati hiyo imekubali kuwa sheria ya gesi haiwezi kupitishwa bungeni hadi hapo itakapofanyiwa marekebisho ambayo yatawanufaisha Watanzania wote na gesi badala ya wawekezaji au wajanja wachache.
  Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo katika ukumbi wa utawala bungeni jana, Mwenyekiti wa Mtandao usio wa Kiserikali wa Oil Natural Gas Environmental Alliance (ONGEA) Denis Mwendwa alisema kama rasimu hiyo itapitishwa bila marekebisho, haitakuwa na manufaa yoyote kwa Watanzania.
  Alisema moja ya mapungufu hayo ni namna ambavyo rasimu hiyo imetoa uhuru zaidi kwa Waziri wa Nishati na Madini katika kusaini mikataba mbalimbali bila ya kushauriana na wadau wengine.
  Alisema mbali na mamlaka makubwa ya waziri katika kusaini mikataba, pia mgawo wa rasilimali kwa wahusika wa maeneo ambako gesi inapatikana ni mdogo.
  “Moja ya mapungufu ya sheria hiyo ya gesi ni pamoja na madaraka makubwa ya waziri ambapo anaweza kusaini mkataba bila hata ya kuhojiwa na mtu yeyote, hivyo tumeona lazima tuzungumze na wahusika ili iweze kuboreshwa,’’ alisema Mwendwa.
  Alisema kuwa ONGEA kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanahabari wa Kupambana na uharibifu wa Mazingira (EMNet), walitumia wataalamu mbalimbali katika kuyabaini mapungufu hayo na ndio maana wakaona ni vema kuyafikisha kwa wahusika ili yaweze kufanyiwa kazi kabla ya kuanza kutumika kuwa sheria.
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Seleman Zedi, ambaye pia ni mbunge wa Bukene (CCM) alikiri kuyapokea maoni ya taasisi hizo na kueleza kuwa watawashawishi wabunge wengine kuipinga sheria hiyo kama haitafanyiwa marekebisho.
  Zedi alisema kwa sasa hakuna mkataba wowote ambao waziri anaweza kuingia kuhusu uchimbaji au utafutaji wa mafuta kwani hata kabla ya kupewa elimu hiyo ya jana, tayari kamati yake ilishabaini mapungufu kadhaa na hivyo wakataka serikali izuie uwekaji mikataba yoyote kwa sasa.
   
 2. M

  Mokte New Member

  #2
  Jul 23, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hoja zinazotolewa na Mwenyekiti wa Oil Natural Gas Environmental Alliance (ONGEA) hazina mshiko, zinawalakini mkubwa na pengineni kutokuelewa mambo muhimu katika Sheria inayokusudiwa kutungwa.Lengo kuu na Sheria ya Gesi inayokusudiwakutungwa ni kusimamia sekta ndogo ya gesi asili katika maeneo yakufatayo: i. Usafirishaji wa gesi asili; ii. Usambazaji wa gesi asili;iii. Hifadhi ya gesi asili iv. Matumizi ya gesi asili; v. Biashara ya gesi asili; na vi. Masuala mengine yanayiohusiana nagesi Majukumu ya Waziri mwenye dhamana nagesi asili (Powers of the Minister)ni kama ifuatavyo: i. Kuweka sera itakayosimamia sektandogo ya gesi asili; ii. Kuandaa Sheria, kanuni na miongozomabli mbali ya kusimamia sekta ndogo ya gesi asili;iii. Kufanya tathmini za mara kwa marakuhusu namna bora ya kuebndeleza sekta ndogo ya gesi; iv. Kufanya uchunguzi pale inapotokeamaafa katika mfumo wa gesi asili; v. Kusimamia upatikanaji wa gesi asiliwakati wa dharura.Hakuna mahali popote katika rasimuya Sheria ya Gesi ambapo Waziri amepewa mamlaka ya kuingia mikataba. Aidha, Sheriahii itakuwa tofauti sana na Sheria Ya Utafutaji na Uzalishaji wa Mafuta na gesiya mwaka 1980 ambayo ni Sheria yaMuungano inayosimamia utafutaji na uzaliaji wa mafuta na gesi nchini (Regulation of Upstream Operations).Sheria ya gesi inayokusudiwa kutungwa itasimamia DownstreamOperations. Ningeshauri Mwenyekiti wa ONGEA kabla ua kukurupuka atafute taarifa za msingi na apateuelewa wa jambo lenyewe kuliko kupotoshaWaheshimiwa Wabunge na Wananchi.Je Tutafaidika naGesi asili? Fadia za Gesi asili ni kubwasana ikiwa ni pamoja na: i. Upatikanaji wa nishati mbadala kwa ajiliya matumizi nchini. Tangu tuanze kutumia gesi mwaka 2004 Taifa limeokoa zaidiya US$ 2.0 billion ambazo zingetumika kununua mafuta ya petrol kutoka nje.Aidha zaidi ya asilimia 40 ya umeme unaozalishwa hivi sasa unatokana na gesiasili; ii. Upatikanaji wa ajira katika miradi namakampuni mbali mbali yanayojishughulisha na biashara ya gesi asili. iii. Kutunza mazingira kwa kuwa gesi nibora zaidi kimazingira ukilinganisha na mafuta ya petroli au makaa ya mawe; iv. Kutoka na na kuwepo na nishati ya gesinyingi na ya gharama nafuu sana, hii itavutia uwekezaji katika viwanda mbalimbali kama vile uzalishaji wa mbolea za chumvi chumvi, viwanda vya kutengelezakemikali kama methanol, plastics na kadhalika, viwanda vya chuma, aluminium,saruji, na vingine; v. Mapato yatokanayo na mauzo ya gesiyanatarajiwa kuwa makubwa sana kiasi kwamba taifa inabibi kuanza mikakakti yanamna bora ya kutumia mapato hayo;
   
 3. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  bado hizi zinaendelea kuwa habari mbaya. Mwalimu alikadiria umri wa maturity akitegemea kuwa kwa kuzuia exploration ya hizi rasilimali usifanyike mpaka at that ege of maturity. Sina uhakika kama alifikiria mbali sana zaidi ya umri miaka 50 lakini katika umri huo tumeonekana kuwa wapuuzi zaidi hata ya 'udogoni'!

  Sawa, waziri kapewa madaraka makubwa lakini wote tunajua yaliyotokea na yanayotokea, huwezi kumwamini hata kidogo! Je na hilo Bunge nalo unadhani linaaminika, ikiletwa sheria hata pale walipoandika 2+2 =22, baadhi yao watayaona hayo makosa lakini sheria inasema walio wengi na kwa hakika wataipitisha. Labda tuombe iletwe baada ya 2015 lakini tayari gesi inachimbwa hivi tunavyoongea

  We omba uhai na ukibahatika utalishuhudia hilo!
   
Loading...